Wana JamiiForums tafadhali! Msaada, rafiki yangu kanichunia

Wana JamiiForums tafadhali! Msaada, rafiki yangu kanichunia

Kwanza poole kwa yaliyokusibu na hongera kwa kupata ujasiri wa kuomba ushauri.

Kwa mjibu wa maelezo yako inaonesha unauzoefu hafifu katika mahusiano na jinsia ya kike.mf "mlipendana"ingawa hukumtokea lakini tayari ukaribu wenu tayari ulikuwa na hisia za kimapenzi ndani yake.

Sasa ghafula umeanza ukaribu na msichana mwingine;hili ni tatizo endapo utaonesha kumjali huyo wa awali kwani binadamu tuna wivu.

Sasa cha kufanya kama unampenda huyo wa awali kuwa na msimamo na mwambie ukweli unampenda na unamhitaji,lakini pia jitahidi kujua ni nani unamhitaji zaidi kati yao.
mwisho jitahidi kupunguza ukaribu na wadada usiokuwanao malengo hii itakusaidia kupata wepesi katika ulimwengu wa mapenzi.

Kuhusu wanajamvi wanakejeli ama kubeza tatizo "hakuna tatizo dogo kwa mtu binafsi.ni dogo kwakuwa halijakusibu'
 
kwanini usimuulize mbona unafanya hivi .....

walimu wa sasa hivi wana tabu sana......mana mtu hataki kufikiri mpaka afikirishwe na wengine......

Unaweza ukawa unamshauri mwanao....wewe unadhani mtu mzima anasumbuliwa na jambo dogo kama hili...??
 
Mods kadri mnavyochelewesha kuweka jukwaa la watoto ndio mnazidi kutuongezea kero humu ndani....
 
Naona uleamavu wa akili unaingia kwa kasi ya kutisha nchini. Tatizo dogo tu mtu huyo kishakimbilia JF kuomba ushauri.

sijui wazazi ndiyo tuna matatizo....hatuwajengi watoto wetu katika misingi ya kujitegemea kutatua matatizo madogo madogo ambayo wala hayahitaji akili za watu wengine......au mfumo wa maisha wa sasa unalemava watoto.....yani sijui kwa kweli shida iko wapi....
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Wadau mpo poa! Mm tatizo langu kuna binti niliyekuwa nikimpenda sana na yeye pia alinipenda! Maana mara nyingi alikuwa akinifata tunapiga story! Ingawa sikuwahi kumtokea! Kilichokuja kutokea ni pale nilianza kuwa na ukaribu na msichana mwingine ambao sio wa kimapenzi! Yule binti akawa anaanza kuwa kama ananitenga! Mara anajifanya kama hanioni wakati mwingine nikimsalimia haitikii! Me nimeshindwa kumuelewa! Maana hata yule msichana ambaye nipo nae karibu huwa tunapiga stori za kawaida na pia ana mtu! Nimueleweje huyu binti wana JF?

Bora shule zifunguliwe tupumzike na issue za machalii.
 
Me ckupi pole....niko sambamba na mkuu "sister" kwa mistari yake. Ukiendelea hivi utakua kidume dhaifu...omba hao ma- she wasing'amue hili watakufanya shosti. USHAURI...Wanaume uwa tunaamua kum-face ke. MFUATE na umuulize kama ulivotuuliza humu. ..yey dhaifu na wew dhaifu...usirudie kuwa dhaifu hivi.
 
Unachosema ni kweli kabisa. Na hili tatizo la kuomba ushauri mtandaoni kwa tatizo dogo halipo kwa watoto tu, wengine watu wazima tatizo dogo kishakimbilia JF kutafuta ushauri wa nini cha kufanya.



sijui wazazi ndiyo tuna matatizo....hatuwajengi watoto wetu katika misingi ya kujitegemea kutatua matatizo madogo madogo ambayo wala hayahitaji akili za watu wengine......au mfumo wa maisha wa sasa unalemava watoto.....yani sijui kwa kweli shida iko wapi....
 
Siamini kama mbegu zetu za uzazi zimekosa ubora kiasi hiki! maana mazao kama haya hata wa kumuuzia tutamkosa.
 
Watoto wa siku hizi matatizo sana! Mtu anapendwa lakini hajielewi. Huoni ya kuwa huo ni wivu unaotokana na yeye kuwa na upendo kwako? Haya subiri hapo hapo! Take that 'uhusiano' to the next level bwana mdogo!
 
Back
Top Bottom