Wana Jamiiforums!! Karibuni Tupande Mlima Kilimanjaro.

Wana Jamiiforums!! Karibuni Tupande Mlima Kilimanjaro.

kiwatengu

Platinum Member
Joined
Apr 6, 2012
Posts
19,489
Reaction score
18,379
Habari za Jioni wakuu,
Kwa wale ambao hawajawahi kuupanda Mlima Kilimanjaro, Nawashawishi sasa tuungane pamoja tuupande huu mlima.

Binafsi nitapanda siku ya ijumaa, na nimepanga kupanda mpaka kileleni kuipeperusha bendera ya
Jamiiforum, niwaambie tu! mlima kilimanjaro ni moja ya kivutio kikuu nchini Tanzania, tunavivutio vingi ila huwezi kuvifananisha na Mlima Kilimanjaro.
Get ready nitaandaa trip maalumu kwa ajili ya wanajamii walioko tayari, baada ya kipindi cha High season kuisha.

Najua humu ndani wamo wataalamu(Guiders) wanaofahamu mambo mengi sana kuhusu mlima Kilimanjaro, hapa pia tutaomba msaada wao.

Kwa wale watakao kuwa tayari, utaratibu nitautoa mwezi mmoja kabla ya safari ili kila mwenye uwezo
wa kupanda aweze kujiandaa vizuri.

Ikumbukwe kupanda kama kundi kuna unafuu mkubwa wa gharama, than to climb as individual,
Hii ni nafasi kubwa sana kwako wewe Mtanzania uliyekuwa na shauku ya kupanda mlima mrefu kuliko yote Afrika na usijue njia za kufuata.

Naomba nitoe gharama kwa ufupi,
Tozo za hifadhi ni sh. 10,000/= kama kiingilio kwa wazawa wa Afrika Mashriki..
5000/= kwa usiku mmoja kwa ajili ya malazi na sh. 2000/= kama tozo ya uokoaji.
Kwa hiyo kama ni kupanda mpaka Kileleni kwa Siku Tano Tozo yote ni sh. 72,000/=

Gharama za Maguide na mapota pamoja na mpishi ni juu yetu wenyewe.

Inawezekana kabisa.
Ni wakati wako sasa....
Mkuu Invisible umewahi kupanda mlima Kilimanjaro wewe? kama bado its your time now..

OLESAIDIMU ulisema nikukumbushe mambo yakiwa sawa, yanakaribia sasa...

NB: Nikianza tripu hiyo siku ya ijumaa nitawa update each and everything...

Karibu sana.

CC; Arushaone, marejesho, PakaJimmy & Filipo
 
Last edited by a moderator:
Pamoja sana mkuu kiwatengu, huo ndiyo uzalendo, charity begins at home!!
 
Last edited by a moderator:
Pamoja sana mkuu kiwatengu, huo ndiyo uzalendo, charity begins at home!!
 
Last edited by a moderator:
Tupe totol coast kama camp au banda,foods na guide ili tujipange

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom