Wanafunzi 1,200 UDSM warudishwa nyumbani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanafunzi 1,200 UDSM warudishwa nyumbani

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Rutashubanyuma, Feb 10, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Feb 10, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,748
  Likes Received: 416,592
  Trophy Points: 280
  Wanafunzi 1,200 UDSM warudishwa nyumbani
  Wednesday, 09 February 2011 21:40

  ZAIDI ya wanafunzi 1,200 wa shada ya kwanza katika Koleji ya Uhandisi na Teknolojia (COET) ya chuo kikuu cha Dar es Salaam, wamesimamishwa masomo kwa muda usiojulikana baada ya kugoma kwa siku tano mfululizo na kufanya vurugu chuoni hapo.

  Hayo yalibainishwa jana jijini Dar es Salaam na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Profesa Rwekaza Mukandala, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari chuoni hapo.

  Kwa mujibu wa mukandara, kuanzia Februari 4, waka huu, kikundi cha wanafunzi wa koleji hiyo, wamekuwa wakivuruga madarasa, kuwatisha wahadhiri na kuwazuia wenzao kufanya mitihani.

  Alisema chanzo cha vurugu hizo, ni kushinikiza uongozi wa chuo, usimsimamishe masomo mwanafunzi mwenzao wa mwaka wa tatu Jamson Babala, ambaye Novemba 12 mwaka jana wakati wa mtihani wa marudio, alikutwa na karatasi kwenye chumba cha mtihani, na alipotakiwa kuitoa mwanafunzi huyo aliitafuna na kuimeza.

  “Kufuatana na taratibu za mtihani, msimamizi wa mtihani alimtaka mtahiniwa andike na kutia saini tamko kwenye kijitabu chake cha kujibia maswali kuthibitisha yaliyotokea, na mtahiniwa akafanya hivyo, kisha akaruhusiwa kuendelea na mtihani wake wa mwisho,” alisema Profesa Mukandala.

  Profesa Mukandala alisema suala hilo, lilifikishwa katika kikao cha kamati ya masomo ya shahada za awali.
  Alisema kamati hiyo, ilimuhoji mwanafunzi huyo pamoja na wasimamizi wa mitihani, na ilijiridhisha kuwa mwanafunzi huyo ana hatia na ilipendekeza kwa seneti ya chuo hicho, mwanafunzi huyo, achishwe masomo.

  Kwa mujibu wa Profesa Mukandala, baada ya mwanafunzi huyo kufahamishwa juu ya hatua hiyo, aliiandika barua kwa makamu mkuu wa chuo hicho, Profesa Mukandala kutaka kupunguziwa adhabu, lakini suala hilo lilikataliwa na wanafunzi wenzao baada ya kuanza mgomo, walisema hawawezi kusoma bila kuwa na mwenzao huyo.

  “Kitu walichokifanya hakikubaliki, hatuwezi kuendesha chuo kwa kushinikizwa,” alisema Profesa Mukandala.
  Alisema kutokana na hali hiyo, wanafunzi hao watarudi majumbani kwao kwa muda usiojulikana wakati taratibu za kubaini vinara wa vurugu hizo, zikiendelea.

  “Masharti ya kurudi na lini watarudi tutasema baadaye, sasa hivi kwanza tunataka amani irudi chuoni, watu waweze kuendelea na masomo yao, hatuwezi kuendesha chuo kwa kulindwa na polisi,” alisema Profesa Mukandala.
  Mara baada ya kupokea taarifa ya kufungwa kwa chuo, wanafunzi hao walikubaliana na uamuzi huo, na waliondoka katika chuo hicho kwa utulivu.

  Juzi Mwananchi ilishuhudia wanafunzi ha, wakifanya mandamano ndani ya chuo hicho huku wakikmba nyimbo za kejeli dhidi ya uamzi wa kumufukuza mwanafunzi huyo na kutishia kuwa wasingekuwa tayari kurudi darsanani hadi hapo atakaporudishwa.

  Pamoja na kufanyamaandamano hayo ya ndani pia badhi yao waliweka ulinzi mkali getini na kuzuia mtu yeyeto asiyehusika kuingia ndani ya Chuo hicho wakiwemo waliokuwa wakiingia kwa lengo la kujisomea.

  “Angusha kitambulisho chako hapa,eleza unataka kwenda wapi kufanya nini kama huna kitambulisho hakuna kuingia ndani na wale wanaokwenda kwenye kipindi leo hakuna masomo”alisikika mwanafunzi mmoja akipaza sauti getini hapo.

  Juzi Mwananchi ilishuhudia idadi kubwa ya wanafunzi ambao walionekana kutokubaliana na mgomo huo na kwamba wanafunzi hao walilazimika kwenda kukaa kwenye miti iliyoko nje ya geti la Chuo hicho na kujisomea.
  Habari hii imeandaliwa na Fredy Azzah,Geofrey Nyangóro na Edom Mwasamya  Comments
  0 #3 george chrissy 2011-02-10 08:21 siku zote matunda mabaya yanautambulisha mti kuwa mbaya, mti mbaya huzaaa matunda mabaya. hii ina maana kuwa migomo na maandamano karibu kote nchini hasa katika vyuo vikuu ni kutambulisha kuwa mfumo (system) mbovu kuanzia juu serikalini hadi uongozi wa juu wa vyuo.
  MWANAUDSM

  Quote

  +1 #2 avemaria 2011-02-10 07:47 Kwa kuwa viongozi wa nchi ni wezi, kila mtu anatamani kuwa mwizi katika kada yake. Ona huyu alitaka naye aibe majibu., mwacheni bana.
  Quote

  #1 Mhifadhi 2011-02-10 06:43 Nafikiri hii nayo inasikitisha kama lisemwalo ni la kweli kuwa msomi huyu alichungulia kwenye mtihani. Mimi nafikiri tunapozungumzia utawala wa sheria ni kuwa taratibu husika zichukue mkondo wake ila sidhani kama tatizo ni hilo tuu. Kutakuwa na mengi zaidi ambayo yamewasibu hawa wasomi mpaka wakaweka mgomo. Ama hata mpaka wakahamua kudanganya ktk mtihani. Mathalani waalimu kutowajibika ipasavyo kufundisha ama pia waalimu kutokuwa na uelewa wa yale wafundishayo vya kutosha. Haya nimekutana nayo na yanatokea kwa sasa. Inabidi pande zote ziangalie kiini haswa cha tatizo na sii kukimbilia kuzima moshi
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Feb 10, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,748
  Likes Received: 416,592
  Trophy Points: 280
  Wanafunzi 1,700 wasimamishwa vyuo vikuu


  *Wamo wa uandisi Mlimani, Teofilo Kisanji
  *16 wapandishwa kizimbani mkoani Mbeya


  Na Dunstan Bahai na Charles Mwakipesile

  WANAFUNZI wote 1,200 wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kitengo cha
  Uhandisi na Teknolojia (CoET) wamesimamishwa masomo kwa muda usiojulikana kutokana na kufanya vurugu chuoni hapo.

  Vurugu hizo zilizoanza Ijumaa wiki iliyopita, zilihusisha baadhi ya wanafunzi hao kuwapiga wenzao na kuwazuia wasiingie darasani wakiushinikiza uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kumrejesha mwanafunzi mwenzao wa mwaka wa nne, Jamson Babala aliyefukuzwa chuoni hapo kutokana na kukiuka taratibu na sheria za mitihani.

  Akizungumza jana na waandishi wa habari, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu, Profesa Rwekaza Mukandala, alisema hatua ya kuwasimamisha masomo wanafunzi hao imeamuliwa na vikao vya chuo vilivyokaa juzi na jana.

  "Suala hilo lilijadiliwa katika kikao cha dharura cha Baraza la Chuo kilichofanyika Februari 8, 2011. Baraza liliagiza kwamba ikiwa vurugu zinazoendelea hazitasitishwa, masomo ya shahada za kwanza katika koleji ya Uhandisi na Teknolojia yasimamishwe na wanafunzi husika waondolewe chuo," alisema Profesa Mukandala.

  Alisema kutokana na vurugu hizo zilizoanza Ijumaa wiki iliyopita, uongozi wa Chuo Kikuu umechukua uamuzi wa kutekeleza maelekezo hayo ya Baraza la Chuo ya kusimamisha masomo ya shahada za kwanza katika kitengo hicho cha Uhandisi na Teknolojia na kuwaondoa wanafunzi wote kuanzia wa mwaka wa kwanza hadi wa nne.

  Akizungumzia sababu za vurugu hizo, Profesa Mukandala alisema Novemba 12, mwaka jana wakati wa mitihani ya marudio, mwanafunzi Babala wa mwaka wa tatu, alikutwa na msimamizi wa mitihani akiwa na karatasi, kktu ambacho ni kinyume na taratibu za mitihani.

  Kwa mujibu wa Makamu Mkuu wa Chuo, mwanafunzi huyo baada ya kugundulika, aliamua kuitafuna na kuimeza karatasi hiyo lakini msimamizi alimtaka aandike na kutia saini tamko kwenye kitabu chake cha kujibia maswali kuthibitisha yaliyotokea, na alitii na kuendelea na mitihani yake.

  Alisema Disemba 6, mwaka jana suala hilo lilifikishwa katika Kamati ya Masomo ya Shahada za Awali ambako mtahiniwa huyo alikiri kufanya kosa hilo, ingawa alisema karatasi hiyo haikuwa na maandishi yoyote.

  "Pendekezo la kumwachisha masomo mwanafunzi huyo lilifikishwa katika Kikao cha Seneti Desemba 15, 2010 na kukubaliana na pendekezo hilo na hivyo kupitisha uamuzi wa kumuachisha masomo. Baraza la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam lilifahamishwa kuhusu uamuzi huo katika kikao chake kilichofanyika Januari 27, 2011 na likaridhia," alisema Profesa Mukandala.

  Alisema kutokana na uamuzi huo wa Seneta, Januari 17 mwaka huu mwanafunzi huyo alimuandikia barua Makamu Mkuu wa Chuo akiomba radhi kwa yaliyotokea na kuomba kupunguziwa adhabu hiyo na hasa ikizingatiwa kuwa ni mwanafunzi wa mwaka wa nne huku matokeo yake ya mitihani iliyopita yakiwa ni ya kuridhisha.

  "Kwa kuzingatia kanuni za mitihani na sheria nyingine, ombi hilo halikukubaliwa. Hivyo Jamson Babala akawa si mwanafunzi tena wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam," alisema.

  Profesa alisema kuwa kutokana na uamuzi huo, wanafunzi wenzake wa Uhandisi na Teknolojia waliamua kufanya vurugu tangu Ijumaa wiki iliyopita, wakiwapiga wenzao na wengine kujeruhiwa vibaya na kwamba kesi zao ziko polisi kwa taratibu za kisheria.

  Kuhusu masharti ya wanafunzi hao kurejea chuoni hapo, Profesa Mukandala alisema uchunguzi unaendelea kipindi watakachokuwa nje ya chuo na chuo kikijiridhisha kwa baadhi yao kutofanya vurugu, kitawarejesha.

  Hali ya usalama chuoni hapo na katika hosteli ya Mabibo iliboreshwa na Profesa alisema kuwa hakukuwa na vurugu hadi jana.

  Wasimamishwa Teofilo Kisanji

  Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji mkoani hapa kimewasimamisha wanachuo 508 wa mwaka wa tatu wanaosoma Historia kwa muda usiojulikana kwa kosa la kufanya vurugu na maandamano.

  Miongoni mwao 16 wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mbeya kwa kosa hilo.

  Akitangaza msimamo huo baada ya vikao vya uongozi wa chuo hicho kinachomilikiwa na Kanisa la Moravian Tanzania, Makamu Mkuu wa Chuo, Profesa Tuli Kasimoto alisema kuwa wanachuo hao waliamua kufanya vurugu kwa madai ya kutomtaka mwalimu wao somo hilo.

  Alisema kuwa wanachuo hao wakichochewa na morali wa kisiasa walianza vurugu hizo za kutaka mwalimu wa soimo la Historia aondolewa tangu January 25 ambapo baada ya kuona hawasikilizwi waliamua kuanzisha mgomo February 6, mwaka huu na kusababisha masomo kusimama kwa siku tatu.

  Profesa Kasimoto alisema kuwa wanachuo hao wakionesha kuwa walikuwa na ajenda ya siri waligoma kumsikiliza na kukubali kuwasikiliza vinara wa mgomo huo waliokuwa wanaongozwa na mmoja wa mwanachuo ambaye alikuwa akionesha wazi kuwa ni mwanasiasa.

  Alisema kuwa baada ya kuona kuwa jitihada zao za kutumia njia ya mazungumzo ya viongozi wa Serikali ya Wanachuo (TEKUSO) kushindikana uongozi ulitoa taarifa kwa Jeshi la Polisi na ndipo vurugu kubwa zilipoibuka kuanzia katika chuo hicho hadi barabara kuu wakati waandamanaji hao wakiongozana kutaka kwenda kwa mkuu
  wa mkoa.

  Makamu Mkuu wa chuo alisema kuwa tabia iliyooneshwa na wanchuo hao ya kutotaka kusikiliza uongozi wa chuo na kushikilia misimamo yao huku wakitamba kuwa mabadiliko lazima, uongozi ulichukua hatua na kumsimamisha mwalimu aliyekuwa analalamikiwa.

  "Unajua kama walivyotwambia sisi na hata mimi nashindwa kuelewa tatizo lao kwani kama ni mwalimu uongozi ulikwishamsimamisha mapema tangu tulipopata malalamiko yao, kwani ni hatari kumwacha mkufunzi asiyekubalika chuoni," alisema.

  Alisema kuwa walichoshangaa ni kuona pamoja na kuuambia uongozi wa serikali ya wanafunzi kuwa mwalimu anayelalamikiwa wamekwishamsimamisha, bado wanachuo hao waliendelea na msimamo na kuzuia wenzao waliokuwa wanataka kuendelea na masomo.

  Alisema kuwa baada ya mazungumzo baina yao, uongozi wa wanachuo na Mkuu wa Mkoa wamekubali kuwarudisha chuoni kwa masharti ya kufuata taratibu zilizowekwa na chuo ikiwa ni pamoja na wanachuo waliosimamishwa kutakiwa kuandika barua ya kuomba radhi na kujaza fomu maalumu.

  [​IMG]
   
 3. O

  ODILI SAMALU JF-Expert Member

  #3
  Apr 20, 2014
  Joined: Dec 13, 2013
  Messages: 1,261
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  hali iliwahi kuwa mbaya sana
   
 4. CHAMVIGA

  CHAMVIGA JF-Expert Member

  #4
  Apr 20, 2014
  Joined: Oct 5, 2012
  Messages: 7,694
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Daah!? Kuibia kwenye mtihani ni dhambi kubwa sana isiyosameheka. Japo inauma sana kijana wa mwaka wa tatu kufukuzwa akiwa amebakiza mwaka wake 1 au 2 lakini sheria msumeno.
   
Loading...