Wanachokwepa Waziri Ndalichako Na Naibu wake Hiki Hapa

Maistro 1

JF-Expert Member
Sep 4, 2015
422
181
Waziri wa elimu Prof. Joyce Ndalichako ameendeleza kile kile alichoanzisha naibu wake, Eng.Stella Manyanya ila yeye amekirekebisha kidogo tu, Eng. Stella Manyanya yeye alisema watakaongia darasa la III bila kujua kusoma na kuandika watawawajibisha walimu wakuu, yeye ameagiza darasa la II.

Mawaziri hawa wanashindwa kuweka wazi kwa umma kuwa mtoto asiyejua kusoma, kuandika na kuhesabu (kwa maana ya kujumulisha na kutoa) asiruhusiwe kuingia darsala la II (yaani akariri darasa la I) kwahiyo hii kazi wanawabebesha walimu wakuu na walimu wao.

Ila ukumbukwe kuwa kwa muda mrefu mfumo na sera yetu ya elimu hairusu watoto kukariri madarasa, watoto huwa wanaswagwa tu kuingia darasa jipya unapofika mwaka mpya wa masomo.

Sasa Waziri Joyce Ndalichako anajua kabisa akiagiza kuwa watoto wasiojua kusoma na kuandika wakiriri la darasa la I, karibia 90% ya watoto watakuwa wanakariri kwahiyo shule zetu kwa kuwa zina uwezo mdogo na vyumba vichache vya marasa zitashindwa kuwa accommodate watoto na idadi ya watoto wanao hitimu darasa la VII itashuka, na vile vile bajeti ya kuwasomesha hawa watoto wenye uwezo mdogo itakuwa kubwa.

Hii ndiyo sababu wanayokwepa, wanajua kutokana na umasikini na hali duni za watanzania wengi hata watoto wao wengi uwezo wa ufahamu wao ni mdogo kutokana na lishe duni na malezi yasiyo bora, kwahiyo wakiagiza kuwa wakariri darasa utakuwa mzigo mkubwa.

Kwahiyo wameamua kuwabebesha zigo walimu wakuu na walimu wao kwa vitisho. Si kweli kuwa kutojua kusoma na kuandika kunatokana uzembe wa walimu, hii mimi naipinga maana walimu wa shule za msingi wanafundisha sana na kwa wasio jua kuna hawa waratibu elimu wa kata wanawabana sana walimu na karibia kila wiki wanawakagua mara kwa mara na wanahakikisha hizo lesson plan na scheme of work zinaandaliwa kulingana syllabus na kuna baadhi ya shule za msingi watoto wanaingia darasani saa moja kamili asubuhi na hawa waratibu wanahakikisha walimu wanakuwepo na wana attend vipindi kama kawaida kuanzia hiyo saa moja asubuhi lakini ikifanyika assessment mwisho wa mwaka wengi wa watoto hawa huwa wanamaliza madarasa hawana chochote kwanini? uwezo wa ubungo wao ni mdogo.

Kwahiyo waziri asitoe vitisho kwa walimu wakuu yeye aagize tu mtoto ambaye atakuwa hajapata maarifa ya KKK vizuri (amei master KKK vizuri) akariri darasa la I na hii ndiyo iwe kichwa cha habari kwenye magazeti harafu aone outcomes na amini atasikitika mpaka atalia maana idadi kubwa ya watoto walewale watakariri darasa mwaka hadi mwaka.
 
Last edited:
Yani ukweli kama wataweka vizuri hali za walimu zikawa za kuridhisha mazingira mazuri na mishahara inayokidhi mahitaji yao wasiojua kusoma na kuandika watapungua sana au kuisha kabisa maana walimu watafundisha kwa moyo mmoja bila kufikiria mambo mengine
 
Yani ukweli kama wataweka vizuri hali za walimu zikawa za kuridhisha mazingira mazuri na mishahara inayokidhi mahitaji yao wasiojua kusoma na kuandika watapungua sana au kuisha kabisa maana walimu watafundisha kwa moyo mmoja bila kufikiria mambo mengine
ndugu yangu hamna mishahara wa maslahi duni kwa 'mateacher' ukweli tunaitaji kukagua uwezo wao na vyeti ni mada ndefu kiukweli, walimu kwa walimu tu wanashangaana uwezo wao, naamini hata ikiwa wanalipwa laki moja kwa saa 75% hali itabaki kama ilivyo!
 
Sio watoto wote wana uwezo wa kusoma hili nalipinga kabisa kuwalaumu waalimu ni kosa au niseme uelewa mdogo wa kutokujua kwa nini mtoto anashindwa kusoma na kuandika kwani wapo wenye learning difficulties, hao wanahitaji special schools na waalimu wenye uwezo wa kuwafundisha.

Mtoto anapigwa kwa kutokuelewa kusoma wakati tatizo ni ubongo hata umkate sikio na kumtisha kukata lingine bado utamaliza viungo vyote na bado hataelewa.

Tusionee waalimu wala wanafunzi ila watafutiwe special school hao wanafunzi na wataalamu wasijitoe ufahamu wafuatilie kwa kina zaidi
 
Wapeni walimu kipaumbele wasikilizeni maitaji yao alafu wazaz watoe ushirikiano kwa walimu sio kuwaingilia majukum yao sasa ivi wazaz nao wanajifanya walim
 
mfano! Darasa lina wanafunzi 40, 35 wanaweza kusoma, watano hawawezi bado watawawajibisha?

Kama ndiyo ni kwanini wakati hao 35 wanaoweza watakuwa wamefundishwa na walimu hao hao??
 
Mchakato wa elimu (utoaji wa maarifa na ujuzi) kwa mwanafunzi yeyote sio "one side process", kwamba ina muhusu mwalimu tu, hapana...hapana na tunakosea sana kufikiri hivyo hasa hasa ktk ngazi ya elimumsingi!!

Kwa nini alaumiwe mwalimu tu, tena hawa wakubwa wanam- pin elmwalimu mkuu tu eti ndiye awe wa kuwajibika iwapo atatokea mtoto mmoja au zaidi asiye jua kusoma na kuandika.

Kwani katika hili nafasi ya mzazi/mlezi ambaye in real sense ndiye mwenye mtoto iko wapi?

Kabla ya kumwajibisha huyu mwalimu mkuu, tunakuwa tumejiridhisha vya kutosha kuwa mzazi au mlezi wa mtoto huyu
yeye kwa upande wake anakuwa ametekeleza wajibu wake ipasavyo?

Je, tunatambua kuwa kuna wazazi/walezi wengine ni "destructive factor" kwa watoto wao wenyewe na kwamba hata mwalimu akalale nyumbani kwake na huyu mtoto akimfundisha usiku na mchana kamwe hawezi kujua chochote?

NA JE KABLA YA KUCHUKUA HATUA DHIDI YA MWALIMU, tunakuwa tumejiuliza na kujiridhisha kuwa serikali kwa upande wake nayo inakuwa imetekeleza wajibu wake?

Kwa nini walimu kila uchao wanailalamikia serikali? Je ktk mazingira haya tutarajie nini eti?

Kwa mtazamo wangu, inawezekana kabisa ukampeleka vyema punda hadi mtoni kwenda kunywa maji, lakini kamwe huwezi kumlazimisha kuyanywa maji hayo!!

Ualimu mkuu hausomewi. Kama ni suala la kufukuzana pasipo kila mdau wa elimu kwa maana ya jamii (wazazi/walezi, serikali na walimu wenyewe) kutimiza wajibu wake basi hakuna atakayeweza kuwa mwalimu mkuu!!
 
Last edited:
Mchakato wa elimu (utoaji wa maarifa na ujuzi) kwa mwanafunzi yeyote sio "one side process", kwamba ina muhusu mwalimu tu, hapana...hapana na tunakosea sana kufikiri hivyo hasa hasa ktk ngazi ya elimumsingi!!

Kwa nini alaumiwe mwalimu tu, tena hawa wakubwa wanam- pin elmwalimu mkuu tu eti ndiye awe wa kuwajibika iwapo atatokea mtoto mmoja au zaidi asiye jua kusoma na kuandika.

Kwani katika hili nafasi ya mzazi/mlezi ambaye in real sense ndiye mwenye mtoto iko wapi?

Huyu kabla mwalimu mkuu hajawajibishwa in case of this situation

Walimu chapeni kazi acheni mambo ya kulalamika. Huko mashuleni kuna walimu wengine wazembe sana; yaani wengine pamoja na kauli kali za viongozi bado wanapuuza tu na wanaendekeza ulevi tu.!
 
Una
Walimu chapeni kazi acheni mambo ya kulalamika. Huko mashuleni kuna walimu wengine wazembe sana; yaani wengine pamoja na kauli kali za viongozi bado wanapuuza tu na wanaendekeza ulevi tu.!
Unatukosea adabu wengine hata pombe hatuijui ina radha gani. Ukwel ni huu boresheni mazingira ya kufundisha na kufundishia. Hvi salary ya laki tano bila posho jamani na hali ya maisha mnaijua plus overcrowed classroom, capability of individual child, mitaala nyanya, hakuna madawati, watoto hawali shuleni n.k halafu utegemee hayo mnayoyataka?. Wajikite kutatua changamoto hayo mengine yatakuja yenyewe
 
Walimu chapeni kazi acheni mambo ya kulalamika. Huko mashuleni kuna walimu wengine wazembe sana; yaani wengine pamoja na kauli kali za viongozi bado wanapuuza tu na wanaendekeza ulevi tu.!

Unakosea sana unapo "generalize" mambo. Haiwezekani ktk shule yenye walimi 20, wawili au mmoja akawa mlevi basi iathiri utendaji kazi wa wengine woote!!

Na ukumbuke kuwa walevi wako ktk kila sekta ya utendaji na haiwezi kuwa kigezo kikubwa na pekee cha watoto kumaliza shule wakiwa hawajui kusoma na kuandika!

Fikiri ukiwa nje ya boksi mkubwa, fanya research kisha njoo na arguments zenye nguvu juu ya hili!!
 
Last edited:
Walimu chapeni kazi acheni mambo ya kulalamika. Huko mashuleni kuna walimu wengine wazembe sana; yaani wengine pamoja na kauli kali za viongozi bado wanapuuza tu na wanaendekeza ulevi tu.!
Leta takwimu za hao walimu wazembe na walevi kama hautaibika
 
Kuna mambo mengi ya kuangalia kwa undani na umakini. Jambo la kwanza ni background ya mwanafunzi. Je mwanafunzi huyu anapata chakula nyumbani walau chai asubuhi kabla ya kwenda shuleni? Safari ya kwenda shuleni haimchoshi? Anapotoka nyumbani hali ikoje? Jambo la pili anapofika shuleni mazingira ya usomaji na ujifunzaji yakoje? Je kuna vifaa vya kutosha kujifunzia na kufundishia? Shuleni kuna chakula? Tatu kuna vitu vinavyopoteza muda mwingi sana wa wanafunzi. Mfano michezo. Micheo hii ni vyema ikawepo lkn siku za masomo zizingatiwe. Mfano sekondari siku za
kusoma ni 196 ktk mwaka. Hapo siku za mitihani ni wiki mbili tu yaani siku kumi tu kwa mwaka. Pia shughuli za Umisetta ziko hapo hapo kwenye siku za masomo. Jambo la nne ni swala la vitabu vya kufundishia na kujifunzia. Hakuna utaratibu katika vitabu hivi. Ndiyo maana kila shule inatumia kitabu chake. Wakati mwingine kuna makosa mengi kwenye vitabu hivi mfano kitabu kinachoitwa geography in focus book one kinasema kuna 8 planets! Kitabu hiki kimepewa nembo ya EMAC. Maana yake kinafaa kutumika kwa elimu yetu. Tano maslahi ya walimu. Hakuna semina za mafunzo kazini. Semina hizi waliachiwa wakuu wa shule wakawa wanazifanya wanavyojisikia. Wanasingizia hela hakuna lkn taratibu zinasema kuna asilimia kwenye ada ilitakiwa kufanya shughuli hii. Pia madeni mengi wanayoidai serikali n.k.
 
Walimu chapeni kazi acheni mambo ya kulalamika. Huko mashuleni kuna walimu wengine wazembe sana; yaani wengine pamoja na kauli kali za viongozi bado wanapuuza tu na wanaendekeza ulevi tu.!
Wakati nipo shule ya Msingi nilifundishwa na mwalimu mlevi kabisa lakini ndiye tuliyekuwa tunamuelewa kupita wote, sio kila mlevi hawezi kafanya kazi bora...waiter lete baridi.
 
Huku walayani kwetu walimu wa k3 walipata semina,na pia wa masomo mengine,tusilaumu sana walimu.
 
ndugu yangu hamna mishahara wa maslahi duni kwa 'mateacher' ukweli tunaitaji kukagua uwezo wao na vyeti ni mada ndefu kiukweli, walimu kwa walimu tu wanashangaana uwezo wao, naamini hata ikiwa wanalipwa laki moja kwa saa 75% hali itabaki kama ilivyo!
Hili umenena mkuu
 
Niliona kupitia television huko Nkwimba, Mwanza walimu takribani 300 wa shule za msingi na sekondari wakiwa wameandamana na "kuvamia" ofisi ya DC na DED wakidai zaidi ya Tshs 500,000,000/= (milioni mia tano) kama malimbikizo ya mishahara, likizo, matibabu, uhamisho nk

Mkurugenzi alipohojiwa akasema wamepokea 80,000,000 na tayari wameshazilipa kwa walimu. Sasa hebu tufikiri madeni ya walimu ni Tshs. milioni 500 serikali inapeleka milioni 80 tu, wapi na wapi hili??

Tafsiri yake hapa ni kwamba kuna baadhi watalipwa na wengine kuachwa and yet utegemee walimu hawa wawe na morali ya kufanya kazi yao kwa ufasaha!!...Hapa ni kujidanganya tu.

Na tukumbuke hizi milioni 500 ni madai ya walimu wa wilaya moja tu ya Nkwimba huko Mwanza. Je katika wilaya zaidi ya 140 za Tanzania yote wanaidai serikali hii kiasi gani?

Ndiyo maana tunasema, uchunguzi ufanyike ili ijulikane ni kwa nini walimu wanafanya kazi zao kwa madeni yasiyolipwa miaka na miaka? Hakuna fedha au nini? Kama zipo huwa zinakwenda wapi zisiwafikie walimu walengwa?.....Something is wrong somewhere ktk sekta ya elimu na suluhisho lake si kutishia kufukuza watu!!!

Tumuulize huyu Waziri Ndalichako, yeye kapata appointment a week ago ya kuwa Waziri. Hebu atuambie amelipwa haki zake au bado ni deni ambalo halijulikani litalipwa lini??
 
Last edited:
Uwezo wa walimu ndo shiida, tatizo si mishahara duni acheni visingizio




Hata kumfundisha mtoto kusoma huyu mwalimmu hana uwezo??
 
Back
Top Bottom