Wanafunzi 40 warudishwa masomoni UDSM

bampami

JF-Expert Member
Nov 5, 2011
5,697
4,107
ONGOZI wa Chuo Kikuu cha
Dar es Salaam (UDSM)
umewarejesha masomoni
wanafunzi 40 kati ya 43
waliosimamishwa na
kuhojiwa kuhusu uchochezi wa vurugu na migomo chuoni
hapo kwa kuwa hawana
hatia. Aidha, umewakuta na kesi ya
kujibu wanafunzi watatu
waliohojiwa katika awamu
ya kwanza ya mahojiano
yanayoendelea kwenye Hoteli
ya Blue Pearl, Ubungo Dar es Salaam na kuagiza
wafikishwe mbele ya Kamati
ya Nidhamu ya Chuo hicho,
inayotarajiwa kukutana
Februari 28, mwaka huu. Akizungumza na gazeti hili
jana, Waziri Mkuu wa Serikali
ya Wanafunzi wa Chuo hicho
(DARUSO), Hassan Mustapha
alisema miongoni mwa
wanafunzi waliohojiwa na kukutwa na kesi ya kujibu ni
Katibu wa Bodi ya Daruso,
Shaibu Ado. “Lakini Ado anahaki ya
kuwasilisha ushahidi
mwingine kwa uongozi
unaoendesha mahojiano ili
hatua hiyo ya kujieleza kwa
Kamati ya Nidhamu itenguliwe, kwa hiyo
mabadiliko yanaweza
kutokea endapo atafanikiwa
kufanya hivyo kabla ya
tarehe ya kikao hicho,”
alisema Mustapha. Kwa mujibu wa Mustapha,
walioachiwa huru walielezwa
juu ya kutopatikana na hatia
wakati mahojiano ya kila
mmoja yalipomalizika. Kila
aliyehojiwa na kutakiwa kurejea chuoni aliambiwa
akachukue barua yake siku
iliyofuata, akiwemo Rais wa
Daruso, Kilawa Simon. Wengine waliotakiwa
kuendelea na masomo chuoni
hapo ni Naibu Spika wa Bunge
la Wanafunzi, Mwalo
Innocent, aliyefukuzwa
Januari 09, mwaka huu na mawaziri waliokuwa
wamesimamishwa; Yahaya
Kiyabo (Fedha) na Kanyondo
William (Mazingira na Maji). Naibu mawaziri
waliorejeshwa ni Janeth
Mwalupilo (Mawasiliano),
Erick Mfugale (Michezo),
Geofrey Steven (Katiba na
Sheria) na wengine ambao Mustapha alidai kutokumbuka
vizuri majina yao. “Hao ndio ninaowakumbuka
kwa sasa, wengine kama
Spika wa Bunge bado
hawajahojiwa. Lakini
mahojiano yanaendelea leo
sasa huenda akawepo kwenye awamu hiyo ya pili,”
alisema Mustapha. Uamuzi wa kufukuza
wanafunzi 13 Januari 9,
mwaka huu na
kuwasimamisha wengine 186,
ulitangazwa na Makamu
Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Rwekaza Mukandala baada ya
wanafunzi hao kutuhumiwa
kuchochea, kufanya vurugu
na migomo iliyolenga
kushinikiza wenzao 48
waliofukuzwa Desemba 14, mwaka jana warejeshwe bila
masharti.
 
Back
Top Bottom