The Palm Beach
JF-Expert Member
- Dec 30, 2015
- 3,612
- 9,269
Hawa jamaa (CCM) rushwa iko kwenye damu zao. Hii rushwa ya ndani ya chama chao ni tone kwenye ziwa Victoria....
Kwenye ushindani na vyama vingine, huko wanapora na kuiba kila kitu, wanateka, kupoteza na kuua kabisa wapinzani wao...
Tunaposema, hawajawahi kushinda uchaguzi wowote kihalali muwe mnaelewa...
Hii ndio maana ya NO REFORMS NO ELECTION
Ushahidi huu hapo. Mbwa kala mmbwa mwenzake
=================
Baadhi ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Ambureni, Jimbo la Meru, Wilaya ya Arumeru, Mkoa wa Arusha, ambao ni mabalozi wa nyumba kumi na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Kata, wamerudisha vyakula na zawadi walizopewa na mgombea udiwani wa kata hiyo katika ofisi ya chama, wakidai kuwa ni rushwa, ambayo chama kinapinga kutolewa wakati wa kipindi cha uchaguzi.
Uamuzi huo umetokana na kile walichodai kuwa mgombea huyo alikataa kufungua geti la nyumbani kwake walipokwenda kumrejeshea vyakula hivyo, ambavyo ni pamoja na mchele, mahindi, unga, sabuni, sukari, na chumvi.
Baada ya kugoma kupokea, walivipeleka moja kwa moja katika ofisi ya chama kata ili viongozi wa kata waweze kumkabidhi rasmi.
=========================
Baadhi ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Ambureni, Jimbo la Meru wilayani Arumeru, wamechukua hatua isiyo ya kawaida kwa kurudisha vyakula na bidhaa mbalimbali walizodai kupewa na mgombea wa udiwani, wakitafsiri hatua hiyo kuwa ni jaribio la kutoa rushwa ya uchaguzi.
Kwa mujibu wa tovuti ya Habarileo, wanachama hao ambao ni mabalozi wa nyumba kumi na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Kata, walifika katika ofisi ya CCM kata hiyo wakiwa na vyakula ikiwamo mchele, mahindi, sukari, unga, sabuni na chumvi, wakidai kuwa si sahihi kwa mgombea kutoa zawadi kipindi hiki cha uchaguzi ndani ya chama.
Wamedai kuwa mgombea huyo, Faraja Maliaki, alikataa kufungua geti nyumbani kwake walipojaribu kumrudishia bidhaa hizo, hali iliyowalazimu kuzielekeza katika ofisi ya chama.
Wanachama wa CCM akiwamo Sabrina Ndosi, Mery Thadei na Loy Mbise wamesema kuwa iwapo mgombea ana uhakika na kazi aliyoifanya akiwa diwani, hapaswi kutumia mali kuwashawishi wapiga kura, bali kusubiri maamuzi ya sanduku la kura.
Kwa upande wake, Katibu wa CCM Kata ya Ambureni, Josiah Mollel, alithibitisha tukio hilo na kueleza kuwa chama hakiwezi kupokea vyakula hivyo kwa kuwa hakijamtuma mgombea kutoa misaada hiyo.
“Ni kweli niliwakuta ofisini na niliwakaribisha wakiwa na mchele, mahindi, unga, sabuni, sukari na chumvi lakini niliwaambia chama hakiwezi kupokea na niliwashauri kupeleka nyumbani kwa mgombea udiwani kwa chama hakijamtuma kufanya hivyo lakini wana CCM hao walisema kuwa nyumbani kwa mgombea kuna ulinzi mkali”, amesema Mollel.
Akijibu tuhuma hizo, Faraja Maliaki, aliyekuwa Diwani na sasa anawania tena nafasi hiyo, amesema kitendo hicho ni njama za kisiasa zilizopangwa na wapinzani wake kumchafulia jina, huku akisisitiza kuwa misaada aliyowahi kutoa ilihusiana na taasisi yake ya Faraja Foundation, na ilitolewa mwishoni mwa mwaka jana, na haikuwa sehemu ya kampeni.
Katibu wa CCM Wilaya ya Meru, Rehema Nzuye, hakupatikana kutoa maoni yake kuhusu tukio hilo.