Makonda atawasambaratisha Wapinzani wasipobasilika.
Vijana wengi wanamkubali sana Makonda .
Dr. Slaa na maalim Seif walikua ni makatibu wakuu Toka Upinzani waliokua wanaojua siasa vilivyo.
Kwa Sasa Upinzani umepooza sana.
Wapinzani hawana Dira maalumu Kama ilivyo CCM.
Mbowe ni mpinzani mahiri mwenye msimamo Lakini ameshindwa kuzisoma siasa za watanzania Wa Hali ya Chini.
CCM 2025 Ilikua iwekwe makumbusho Lakini kutokana na Upinzani kuungana na wanyonyaji kulamba Asali CCM itaondolewa Kwa rehema za MUNGU pekee.
Polepole
Gwajima
Bashiru
Ndugai
Majaliwa
Mpina
Mwakyembe
Mrisho Gamboa
Makonda
Bado ni watetezi kindakindaki Wa Wananchi maskini wanaohitaji kutetewa na kupata mkate wao halali katika nchi iliyoumbwa na Mungu na SIO kunyonywa na kutaabika chini ya Matajiri Wenye hulka za kinyama na wasioshiba pesa Hata walipewa Dunia Nzima watabuni mbinu za ulaghai ,Unyonyaji na fitina.
Makonda ni Wa kumwangalia Kwa akili sana mana Ana kipaji kikubwa sana katika siasa za Wanyonge ambao ndio wapiga kura wengi. Kuwadharau wanyonge ni kujichimbia kaburi.
Makonda alitakiwa apambanishwe na John Heche.
Mwenyekiti Wa CCM mbadala wake SIO Mbowe ni Lisu.
Lisu Ana siasa za Tofauti na CCM Lakini Mbowe ni moja ya kundi la wapigaji.
Ni Awamu ya wapigaji hivyo Mbowe Hawezi kuitikisa hii CCM ya wapigaji Wala Zito Kabwe.
Yule Wa CCM ,Yule Wa Chadema na Yule Wa ACT Wazamiauhondo wote ni wapigaji na Wenye uchu mkubwa sana Wa fedha na madaraka na Mali. Hawa ni walevi Wa Mali na watumwa mbele ya Mali. Hawa Hata kuingia kwenye ufalme Wa MUNGU ni mpaka Tembo aingie kwenye Tundu la Sindano.