Wana MMU, tujengane na sio kushindana

Wana MMU, tujengane na sio kushindana

Hekima zako zilikosekana humu. Hili la vita humu ya wanawake na wanaume (kuzungumzia mabaya za jinsia zote mbili) mie linanikera sana. Na athari zake haziishii humu bali kwenye jamii yote ya Watanzania na kuwa sumu kubwa ya mahusiano ya kimapenzi.

Nilijaribu kulipinga hili lakini ni gumu sana kupambana nalo. Hata kuna mdada humu alikuja kuandika mambo mazuri sana kuhusu ndoa yake. Wengi walimsifia sana huyo bi dada na mimi kuwa mmoja wao.

Pamoja na kuwa matatizo yapo lakini si kuwahusisha wanawake au wanaume wote kwenye matatizo hayo na pia lugha zinazotumika hazina staha hata chembe.

Shukrani sana kwa kuanzisha huu uzi.

Cookie

Habarini wana MMU

Niende moja kwa moja kwenye point

Kumekuwa na wimbi la wanawake kuchambuliwa na kutupiwa mzigo wa lawama na tabia mbaya zisizoisha,tena mbaya zaidi hata kama ni ushauri hautolewi kaika njia ya kujenga ujumbe unatolewa in a way ya kuponda kukomoa au kumfanya mtu ajisikie vibaya au kujiona hafai as if tuko kwa mashindano wanaume versus wanawake

Wanaume badala ya kuponda na kuchambua chambua wanawake kupita kiasi na isivyo lazima kwa nini zisiwe zinafunguliwa thread za kushauri au kusema ukweli katika njia ya staha na isiyomuumiza mtu? Hakuna anayekataa kurekebishwa au kupewa ushauri in a good way.

Wana MMU hatuhitaji kuwa na ligi humu nani aonekane zaidi kwa sababu wanawake watabaki kuwa wanawake na wanaume watabaki wanaume sikuzote hakuna kitakachobadilisha hilo, cha msingi ni kukumbuka kuwa kama wanaume wana moyo na wana hisia na wanaumia wanapochambuliwa,wanawake pia wana hisia wanaumia wanapochambuliwa kupita kiasi na ikiwa wanaume wanahitaji heshima wanawake pia wanaihijitaji hiyo heshima hakuna jinsia ambayo inapaswa kuvunjiwa heshima.

Tujengane jamani tusiumizane au kushindana tufikiriane wana MMU kila mmoja humu ana mama dada shangazi mabinti wa kike em tujiweke katika viatu vya hii jinsia ya kike kila jiwe linakuja kwako.Just imagine tu una mtu wako wa karibu wa jinsia ya kike then mbele yako anatupiwa kila aina ya sifa mbaya,utahisije??
 
Ndio nishamaliza hivyo...

Mitazamo ya watu haifanani, humu ndani kuna wapumbavu, werevu, wajinga, wema, maarufu n.k...

Wewe kama mwerevu wala hutahangaishwa na mtu mpumbavu maana ndio yupo hivyo...

Btw habari za miaka?
You say so but nina imani kuwa hata mwerevu kuna wakati inafika anaweza kuhangaishwa na huyo anayeonekana mjinga au mpumbavu,najua hata wewe hilo unalitambua moyoni mwako unless otherwise uwe unaishi mbinguni au kwenye ulimwengu wako,Hivi wanaoandika vitabu vya kuwainspire watu wachange ni werevu wanaohangaishwa na wajinga au wapumbavu au wasiojielewa?

Za miaka nzuri sana mkuu tunapambana na hali zetu tu hapa.
 
Hekima zako zilikosekana humu. Hili la vita humu ya wanawake na wanaume (kuzungumzia mabaya za jinsia zote mbili) mie linanikera sana. Na athari zake haziishii humu bali kwenye jamii yote ya Watanzania na kuwa sumu kubwa ya mahusiano ya kimapenzi.

Nilijaribu kulipinga hili lakini ni gumu sana kupambana nalo. Hata kuna mdada humu alikuja kuandika mambo mazuri sana kuhusu ndoa yake. Wengi walimsifia sana huyo bi dada na mimi kuwa mmoja wao.

Pamoja na kuwa matatizo yapo lakini si kuwahusisha wanawake au wanaume wote kwenye matatizo hayo na pia lugha zinazotumika hazina staha hata chembe.

Shukrani sana kwa kuanzisha huu uzi.

Cookie
Hata baada ya kitambo kingi kupita bado u BAK yule yule ninayemfahamu sikuzote never changing,inapendeza sana mkuu.

Ni kweli na niwazi kuwa vita hii kupigana nayo ni vigumu sana tayari tumeshaukubali mfumo wa mshindano kati ya wanaume na wanawake tena mashindano ambayo hayana maana na wala hayatusaidii chochote maishani mwetu zaidi ya kujenga chuki baina yetu na kuishi kinafiki,tunasahau kuwa tumezungukwa na wale wale ambao kutwa hatuishi kuwapondea na kuwadhallisha kwa lugha zisizo na staha hata kidogo tunasahau kuwa hao hao wengine ni mashangazi,wajomba,baba,mama,mabinti au hata vijana wetu.

Ni kweli matatizo yapo na yanaonekana wazi lakini shida ni vile yanavyokuwa addressed,ni katika njia ambayo inavunjia heshima jinsia Fulani inayoongelewa kwa wakati huo inabakiza makovu mioyoni mwa watu na hilo linaonekana wazi kwa jinsi watu wanavyocoment.

Lakini hilo halipaswi kufanya watu wake kimya kabisa wakiona mahali kuna tatizo ni vyema kusema ili kama kati ya watu kumi kuna mmoja akikumbushwa au kukosolewa anaelewa ni bora zaidi kuliko kukaa kimya kabisa na kumkosa hata huyo mmoja anayeweza kuthamini na kugundua kuwa kuna mahali mambo hayako sawa.

Mwisho napenda kukushukuru kwa dhati kwa walau kuelewa hangaikio langu mkuu BAK na kuona sababu ya mimi kuandika nilichokiandika.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Pamoja sana Blue G nawe pia hekima na busara zako bado ziko pale pale. Ni vizuri mwanadamu kujitambua unasimamia maadili yepi katika maisha hata kama wanaokuunga mkono ni wachache lakini ukiwa na msimamo usiotetereka baadhi ni lazima watakupa heshima zako kwenye jamii.

Ningekuwa MOD hizi mada za kupondana wanaume na wanawake humu ningezipiga vita sana pamoja na kujua kuna matatizo, lakini kupondana hakuondoi tatizo kwenye jamii yetu bali ndiyo tatizo linazidi kuongezeka.

Shukrani sana Blue G [emoji1431][emoji1431][emoji1431][emoji257]
 
Pamoja sana Blue G nawe pia hekima na busara zako bado ziko pale pale. Ni vizuri mwanadamu kujitambua unasimamia maadili yepi katika maisha hata kama wanaokuunga mkono ni wachache lakini ukiwa na msimamo usiotetereka baadhi ni lazima watakupa heshima zako kwenye jamii.

Ningekuwa MOD hizi mada za kupondana wanaume na wanawake humu ningezipiga vita sana pamoja na kujua kuna matatizo, lakini kupondana hakuondoi tatizo kwenye jamii yetu bali ndiyo tatizo linazidi kuongezeka.

Kwanza Asante kwa compliment yako am humbeled kwa kwelii

Pili ni kweli kabisa Mkuu BAK kuponda hakuondoi tatizo zaidi ya kutunza vinyongo na hasira na kutengeneza mitazamo ya kuoneshana ubabe na ndo maana kutwa thread za kuumizana na kuchamubuana humu haziishi kama njia ya kuoneshana umwamba na kulipa kisasi kwa yule aliyetuumiza kwa njia isiyo ya moja kwa moja.

Tutafika tu lakini tusivunjike moyo

Hakuna siku ambao dunia itakuwa na watu wenye mitazamo hasi na mibaya tu kuelekea watu wa aina au jinsia fulani, people with positive attitudes will always be there hata kama wachache inatosha na kufariji pia.
 
You say so but nina imani kuwa hata mwerevu kuna wakati inafika anaweza kuhangaishwa na huyo anayeonekana mjinga au mpumbavu,najua hata wewe hilo unalitambua moyoni mwako unless otherwise uwe unaishi mbinguni au kwenye ulimwengu wako

Mpumbavu atamsumbua mwerevu endapo tu huyo mtu mwerevu ataamua kuketi au kuambatana na mpumbavu...

Hivyo kwangu mimi mtu mpumbavu hata huwa hanisumbui, huwa nawapuuzia tu watu namna hiyo labda wabadilike...

Hivi wanaoandika vitabu vya kuwainspire watu wachange ni werevu wanaohangaishwa na wajinga au wapumbavu au wasiojielewa?

Wapo waandishi wanaopoteza muda kwa kuwa kuna wapumbavu wengine kamwe hawabadiliki kwa makanyo ya maandishi maana kwao upumbavu ni kama ngozi...

Za miaka nzuri sana mkuu tunapambana na hali zetu tu hapa.
Nimefurahi kujua hivyo maana ni muda mrefu sana...
 
Hongera kwa mawazo yako lakini tambua kila mtu ana akili yake mkuu ukianza kutaka akili za wana MMU wote zifanane ni ngumu na haiwezi ikawa aisee.

Kwa sababu kuna mwingine anaona kutoa siri za fulani au kumkosesha amani fulani kwake ndio raha yake yaani anajisikia burdaani kabisa.
Nafikiri ni ushauri tu kwahiyo kama mtu anaona unamfaa anaweza kuuchukua. Ni sawa na kuhubiri amani na upendo kila siku, haimaanishi wote watafuata ila walio na utu na kujitambua lazima wataona kuna umuhimu wa kufuata.
 
Mpumbavu atamsumbua mwerevu endapo tu huyo mtu mwerevu ataamua kuketi au kuambatana na mpumbavu...

Hivyo kwangu mimi mtu mpumbavu hata huwa hanisumbui, huwa nawapuuzia tu watu namna hiyo labda wabadilike...

Wapo waandishi wanaopoteza muda kwa kuwa kuna wapumbavu wengine kamwe hawabadiliki kwa makanyo ya maandishi maana kwao upumbavu ni kama ngozi...

Nimefurahi kujua hivyo maana ni muda mrefu sana...
Haya sawa mkuu hongera kwa kumanage kuwapuuzia wapumbavu na kutosumbuliwa na watu wa namna hiyo kwa mujibu wako ila

Binafsi pale napotakiwa kusema na naona yafaa kusema nitasema atakayeona nimefanya kitu chema ataniunga mkono na atakayeona napoteza muda anaruhisiwa pia kuona hivyo kwa utashi wake

[emoji4] [emoji4] [emoji4] [emoji4] [emoji4]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nafikiri ni ushauri tu kwahiyo kama mtu anaona unamfaa anaweza kuuchukua. Ni sawa na kuhubiri amani na upendo kila siku, haimaanishi wote watafuata ila walio na utu na kujitambua lazima wataona kuna umuhimu wa kufuata.
Shukrani mkuu kwa kuelezea hilo kinagaubaga [emoji120]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Binafsi pale napotakiwa kusema na naona yafaa kusema nitasema atakayeona nimefanya kitu chema ataniunga mkono na atakayeona napoteza muda anaruhisiwa pia kuona hivyo kwa utashi wake

Ukiwa kama fanani wakati mwingine kama sio wote yakupasa utambue hadhira unayotaka kuwakilisha maudhui yako kwayo...
 
Pengine uko sawa lakini unapaswa utambue kuwa utambuzi wangu na wako ni vitu viwili tofauti mkuu labda kwa utambuzi wako usingeweza kuwakilisha maudhui kama haya ya kwangu kwa jinsi ambavyo wewe umeidefine hadhira ya watu humu MMU lakini kwa utambuzi wangu na nilivyoidefine hadhira ya watu humu naona inafaa kabisa kuwasilisha kile nilichokiwasilisha

na uzuri hakuna mahali nimelazimisha watu wafate nlichokiandika

Na uzuri hata ningelazimisha ingekuwa ndoto ya alinacha kwa sababu hata Mungu hawalazimishi watu kufata njia inayofaa na kuishi katika maadili yatufaayo.

Walioelewa na waelewe walioona mantiki na waione wasioelewa na wasielewe wasioiona mantiki na wasione pia

[emoji4] [emoji4] [emoji4] [emoji4] [emoji4]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Hongera kwa mawazo yako lakini tambua kila mtu ana akili yake mkuu ukianza kutaka akili za wana MMU wote zifanane ni ngumu na haiwezi ikawa aisee.

Kwa sababu kuna mwingine anaona kutoa siri za fulani au kumkosesha amani fulani kwake ndio raha yake yaani anajisikia burdaani kabisa.
Kabisa dada Emmy watu wametofautiana tabia kila MTU mtu ana malezi yake...
Jibu la mjinga ukimya.
 
Back
Top Bottom