Imetokea eneo la Manyanya Kinondoni ambapo CCM wakiwa na sare za chadema wakiratibiwa na yuleyule Masaburi leo wamekusanyika Manyanya wakitaka kuandamana kwenda makao makuu ya chadema kupinga kile walichodai kauli ya udini iliyotolewa na Mgombea urais wa Ukawa Bw Lowasa.
Vijana wa chadema halisi wakastukia hilo ndipo kwa kushirikiana na vijana wazalendo wa bodaboda wakawasambaratisha vijana wa CCM waliojifanya chadema na kutaka kuandamana.
Waandishi wa Star TV na gazeti la Uhuru walikuwa miongoni mwa mapandikizi ya CCM. Walijikuta wakipigwa vibaya na kuharibiwa vifaa vyao vya kazi zikiwemo kamera.
Mwandishi wa Star TV amekwenda kupata matibabu kuokoa maisha yake hospitali ya kinondoni huku yule wa uhuru akiwa kaumizwa vibaya na haijulikani alikimbilia hospitali ipi licha ya kudaiwa kuwa Mwananyamala.
Maandamano hayo yanadaiwa kuratibiwa na Masaburi na Antony Dialo ili kumharibia Lowasa na Ukawa kama ilivyokuwa yale maandamano feki la kumuunga mkono Slaa.