Zurie
JF-Expert Member
- Jul 6, 2014
- 2,002
- 5,535
Wanafunzi 130 wa Chuo Kikuu cha Tumaini tawi la Mbeya kutofanya mtihani wa mwisho kwa kukosa usajili NACTE.
==================
Wanafunzi 130 wa Chuo cha Tumaini wako hatarini kuhitimu baada ya kuchelewa kusajiliwa NACTE.
Zaidi ya wanafunzi 130 wanaosomea kozi ya afya ya jamii katika Chuo kikuu cha Tumaini Makumira tawi la Mbeya wako hatarini kutofanya mitihani yao ya mwisho baada ya uongozi wa Chuo hicho kushindwa kukamilisha taratibu za kuwasajili kwa wakati kwenye kwenye Baraza la taifa la elimu ya ufundi,NACTE.
Wanafunzi wa Chuo kikuu cha Tumaini Makumira tawi la Mbeya ambao wamebakiza mwezi mmoja kuhitimu elimu yao chuoni hapo,wamekusanyika mbele ya majengo ya utawala ya chuo hicho na kupaza sauti zao wakitaka kujua hatma yao kuhusu usajili wao katika baraza la taifa la elimu ya ufundi,NACTE.
Katika kutaka kujua uongozi wa chuo hicho unazungumziaje suala hilo, ITV ikaingia ofisini kwa Makamu Mkuu wa chuo hicho,Mchungaji Mengele Mligo,lakini mchungaji huyo hakuwa tayari kuzungumza jambo lolote.
Kutokana na kutokuwa na uhakika wa kuhitimu elimu yao kwa amani,wanafunzi hao wamesikitishwa na uongozi wa chuo hicho kinachomilikiwa na Kanisa kwa vitendo wanavyofanyiwa,hivyo wakaiomba serikali kuingilia kati ili waweze kutendewa haki.
Chanzo: ITV