SHIRIKA la Umeme (Tanesco) jana lilitangaza mgawo mpya na mkubwa wa nishati hiyo ambao utavifanya viwanda, maduka, ofisi na makazi kukosa umeme kwa kati ya masaa sita hadi 12 kwa muda wa mwezi mzima.
Ndugu wana Jf ningependa tulijadili hili kwa umakini mkubwa sana kutokana na umuhimu wake
Hivi tatizo la UMEME Tanzania ni nani wa kulaumiwa? kwani tukilinganisha na nchi nyingine za Africa Tanzania tunaongoza kuwa na vyanzo vingi sana vya Umeme
lakini chakushangaza sisi tz ndio wakwanza kutangaza mgawo wa umeme kila ufikapo mwezi wa 12
Je serikali ya CCM haioni umuhimu wa tz kuwa na umeme wa kudumu? kwanini serikali haitaki kuruhusu watu binafsi kuanzisha uzalishaji wa umeme ambao utauzwa kwa TANESCO na Tanesco kuwasambazia wateja wao?
nani wa kulaumiwa juu ya hili Tanesco na viongozi wake ama Serikali ya CCM na viongozi wake?
karibuni jamvini
mapinduziiiiii daimaaaaaaaa :target::target: