TataMadiba
JF-Expert Member
- Feb 7, 2014
- 9,866
- 5,743
Jana niliandka mada yenye kichwa "Prof. Lipumba Barua Ungemwandikia Lowassa na siyo Maalim Seif", lakini kama kawaida ya JF mada zinazoonekana kumpinga Lowassa ama huondolewa au huunganishwa na zingine au hata mtu kula ban, basi sijui ilipotelea wapi. Katika Mada hiyo nilionesha namna ambavyo Prof. Lipumba katika kujaribu kurudi katika nafasi yake ya zamani ndani ya CUF, atakabiliana na nguvu ya Lowassa.
Leo nipo kwa wanachama wa CUF ambao ndiyo wenye chama kwa mujibu wa Kariba ya CUF. Hapana shaka kwamba kauli ya Prof. Lipumba ya kumwandikia barua Katibu Mkuu wa CUF ya kutengua barua yake ya kujiuzulu kuwa mwenyekiti wa chama hicho ilipokelewa kwa Shangwe , vifijo na nderemo na Wanachama na hata baadhi ya viongozi wa CUF.
Haikupita hata siku moja, Maalim Seif akiwa marekani akaropoka kuwa Prof. Lipumba asahau kuwa mwenyekiti wa CUF na kwamba ama achague kuanzisha chama chake au akubali kuwa mwanachama wa Kawaida.
Viongozi wengine wa CUF waliosikika wakiponda matamanio ya Lipumba kurejea kuwa Mwenyekiti wa CUF ni Julius Mtatiro.
Maalim Seif na Julius Mtatiro ni VIBARAKA wa Edward LOWASSA. Sababu zipo.
Narudia kauli yangu kuwa Maalim Seif alihongwa na Lowassa ili kushawishi uongozi na wanachama wa CUF kumuunga mkono Lowassa kuwa mgombea urais wa JMT akipeperusha bendera ya UKAWA. Sababu alizozitoa kwa uongozi wa CUF ni kuwa Chama hakikua na pesa kwa ajili ya kugharamia Kampeni za Uchaguzi wa Rais wa JMT. Zipo taarifa kwamba LOWASSA ndiye aliyegharamia kampeni za uchaguzi wa rais Zanzibar.
Julius Mtatiro ni Mhanga ndani ya CUF kwa sasa. Hapana shaka kila mtu anajua figisu figisu zilizofanyika mpaka akapokwa nafasi ya Naibu Karibu Mkuu wa CUF bara, nafasi ambayo inashikiliwa na Magdalena Sakaya. Hapana shaka kwamba kila mtu anajua Julius Mtatiro alivyotelekezwa na Chama chake katika uteuzi wa mgombea Ubunge jimbo la Segerea, ambapo UKAWA walilazimika kusimamisha wagombea wawili, jambo lililompa mgombea wa CCM ushindi.
Mtatiro anajua kabisa kimbilio lake kwa siku za usoni ni kwenda CHADEMA na kwa taarifa za chini chini ni kwamba ndiye anayetoa taarifa za nini kinaendelea ndani ya CUF kwa Tanzania bara na kwa upande wa Zanzibar ni ISMAIL JUSSA akimwakilisha Maalim Seif.
Hivi sasa Chadema wamejipanga kuhakikisha Prof. Lipumba anapingwa kwenye media mbalimbali kama vile Mitandao ya Kijamii, Magazeti, TV na Rwdio.
Nitatoa walichokiandika mwanahalisionline(tovuti ya Mbunge wa Ubungo, Said Kubenea) na alichokiandika kwenye mtandao wa kijamii wa jamiiforums, Mkurugenzi wa Utafiti na Sera wa CHADEMA, Ben Saanane.
Yote hayo wanaandika kwa sababu wanajua wazi kabisa kwamba Prof. Lipumba akirudi CUF kama Mwenyekiti LOWASSA na Chadema yake wako hatarini kutoweka.
WANACHAMA CUF AMA MUMRUDISHE PROF. LIPUMBA CHAMA KIPONE AU MUWASIKILIZE VIBARAKA WA LOWASSA CHAMA KIMEZWE MITHILI YA NCCR-MAGEUZI