kalulukalunde
JF-Expert Member
- May 27, 2016
- 1,056
- 1,086
MIGOGORO ya uongozi imekuwa sehemu ya maisha ya vyama vya siasa nchini tangu mfumo wa vyama vingi uliporuhusiwa tena mwaka 1992. Mara baada ya sheria ya mfumo wa vyama vingi kupitishwa, muungano wa vuguvugu la mageuzi uliojulikana kama NCCR ulimeguka katika vipande viwili, upande mmoja ukiongozwa na Mabere Marando aliyekuwa Mwenyekiti na Prince Bagenda kama Katibu Mkuu.
Upande mwingine uliongozwa na Chifu Abdala Fundikira kama mwenyekiti na Christopher Kasanga Tumbo kama Katibu Mkuu. Kundi la Mabere Marando ndilo lilikuja kuzaa chama cha NCCR-Mageuzi na kundi la Chifu Fundikira likazaa chama cha UMD (United Movement for Democracy).
Baada ya uchaguzi wa mwaka 1995, chama cha NCCR-Mageuzi kilikumbwa na mgogoro mkubwa ukimhusisha Augustino Lyatonga Mrema kama Mwenyekiti na Mabere Marando kama Katibu Mkuu. Hii ilikuwa ni baada ya kumkaribisha na kumpisha Mrema kuwa mgombea na Mwenyekiti wa chama hicho. Mgogoro huu ulikitafuna chama cha NCCR-Mageuzi kwa miaka mingi na athari zake bado zinaendelea kuonekana hadi leo.
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) pia kimeshakumbwa na migogoro kadhaa ya uongozi. Migogoro hii ni pamoja na ni ile iliyomhusisha Mwenyekiti Mbowe dhidi ya Makamu Mwenyekiti Amani Kabourou, Mwenyekiti Freeman Mbowe dhidi ya Makamu Mwenyekiti Chacha Wangwe (Marehemu), na hivi karibuni kabisa ni Mwenyekiti Mbowe dhidi ya aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Zitto Kabwe.
Chama cha Wananchi (CUF) kimeshakumbwa na migogoro ya uongozi zaidi ya mara nne, ukiwahusisha Maalimu Seif dhidi ya James Mapalala, Maalim Seif dhidi ya Hamad Rashid, Maalimu Seif dhidi ya Naila Jidawi, na hivi karibuni kabisa Maalim Seif dhidi ya Profesa Ibrahim Lipumba.
Huu mgogoro wa sasa ndani ya CUF unalingana kwa kiasi kikubwa na mgogoro wa NCCR-Mageuzi wa mwaka 1995 uliosababishwa na chama hicho kumkaribisha Mrema na baadaye kumpisha uenyekiti. Kama ilivyokuwa kwa NCCR-Mageuzi, mgogoro wa sasa wa CUF umesababishwa na tofauti za viongozi wakuu wa chama hicho kuhusu uamuzi wa vyama vya UKAWA kumpa nafasi Edward Lowassa kuwa mgombea urais wa muungano huo mwaka 2015.
Migogoro yote hii imekuwa na hitimisho linalofanana ambalo ni baadhi ya viongozi na wale wanaoonekana kuwa ni wafuasi wao kufukuzwa. Hakuna historia katika vyama hivi ya kufanikiwa kutatua migogoro yao kwa njia ya maridhiano. Kibaya zaidi ni kwamba ugomvi baina ya viongozi hautokani na mgongano wa kifikra za kifalsafa na kisera, bali unatokana na kuzongania madaraka.
Kwa ujumla, kila mgogoro una chanzo chake. Lakini chanzo kikubwa kabisa cha migogoro ndani ya vyama vya siasa vya upinzani ni kuwa na wafuasi wengi wa viongozi na wafuasi wachache kabisa wa misingi ya chama. Matokeo yake inapotokea viongozi kupishana, wafuasi hujikuta wakigawanyika kuwafuata viongozi hao. Kwa maneno mengine ni kwamba vyama vya siasa vimejaa wafuasi wengi ambao ni wafia viongozi lakini wachache mno walio wafia chama na misingi yake.
Ni kwa sababu ya kuwa na wafuasi waliojikita kufia viongozi badala ya kufia misingi ya vyama vyao, mara zote migogoro ya chama inapoibuka huwa tunasikia wafuasi wakigawanywa katika makundi ya viongozi wanaokasimiana.
Ni nadra kusikia wafuasi wakijadili kuhusu taratibu za kikatiba katika vyama vyao zinasema nini kuhusu jambo husika. Mara zote mijadala hutawaliwa na yupi kati ya viongozi wanaogombana ni mzalendo na yupi anatumika na dola au Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Kwa maneno mengine ni kwamba vyama havina walinzi. Walinzi waliopo ni wa viongozi.
Tukirejea katika mgogoro wa uongozi unaoendelea ndani ya CUF, kuna mambo matatu muhimu ya kuzingatia. Mosi, Profesa Ibrahimu Lipumba alitoa notisi ya kutaka kujiuzulu nafasi ya uenyekiti wa chama chake ikiwa ni hatua ya kupinga uamuzi wa viongozi wenzake ndani ya UKAWA kumkaribisha Lowassa kuwa mgombea wa urais.
Sababu alizotoa ni kwamba uamuzi wa kumsimamisha Lowassa ulikuwa unakwenda kinyume na misingi mama ya kuanzishwa kwa UKAWA, ambayo ni kupiga vita ufisadi na kupigania Katiba mpya inayoakisi maoni ya wananchi kama yalivyokuwa yamewasilishwa ndani ya Rasimu ya Katiba iliyopendekezwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
Hatua hii ilitokana na ukweli kwamba viongozi waandamizi katika vyama vinavyounda UKAWA, wakiwemo Profesa Lipumba na Dk. Wilbrod Slaa, walikuwa wametumia miaka mingi kumtangaza Lowassa kama ndiyo alama kuu ya ufisadi Tanzania. Kwa hiyo, kumsimamisha mtu kama huyu kuwa mgombea wao ilikuwa ni kama kujitukana na kusaliti vita dhidi ya ufisadi. Aidha, Lowassa alikuwa anajulikana kama kinara wa kupinga muungano wa serikali tatu ambo ndio ilikuwa kiini cha Rasimu ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
Hivyo basi, uamuzi wa kujiuzulu kwa Profesa Lipumba ulijengwa katika misingi ya kuanzishwa kwa UKAWA. Hata hivyo viongozi wenzake waliamua kumeza maneno yao ya miaka mingi na kumkumbatia Lowassa wakiamini kwamba angewawezesha kushinda nafasi ya urais, kitu ambacho kingefuta fedheha ya kumkaribisha ndani ya UKAWA. Hili halikutokea kwa sababu Lowassa hakushinda nafasi ya urais. Ndiyo kusema, katika hali ya kawaida, ile fedheha ilibaki ndani ya viongozi wa UKAWA.
Katika nchi zilizostaarabika kidemokrasia, baada ya kushindwa uchaguzi ingetosha kabisa kwa viongozi wa UKAWA kujiuzulu nafasi zao ili kunusuru taswira ya vyama vyao na kuwapisha wengine kuongoza vyama hivyo.
Lakini hili si jambo linalotarajiwa katika siasa zetu za Afrika zilizojengwa katika misingi ya kusaka madaraka badala ya falsafa na maono ya maendeleo ya kijamii, kiuchumi na kisiasa. Haishangazi basi kuona kwamba viongozi wa vyama hivi wameweza kuimeza fedheha na wanaendelea kudunda bila aibu wakiambatana na mtu waliyemnyanyasa miaka nenda rudi. Kinachoendelea sasa ni Lowassa kuwatesa viongozi wa UKAWA kama wao walivyomtesa kwa miaka mingi. Hili ni jinamizi ambalo tutaendelea kulishuhudia ndani ya vyama vya UKAWA katika miaka kadhaa ijayo.
Swali ambalo linaendelea kuumiza vichwa vya wafuatiliaji wa mambo ya siasa nchini ni je, ilikuwa sahihi kwa Profesa Lipumba kughairi uamuzi wake wa kujiuzulu? Unaweza kujibu swali hili kwa kuzingatia muktadha wa kisiasa, kisheria na utashi wa Profesa Lipumba.
Katika kuzingatia muktadha wa kisiasa tunaangalia ni nani wanaomuunga mkono, na nani wanaompinga Profesa Lipumba ndani na nje ya CUF. Ni wazi kwamba kuna watu wanaomuunga mkono Profesa Lipumba ndani ya CUF ambao ndiyo imekuwa hoja yake ya kurejea katika nafasi yake. Tusichojua kwa hakika ni akina nani hao na wapo wengi kiasi gani.
Hapa ndipo nafasi ya wanachama ilipohitajika. Ilitakiwa mazingira ya haki na kidemokrasia yawepo ili wanachama wa CUF kupitia vikao vyao wafanye maamuzi kwa njia ya kura. Hili halikufanyika. Matokeo yake Mkutano Mkuu wa tarehe 21 Agosti 2016 ukaandaliwa katika mazingira yaleyale ya ujanjaujanja tuliouzoea katika vyama vya siasa Tanzania.
Kwa mfano, badala ya kura ya siri kama ambayo taratibu za kidemokrasia zinataka, na kama ambavyo vyama vya UKAWA wamekuwa wakipigania kutumika katika maamuzi nyeti, ikaandaliwa kura ya wazi ya kunyoosha mikono huku Profesa Lipumba mwenyewe akiwa si mwalikwa katika kikao husika. Ni wazi kwamba kura ya namna hii iliandaliwa ili kuhalalisha nia ovu waliokuwa nao viongozi dhidi ya kiongozi mwenzao.
Kisheria, Msajili wa Vyama vya Siasa ameshalitolea ufafanuzi jambo hili kwa kirefu sana katika barua yake kwa viongozi wa CUF yenye kurasa tisa 9. Kwa kifupi, tafsiri ya barua ya msajili ni kwamba, kwa mujibu wa Katiba ya CUF (Ibara 117(2), mkutano mkuu wa CUF haujawahi kukubali uamuzi wake wa kujiuzulu.
Kufuatia barua yake ya kutengua uamuzi wake wa kujiuzulu, mkutano mkuu haukuwa na haja tena ya kujadili barua yake ya kujiuzulu. Kwa sababu hii, kisheria na kuwa mujibu wa Katiba ya CUF, Profesa Lipumba bado ni mwenyekiti wa CUF.
Aidha, tafsiri ya msajili ni kwamba Kikao cha Baraza Kuu la Uongozi la Taifa kilichokaa tarehe 28 Agosti 2018 hakikuwa na mamlaka ya kufanya maamuzi waliyoyafanya, ikiwemo kuteua viongozi wa kitaifa, wakiwemo Julius Mtatiro kama Kaimu Mwenyekiti na Joram Bashange kama Kaimu Naibu Katibu Mkuu (Bara).
Najua kwamba, kama ilivyozoeleka, Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif, na viongozi wenzake walioondolewa uhalali wa kisheria, pamoja na wale wanaowaunga mkono, wataudhalilisha uamuzi na tafsiri ya msajili wa vyama vya siasa na kumuona kama mtu aliyetumwa na wapinzani wao kuwadhoofisha.
Lakini ni vizuri tukakumbusha kwamba ni ofisi hii ya Msajili iliyowahi kuamua kesi kati ya Maalim Seif dhidi ya akina Hamad Rashid na James Mapalala. Wakati huo ofisi ya Msajili ilitenda haki kwa kuwa uamuzi ulikuwa upande wa Maalim Seif!!
Pamoja na yote, maamuzi ya chama cha siasa yanapaswa kufanyika kisiasa ili yawe na uhalali wa kisiasa. Uhalali wa viongozi wa kisiasa haujengwi kisheria, bali unajengwa kisiasa. Kwa sasa, viongozi wa pande zote katika huu mgogoro wana uhalali wa kisiasa kutokana na idadi kubwa ya wafuasi walio nao ndani ya chama chao.
Kwa mujibu wa barua ya msajili, wajumbe 216 wa Bara kati ya wajumbe 348 waliohudhuria Mkutano Mkuu wa tarehe 21 Agosti 2016, waliandika barua ya kulalamika na kupinga maamuzi ya mkutano mkuu huo. Hii ni takribani theluthi mbili (asilimia 62.1) ya wajumbe wote wa Tanzania Bara.
Aidha, takribani wajumbe wote wa mkutano mkuu wa Zanzibar wanamuunga mkono Maalim Seif na maamuzi ya Kikao cha Baraza Kuu la Uongozi kilichofanyika Vuga. Ndiyo kusema, ndani ya CUF, Profesa Lipumba na Maalim Seif bado wana uhalali mkubwa kisiasa kwa kuzingatia idadi ya wafuasi walio nao.
Kwa mazingira haya, mgogoro wa kisiasa ndani ya CUF unapaswa kumalizwa kisiasa kwa pande mbili kukaa na kuzungumza kwa kuaminiana. Hili litawezekana tu endapo pande zote mbili zitakubali kuaminiana na kuamua kuzingatia maslahi mapana ya chama chao, badala ya kuendeshwa na makundi nje ya chama chao kwa maslahi finyu ya makundi hayo.
Kama makundi mawili ya uongozi yatashindwa kumaliza uhasama wao, ni muhimu sheria za nchi na matakwa ya Katiba ya CUF yakazingatiwa. Kwa sasa, kwa mujibu wa barua ya msajili iliyozingatia matakwa ya Katiba ya CUF, sheria ipo upande wa Profesa Lipumba.
Hata hivyo, ni wanachama wa CUF pekee ambao wana fursa katika vikao mbalimbali wenye uwezo wa kumaliza mgogoro huu kwa maslahi ya chama chao. Katika kukinusuru chama chao, ni muhimu wanachama wakazingatia misingi ya chama chao. Ni muhimu waachane na ufuasi wa viongozi wao na badala yake wavae ufuasi wa chama.
Wakiamua kuwa wafuasi wa misingi ya chama watahakikisha kwamba wanazingatia matakwa ya katiba yao na watafanya maamuzi bila kuangalia sura za Maalim Seif na Prof. Lipumba. Ni katika kuhakikisha wanasimamia misingi ya vyama vyao badala ya matakwa ya viongozi ndipo wanachama wataweza kuzuia viongozi kujitwalia mamlaka ya vikao vya chama katika kufanya maamuzi.
Raia Mwema