Wana psychology, therapists, philosophers na masocialogists masaada wenu hapa

Hu Jintao

JF-Expert Member
Feb 27, 2015
1,356
2,355
Hili suala nimekua nikiliona kwa muda mrefu sana bila kufahamu maana yake au sababu hasa ni nini.

Unakuta mtu labda anakuja upande uliopo ghafla akikuona anajifanya yupo bize labda kuongea na mtu mwingine au kufanya kitu asichopanga kwa muda ule na kubadili uelekeo na kwenda njia nyingine Ili msikutane yaani kama ana kukwepa hivi bila sababu yoyote.

Kipindi hicho Hauna tatizo naye hata kidogo.

Hii kitaalamu imekaaje wadau.
 
Hili suala nimekua nikiliona kwa muda mrefu sana bila kufahamu maana yake au sababu hasa ni nini.
Unakuta mtu labda anakuja upande uliopo ghafla akikuona anajifanya yupo bize labda kuongea na mtu mwingine au kufanya kitu asichopanga Kwa muda ule na kubadili uelekeo na kwenda njia nyingine Ili msikutane yaani kama ana kukwepa hivi bila sababu yoyote. Kipindi hicho Hauna tatizo nae hata kidogo. Hii kitaalamu imekaaje wadau.
hiyo inaitwa Mind your business
 
Nataka nijue kitu gani kinamfanya akukwepe
Tupunguze mazoea yasio kua ya Lazima.
Hivi unajua Mimi Kuna Watu nafahamiana nao zaidi ya miaka 5, Ila Ni salamu tu Basi.
Salamu Yangu.
"Mambo"
Ukijibu "Poa" naondoka sisubili Mambo yawe Mengi sitaki.
 
Na wewe wale ambao hua huwakwepi wanajiuliza,
kwann nikutana na mtu unamkwepa ili kila mtu ajali mambo yake yeye hajiongezi anataka kujua mambo yako.

Huwezi jua.
 
Salamu ni chanzo cha mazoea

Na mazoea ni chanzo cha kujuana

Na kujuana ni chanzo cha kuanza kudharauliana "... aha yule jamaa kumbe yuko vile nilikuwa namchukulia serious sana .."

Huyo ni mimi kabisa kimsingi sipendagi salamu nyingi.
 
Hapo tatizo lipo kwako na sio huyo anayekukwepa.

Kisaikolojia Maisha ni reflection Unavyomtazama MTU na kuhisi yupo hivi au vile maana yake sio yeye yupo hivyo Ila wewe ndo UPO hivyo.


Katika Philosophy , Kuna utofauti wa mvuto na kuvutia , mara nyingi watu wanovutia huwa wanakwepwa Sana na watu wenye mvuto hawakwepwi.


Ili usifike hiyo hatua hiyo tofautisha mvuto na kuvutia uta-enjoy Sana. Maisha.

Sikiliza zaidi na ongea pale unapohisi upo na cha kuongea chenye tija usizungumze zungumza. Usiongelee ongea.
 
Back
Top Bottom