Wanachama wote CCM wahamia CUF

Wanachama wote CCM wahamia CUF

Ukoo Flani

Senior Member
Joined
Sep 1, 2011
Posts
156
Reaction score
41
CHAMA- cha Wananchi (CUF) Wilaya ya Liwale, Mkoa wa Lindi, kimevunja kambi iliyokuwa inategemewa na Chama Cha Mapinduzi ya Kijiji Cha Mkundi, kata- ya Makata baada ya wanachama wote wa tawi hilo kujiunga CUF.

Wanachama hao wapatao 310- wa kijiji hicho ambacho kilikuwa kinafahamika kwa jina la utani la Dodoma ikiwa na maana ya makao makuu ya chama- tawala walikabidhi kadi za CCM ili wakabidhiwe za CUF na Mjumbe wa Baraza la Ushauri- Taifa la CUF ambaye pia ni Mbunge wa Lindi Mjini, Salum Barwany.

Hayo yalitokea kwenye sherehe ya kumpongeza mgombea wa CUF, Jafari Nyimage aliyeshinda udiwani katika uchaguzi uliofanyika Novemba 28.

Akikabidhiwa- kadi ya CUF baada ya kukabidhi kadi ya CCM kwa niaba ya wanachama wengine, aliyekuwa Mwenyekiti wa tawi hilo la CCM, Jafari Masura alisema- wameamua kujiunga na CUF kutokana na matamko ya viongozi wa wilaya wa CCM ambapo alidai kuwa mbunge wa jimbo hilo alipofanya ziara kwenye kijiji hicho mara baada ya matokeo ya uchaguzi mdogo aliwafananisha wakazi wa kijiji na mbuzi aliyepotea.

“Kauli ya mbunge wetu aliyoitoa mwezi uliopita ya kutufananisha na mbuzi aliyepotea na kudai amekuja kuwatafuta kutokana- na kumpatia udiwani mgombea wa CUF ilituudhi hivyo tumeamua kukihama chama hicho”alisema Masura huku akishangiliwa na umati mkubwa wa wananchi kutoka maeneo mbalimbali ya kata hiyo.

Akiwakaribisha wanachama hao wapya waliohamia kutoa CCM mbele ya wanachama na wapenzi wa chama hicho, Barwan aliwashukuru kwa kuamua kujiunga na chama na kuahidi kufanya kila linalowezekana kushirikiana katika harakati za maendeleo.

“Sasa hivi uelewa wa wananchi juu ya mfumo wa vyama vingi umeongezeka sana kwani miaka ya nyuma ilikuwa vigumu kukuta umati mkubwa- kama huu kwenye mikutano ya nyama vya upinzani na hii ilitokana propaganda za viongozi wa chama tawala ambao walidai upinzani ungeweza kusababisha vita,” alisema Barwany.

http://www.mwananchi.co.tz/habari/Siasa/-/1597332/1654696/-/bpbr92z/-/index.html

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Sasa hao wamehama au wamebadili msimamo kwa muda? Maana CUF na CCM ni chama kimoja.
 
Cuf nacho ni chama cha kuchukua wanachama wa ccm hao ni nyumba ndogo yetu au mmesahau jamani hilo wala haliumizi kichwa kabisa,
 
Wapinzani tuko cdm karibuni huku ,huko mmebadili chumba tu nyumba ni ileile yenye nyuki wale wale
 
Wamehamia Cuf, mi nikisikia mwanachama amehama ccm amehamia Tlp, udp, cuf, sau nk inanipa shida kumwamini, mnisamehe tu..
 
Siamini kama kweli uelewi maana ya upingani kwenye medani za siasa!

Ni muhimu kuelewa upinzani aliokusudia kwa vile amesema wako CDM tu! Hata protestants maana yake ni wapinzani, ajieakawa mfano wa hao. Maana amewatenga wengine kuwa sio wapinzani.
 
wapo sawa kote ni upinzani hata kama ni nyumba moja hujaona watu wakaa nyumba moja hata maji hawaombani
 
...ahaaa ahaaa ahaaa...watoto wamemwacha baba sebureni wakakimbilia jikoni kwa mama...
 
Mpinzani wa nini?

wapinzani wa mfumo mbovu wa utawala,umasikini,rushwa,njaa,ufisadi,ufuska,wizi,ulafi na uchu wa madaraka,matibabu duni,elimu duni..................chochote chenye matokeo hasi kwa watz tunapinga.........huwezi amini hata washabikia mifumo mibovu kama wewe tunawapinga...........karibu uwanjani ndugu.
 
Watahama Sana but wakifika CDM ndo ilipo gereji ya magari mabovu. Yanakarabatiwa, yanapakwa rangi yanaingia barabarani na kuyatesa magari yanayodhaniwa kuwa ni mapya ati kwa rangi tu.
 
Back
Top Bottom