Wanafunzi 400 wajisaidia porini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanafunzi 400 wajisaidia porini

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Rutashubanyuma, Jan 17, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Jan 17, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,748
  Likes Received: 416,592
  Trophy Points: 280
  Wanafunzi 400 wajisaidia porini


  na Ambrose Wantaigwa, Tarime


  [​IMG] SHULE ya msingi Nyairoma iliyoko katika kata ya Sirari wilayani Tarime yenye wanafunzi zaidi ya 400 inakabiliwa na upungufu wa vyoo na kusababisha wanafunzi kujisaidia porini.
  Akizungumza na waandishi wa habari mwishoni mwa wiki shuleni hapo, mwenyekiti wa kijiji cha Sirari, Nyangoko Paulo, alisema atalazimika kuitisha kikao cha dharura cha serikali ya kijiji, ili kuwanusuru watoto hao kukumbwa na magonjwa ya mlipuko.
  “Wanafunzi wanalazimika kujisaidia vichakani ama katika vyoo vya shule jirani ya Sirari mita chache kutoka shuleni hapo hali inayowaweka katika hatari ya kukumbwa na magonjwa ya mlipuko kama vile kipindupindu,” alisema.
  Alisema uamuzi wa kuitisha kikao cha dharura cha serikali ya kijiji umechukuliwa baada ya kamati ya shule hiyo kushindwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo kutokana na ufinyu wa bajeti.
  Mmoja wa wazazi, Marwa Masese alitishia kuhamisha watoto wake wawili ikiwa shule hiyo haitachukua hatua za haraka kukabiliana na mazingira mabaya ya kiafya yaliyoko shuleni hapo ikiwa pamoja na kuchimbwa vyoo.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Jan 17, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,748
  Likes Received: 416,592
  Trophy Points: 280
  Hivi nguvukazi hiyo yote ya wananfunzi 400 kwa nini isitatue hili tatizo wajamani?
   
Loading...