Wana CCM watakiwa kujiandaa kwa Uchaguzi wa marudio Zanzibar

assadsyria3

JF-Expert Member
Apr 9, 2013
6,903
4,051
Katibu wa itikadi na uenezi wa Zanzibar akizungumza baada ya kikao cha kamati kuu amesema hata kama mazungumzo yatachukua miezi mitatu basu wanaccm wajipange kwa uchaguzi.

Mytake;

Maalifu Seif huwa anaangalia TV ?

Chanzo: ITV

Leo magazeti mbali mbali yameandika juu ya swala la kurudiwa uchaguzi ZANZIBAR na kauli hizo naona zimetolewa na MWENEZI WA CCM ZENJI

binafsi hii habari haijanifurahisha kabisa. Na sidhani kama ni kauli yenye afya njema katika demokrasia yetu. Jambo la kunishtua hapa ni kwamba yanafikiwa haya maamuzi mpaka kutoa kauli hii nzito sana huku kukiwa na VIKAO VINAVYOITWA VYA MARIDHIANO.


sjajua nini faida ya kuendelea na vikao hivyo laiti Kuna maamuzi haya yalokwisha fikiwa na KIKAO VYA VIONGOZI WAKUU WA CCM ZNZ

Nachokiona hapa CCM haina nia njema juu ya amani ya wazanzibar maamuzi kama haya ya kulazimisha yaweza sababisha fujo na pengine kutoweka kwa amani sote tunafahamu siasa za zanzibar ni tofauti na siasa za bara kwa kila kitu.

Rai yangu

CCM kuweni waungwana
Mkilazimisha mambo yanaweza haribika zanzibar ni mali ya wazanzibar wote.

Kwakua kulikua kuna mazungumzo sidhani ilikua busara kutoa kauli kama hii

Kesho CUF nao wakikaa wakatoa misimamo yao mtawajaza wanzanzibar hofu na taharuki

BUSARA IWAONGOZE
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU KIKAO CHA KAMATI MAALUM YA NEC ZANZIBAR ILIYOFANYIKA AFISI KUU YA CCM KISIWANDUI
TAREHE 27 DESEMBA, 2015.

MAKAMU Mwenyekiti wa CCM, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein leo, amekiongoza Kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC) Zanzibar.

Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC wa Idara ya Itikadi na Uenezi Bibi Waride Bakari Jabu imesema kikao hicho cha kawaidi cha siku moja kilifanyika Afisi Kuu ya Chama hicho, iliyopo Mtaa wa Kisiwandui Mjini Unguja.
Kuhusu Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, 2015.

1. Kikao pamoja na mambo mengine, kimempongeza kwa dhati kabisa Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuteuliwa katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, 2015 na kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (Awamu ya Tano) baada ya kupata ushindi wa kishindo (58.46%) na hivyo kuweza kuendeleza wimbi la ushindi kwa CCM ndani ya Demokrasia ya Vyama vingi vya Siasa nchini. Aidha, kikao kimempongeza Mhe. Mama Samia Suluhu Hassan, kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

2. Kikao kimefurahishwa, kuridhishwa na kufarajika na idadi kubwa ya wana CCM kwa kujitokeza kwa wingi katika Uchaguzi Mkuu wa Dola wa Oktoba 25, 2015 na hatimaye kumchagua kwa kura nyingi za ndio Mgombea wa Chama Cha Mapinduzi wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli, pamoja na Wabunge.

3. Kikao kimewataka wana CCM kujiimarisha, kujiweka tayari na hatimaye kujitokeza kwa wingi katika Uchaguzi wa marudio, ili kukiletea ushindi wa kishindo Chama Cha Mapinduzi Zanzibar kuanzia Rais, Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na Madiwani wakati utakapowadia.
4. Kikao pia kimeridhia majadiliano yanayoendelea kuhusu hali ya Kisiasa Zanzibar yanayoshirikisha Viongozi kadhaa wakiwemo Marais Wastaafu wa Zanzibar Mhe. Ali Hassan Mwinyi, Mhe, Dkt. Salmin Amour Juma na Mhe, Amani Abeid Karume, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi,
Kuhusu Shughuli za Kimaendeleo.

1. Kikao kimepongeza juhudi zinazochukuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) chini ya Uongozi wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi katika kuwaletea maendeleo ya kiuchumi na kijamii wananchi wake. Aidha, imempongeza Mhe. Dkt. Shein kwa kusimamia suala zima la Amani na utulivu wa nchi kwa kipindi chote cha miaka mitano iliyopita.

2. Sambamba na hilo, Serikali imetakiwa kuongeza juhudi na kubuni mikakati madhubuti itakayosaidia kwa kiasi kikubwa kuanzishwa kwa miradi (mipya) mbali mbali ya maendeleo Mijini na Vijijini Unguja na Pemba, ili kuinua mapato ya Taifa.
Kuhusu Uhai wa Chama (CCM).

Kikao kimetoa pongezi za pekee kwa Wajumbe wote wa Kamati Maalum ya Halmashauri
Kuu ya Taifa ya CCM, Viongozi wa Chama na Jumuiya zake kwa kazi nzuri ya kuimarjisha Chama na kuwataka kuwa mstari wa mbele katika kukipigania, kukilinda na kukitetea kwa nguvu zote Chama hicho. Aidha, kimewataka kuendelea kufanya kazi kwa mashirikiano, juhudi na maarifa katika kukijenga na kukiimarisha Chama, kwa maslahi ya Wazanzibari na Watanzania kwa ujumla.

Mwisho, kikao hicho kilihudhuriwa na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar akiwemo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan.
Mwisho.
……………………
Waride Bakari Jabu,
Katibu wa Kamati Maalum wa NEC,
Idara ya itikadi na Uenezi – CCM,
ZANZIBAR.
27/12/2015.
 
Last edited by a moderator:
Hatimae Ccm wamewaandaa wanachama wao Kurudia uchaguzi tena muda wowote kuanzia sasa hivi huko Zanzibar
Kikao hicho cha Ccm kimehudhiriwa na Dr shein na makada wengine maarufu
Najiuliza hayo mazungumzo wanafanya ya nini kama uchaguzi lazima urudiwe?
Source Azam Tv
 
Kikao klmeongozwa na Dr Shein na viigogo wa CCM Zanzibar.Je SEIF kalegezwa?
 
Nafikir hawajafanya sawa kama kunamazungumzo sidhan kama walikua watoe hayo maagizo.pia tume ile ile ndio isimamie uchaguz.naona wameenda kinyume na malengo ya mazungumzo yao.wanarudia uchaguz was rais peke yake au na wawakilishi na wabunge.
 
Ndio mwanzo wa mwisho wa JMT. Huyo Vuai ni msaka tonge tu, ndio hao wanaoitwa wahafidhina wa CCM. Hakuna kitu hicho kitawezekana bila ya umwagaji wa damu. Vuai and co hawajali hilo kwa sababu wana madeni ya mamilioni kutoka kila benki unayoijuwa wewe, na kitu kinachowafanya wasife kwa pressure ya madeni ni kwa kuweko wao madarakani. Siku watakayoondoka madarakani badi benki watawaandama. Hujiulizi wewe kuna nyumba ya spika ilojengwa kea gharama za mamilioni lakini spika bado anakaa nyumbani kwake privately na analipwa housing allowance. Kificho ana madeni mpaka kwenye meno na hana uwezo wa kuyalipa bila ya kuuza assets zake zote kwa sababu haku invest smartly.

Lengo lao ni ku provoke ili wanachama wa CUF wa over react ili wapate justification ya kuanza mauwaji kwa raia. Nashauri wapenda Amani wote Tamzania kwa ujumla kuwapuuza hawa jamaa na kusubiri kauli ya uongozi wa Ukawa. Let's wait and see
 
Wanaota hao manyumbu hakuna uchaguzi utakaorudiwa huko zanzibar.
 
katibu wa itikadi na uenezi wa anzibar akizungumza baada ya kikao cha kamati kuu amesema ht km mazungumzo yatachukua miezi mitatu bas wanaccm wajipange kwa uchaguzi.

mytake

maalifu seif huwa anaangalia TV ????

chanzo; itv

Magambaz wakilazimisha kurudia uchaguzi bila maridhiano ya pande husika basi wawe tayari kubeba lawama kwa maafa yanayoweza kutokea!!
 
niliandika uzi wangu kuzungumzia ccm wanavyohatarisha amani ya nchi moderator aka delete, sijui hata anafikiriaga nini
 
Kwani nyie mlitakaje? nashangaa ni kama hamtaki ufanyike uchaguzi
 
Back
Top Bottom