Wana jf tatizo la umeme tanzania nani wa kulaumiwa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wana jf tatizo la umeme tanzania nani wa kulaumiwa?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by engmtolera, Dec 24, 2010.

 1. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #1
  Dec 24, 2010
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  SHIRIKA la Umeme (Tanesco) jana lilitangaza mgawo mpya na mkubwa wa nishati hiyo ambao utavifanya viwanda, maduka, ofisi na makazi kukosa umeme kwa kati ya masaa sita hadi 12 kwa muda wa mwezi mzima.

  Ndugu wana Jf ningependa tulijadili hili kwa umakini mkubwa sana kutokana na umuhimu wake
  Hivi tatizo la UMEME Tanzania ni nani wa kulaumiwa? kwani tukilinganisha na nchi nyingine za Africa Tanzania tunaongoza kuwa na vyanzo vingi sana vya Umeme

  lakini chakushangaza sisi tz ndio wakwanza kutangaza mgawo wa umeme kila ufikapo mwezi wa 12
  Je serikali ya CCM haioni umuhimu wa tz kuwa na umeme wa kudumu? kwanini serikali haitaki kuruhusu watu binafsi kuanzisha uzalishaji wa umeme ambao utauzwa kwa TANESCO na Tanesco kuwasambazia wateja wao?

  nani wa kulaumiwa juu ya hili Tanesco na viongozi wake ama Serikali ya CCM na viongozi wake?

  karibuni jamvini

  mapinduziiiiii daimaaaaaaaa :target::target:
   
 2. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #2
  Dec 24, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Tatizo la umeme nijukumu la serikali. Na serikali inakuwa tatizo sababu tatizo lililopo linafanyiwa kazi kwa style ya zimamoto.

  Sipingi kuwepo na kampuni binafsi za kuzalish umeme lakini npinga kampuni za kuzalisha umeme wa mafungu. Bila kuwa na centralised power generation hatuwezi kufika popote. hizi kampuni za mafungu haziwezi kule umeme nanfuu. Bila uememe nafuu hata wawekezaji watakuja wale wa kubabaisha

  Leo hii kila wizara ina generator. Pale BOT wanasema uwezo mitambo ya gentator zake inatossheleza kusupply umeme kwa mikoa ya dodoma na singida . KIla taaasis ya serikali ina jinsi ya kukabiliana na tatizo. mwisho wa siku wananchi ndotunjikuta hatuna chetu. Serikali imekosa Dira

  Watendaji wa TANESCO na serikali ama kwa kkujua au kwa kutokujua wamekuwa wanahujumu TANESCO. TANESCO inavyohujumiwa ndivyo mwananci wa kawaida anazidi anaumia.

  Rais akihutubia anasema mgaw ni changamoto. Hivi ni changamoto gani inajirudia kwa miaka zaidi ya mitano bila kupata ufumbuzi wa kudumu. Mgao umekuwa kama mafuriko au tetemeko la ardhi ambayo yanakuja ghafla
   
 3. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #3
  Dec 24, 2010
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Kwakweli serikali inabidi ijipange vizuri juu ya tatizo hili.

  Hii imekuwa ni kero ya muda mrefu kwa jamii .

  Wataalamu wa mambo ya umeme tz wako wapi? Wameshindwa kusoma alama za nyakati nakutafuta solution ya kudumu kwa jambo muhimu kama hili?

  Na haya maghorofa yanayojengwa kwenda juu kila kukicha kwa umeme huu mbona ni issue kubwa?

  Umeme ni muhimu sana kwa maendeleo ya taifa lolote so serikali inatakiwa kutafuta solution ya kudumu kwa bei nafuu na kuondoa hii kero
   
Loading...