Wanachoogopa hasa ni nini?

Wanachoogopa hasa ni nini?

Gypsum Screw

JF-Expert Member
Joined
Jun 10, 2024
Posts
1,393
Reaction score
1,576
Tangu uhuru taifa limekuwa likiongozwa na wao. Kila siku hatuachi kukumbushwa juu ya mazuri na mema mengi sana ambayo wametufanyia (utadhani ni hisani). Hapa utasikia mambo kama tumejenga shule, tumejenga barabara, tumejenga hospitali, tumeleta umeme, tumeleta hiki na kile.

Sasa basi, katika muktadha huo wasiwasi wa mabadiliko ya kuruhusu watu wachague viongozi wanaowataka katika mazingira ya haki na usawa unatokea wapi?

Unasema umewapa watu maendeleo, huku makundi mbalimbali yakijitokeza kuchagiza na kumwagia sifa hata asizostahili yule mgombea aliyejipisha mwenyewe huko chama kinachotawala ili kuonesha kwamba wanampenda sana.

Sasa kama wameleta maendeleo mengi kiasi hiki na watu wanampenda sana mgombea aliyejipitisha mwenyewe huko chama kinachotawala, uoga wa kuacha watu wawachague kwa uhuru na haki ni wa nini?​
 
Tunakushukuru sana mama umetoa bilioni kadhaa kufanikisha hili na lile..umejaliwa moyo wa upendo Kwa watanzania..in chawa's voice
 
1747229080560.png
 
Hivi wasira yupo wapi? Game changer wao walimleta toka reserve
 
Tangu uhuru taifa limekuwa likiongozwa na wao. Kila siku hatuachi kukumbushwa juu ya mazuri na mema mengi sana ambayo wametufanyia (utadhani ni hisani). Hapa utasikia mambo kama tumejenga shule, tumejenga barabara, tumejenga hospitali, tumeleta umeme, tumeleta hiki na kile.

Sasa basi, katika muktadha huo wasiwasi wa mabadiliko ya kuruhusu watu wachague viongozi wanaowataka katika mazingira ya haki na usawa unatokea wapi?

Unasema umewapa watu maendeleo, huku makundi mbalimbali yakijitokeza kuchagiza na kumwagia sifa hata asizostahili yule mgombea aliyejipisha mwenyewe huko chama kinachotawala ili kuonesha kwamba wanampenda sana.

Sasa kama wameleta maendeleo mengi kiasi hiki na watu wanampenda sana mgombea aliyejipitisha mwenyewe huko chama kinachotawala, uoga wa kuacha watu wawachague kwa uhuru na haki ni wa nini?​
Malupulupu yao kuyeyuka- ndio Tatizo- ongezea hakuna kufukua makaburi. Chadema wawambie tu kwamba, malupulupu yao yataendelea kadi kifo chao, na madhambi yao hayatachunguzwa... huo ndio utakuwa mwanzo wa katiba mpya na Tume huru- Period
 
Back
Top Bottom