Wanafunzi 6,000 wakaa sakafuni Kinondoni Dar es Salaam | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanafunzi 6,000 wakaa sakafuni Kinondoni Dar es Salaam

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Dec 25, 2010.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Dec 25, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  ZAIDI ya wanafunzi 6,000 wa shule za msingi katika Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni wanakaa chini kutokana na uhaba wa madawati.

  Aidha manispaa hiyo pia inakabiliwa na changamoto ya uhaba wa walimu katika shule za sekondari ambapo kwa sasa ina jumla ya walimu 800 tu, huku mahitaji yake yakiwa walimu 1,600.

  Akizungumza Dar es Salaam Meya wa Manispaa hiyo Yusuph Mwenda alisema kuwa yanahitajika madawati 3,200 ili kukidhi haja za wanafunzi wake, lakini kutokana na uhaba huo wanafunzi wengi wamekuwa wakikaa chini kutokana na ukosefu wa madawati.

  “Miezi sita ijayo hatutaki kusikia suala la watoto kukaa chini na kwa sasa tunakabiliana na changamoto hiyo ambapo sisi kama halmashauri tutatoa madawati 1,000 na mengine tutawaomba wadau wetu watuchangie na hatimaye kumaliza tatizo hili” alisema Mwenda.

  Alisema kupitia tamko la Rais Jakaya Kikwete la kuwapatia walimu watakaofundisha shule za sekondari ambao watatoka Chuo Kikuu Cha Dodoma itasaidia kukabiliana na changamoto ya ukosefu wa walimu wa sekondari katika manispaa hiyo.

  Alisema mikakati ya manispaa hiyo kwa miaka mitano ijayo kupitia mapato yake imepanga
  kujenga barabara zitakazosaidia kupunguza msongamano wa magari na kila kata kuwa na zahanati yake huku kila jimbo kuwa na hospitali yake.

  Alisema kwa upande wa watumishi watakaobainika kuhusika na uuzaji wa viwanja kiholela sheria itashika mkondo wake bila upendeleo.

  “Nitafanya kazi kwa kufuata utawala wa kisheria Katiba na kanuni zake bila itikadi za kichama na upendeleo wa aina yoyote bila ubaguzi “ alisema Mwenda.
   
 2. tzjamani

  tzjamani JF-Expert Member

  #2
  Dec 25, 2010
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 997
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hii ni aibu kwa sehemu kama kinondoni.... dawati ni sh ngapi?
  mbona kuna mikoa huwezi kuwakuta wanafunzi wanakaa chini uongozi wa kijiji tu unaweza kutatua hili.
   
Loading...