Wanachama wote CCM wahamia CUF

Wanachama wote CCM wahamia CUF

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Posts
15,860
Reaction score
5,803
SIASA
Na Christopher Lilai, Liwale

Posted Jumatatu,Decemba31 2012 saa 10:43 AM

KWA UFUPI

Hayo yalitokea kwenye sherehe ya kumpongeza mgombea wa CUF, Jafari Nyimage aliyeshinda udiwani katika uchaguzi uliofanyika Novemba 28.



CHAMA cha Wananchi (CUF) Wilaya ya Liwale, Mkoa wa Lindi, kimevunja kambi iliyokuwa inategemewa na Chama Cha Mapinduzi ya Kijiji Cha Mkundi, kata ya Makata baada ya wanachama wote wa tawi hilo kujiunga CUF.

Wanachama hao wapatao 310 wa kijiji hicho ambacho kilikuwa kinafahamika kwa jina la utani la Dodoma ikiwa na maana ya makao makuu ya chama tawala walikabidhi kadi za CCM ili wakabidhiwe za CUF na Mjumbe wa Baraza la Ushauri Taifa la CUF ambaye pia ni Mbunge wa Lindi Mjini, Salum Barwany.

Hayo yalitokea kwenye sherehe ya kumpongeza mgombea wa CUF, Jafari Nyimage aliyeshinda udiwani katika uchaguzi uliofanyika Novemba 28.

Akikabidhiwa kadi ya CUF baada ya kukabidhi kadi ya CCM kwa niaba ya wanachama wengine, aliyekuwa Mwenyekiti wa tawi hilo la CCM, Jafari Masura alisema wameamua kujiunga na CUF kutokana na matamko ya viongozi wa wilaya wa CCM ambapo alidai kuwa mbunge wa jimbo hilo alipofanya ziara kwenye kijiji hicho mara baada ya matokeo ya uchaguzi mdogo aliwafananisha wakazi wa kijiji na mbuzi aliyepotea.

"Kauli ya mbunge wetu aliyoitoa mwezi uliopita ya kutufananisha na mbuzi aliyepotea na kudai amekuja kuwatafuta kutokana na kumpatia udiwani mgombea wa CUF ilituudhi hivyo tumeamua kukihama chama hicho"alisema Masura huku akishangiliwa na umati mkubwa wa wananchi kutoka maeneo mbalimbali ya kata hiyo.

Akiwakaribisha wanachama hao wapya waliohamia kutoa CCM mbele ya wanachama na wapenzi wa chama hicho, Barwan aliwashukuru kwa kuamua kujiunga na chama na kuahidi kufanya kila linalowezekana kushirikiana katika harakati za maendeleo.

"Sasa hivi uelewa wa wananchi juu ya mfumo wa vyama vingi umeongezeka sana kwani miaka ya nyuma ilikuwa vigumu kukuta umati mkubwa kama huu kwenye mikutano ya nyama vya upinzani na hii ilitokana propaganda za viongozi wa chama tawala ambao walidai upinzani ungeweza kusababisha vita," alisema Barwany.

 
Samahanini sina cha kupost ila nilisoma vibaya jina la kijiji. Kumbe ni mkundi mimi nilifikiri kuna sifuri mwisho, yaani o713
 
Wenyewivu wajinyonge! CDM wanapenda kusifiwa utadhani vigori!kuuumbe sura baaaya,anaenda utadhani anauya! Lo!
 
Mama SALMA na MEMBE waanze kulia; Wanaweza wasilichukue JIMBO lao hilo la LINDI likaangukia UPINZANI!!!

NA JINSI WALIVYOJIJAZA CCM-NEC; TOBA, walikuwa wanawazia hiyo GAS ya MTWARA...
 
Back
Top Bottom