Wanaccm tuendelee kuwa na umoja tunapitia kipindi kigumu mno

Yusomwasha

JF-Expert Member
Dec 5, 2014
2,092
838
Wana bodi,

WanaCcm tunapitia katika kipindi kigumu sana cha majaribu ikiwemo kupoteza washirika na wanachama. Kuna taarifa ambazo sio rasmi kuwa kutokana na huyu muuza madawa manji yanga wengi wameamua kuhama ccm kwa hasira na uchungu. Najua tunapoteza wanachama maelfu kwa malaki ila tusihofu umoja na mshikamano uwe ngao yetu.

Hii naongelea umoja bcoz kuna taarifa ya kuwepo migawanyiko mikubwa ya waungaji na wapingaji wa kipenzi chetu magufuli. Kuna wanaotafautiana na makonda kuhusu hii vita ya madawa ikiwemo mimi ambaye siungi mkono njia anazotumia. Mwanaccm kamili ni mvumilivu na mstahamilivu na iwe hivyo milele Najua watahama wengi sana, Nimeumia sana wema kuhama na kundi kubwa la watu hivyo ila tunahitaji kukiombea chama.

Lakini haya yote ni makonda huyu sijui kwanini chama kisimtake ajiuzulu anasababisha hasara na tunapoteza maelfu na malaki ya wanachama kutokana na makonda. Mtu mmoja kama huyu kwanini aisababishie ccm iingie hasara hivi? mimi naona makonda hatufai kabisa afate wenzake chadema ili ccm ibaki safi, Tunawapa chadema nguvu na ushawishi kupitia makonda.

Kuna wasiwasi huenda makonda katumwa na wapinzani kuua ccm ukweli nasema huyu hana tofauti na gobachev aliyepandikizwa na nchi za magharibi kuvunja uss. Mchawi wetu ni makonda haiwezekani tuwe na mwanaccm wa ajabu namna hii. Kwanini tukigawe chama huku hawa chadema chama cha hovyo wakifaidika kwanini tunawapa mwanya wapinzani uchwara wa chadema kupitia makonda. Ccm hatutakubali kupoteza maelfu na malaki ya wanachama kupitia mtu mmoja aitwaye makonda.

Makonda jitafakari.

Kidumu chama cha mapinduzi chama imara mpaka wapinzani wanaona gere
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom