Wana CCM na simulizi za Charles Njonjo......

Paka 2025 atang'ang'ania kwa kisingizio chakunyoosha nchi.

Mwafaaaaaaaaa!

ccm mbele kwa mbele.
 
Mtamaliza misemo na mneno yote muyajuayo Dunia hii, lkn CCM ni Chama Dola, kuna sababu kwa nini kinaitwa hivyo, na itabakia hivyo!
Hakuna anayebisha kwamba CCM ni chama Dola. kinachoongelewa hapa, kwa taarifa, na kwa lugha rahisi, ni kwamba huyo jamaa aliyeshika usukani wa hilo CHAMA DOLA, anawashughulikia wanaccm kwa kutumia hiyo hiyo DOLA, na hawana cha kumfanya. yaani kinachoonekana sasa hivi ni kwamba kumbe hili chama dola linakata kila upande, linakula hata watoto wake. naona limeshatoka kwenye uchama dola, limekuwa CHUNUSI
 


Umemuelewesha vizuri na bado hataelewa
 
Umenikumbusha Al-Maarufu Charles Njonjo.

Charles Njonjo alikuwa na suti zake matata sana za Savile Row, mtaa wa kushonesha suti za bei mbaya kabisa hapo London.

Suti maalum za kushonesha ilikuwa ukiziangalia kwa karibu sana unaona zimepigwa chata ya herufi za kwanza za majina yake CN for "Charles Njonjo".

Nyerere alikuwa haachi kumuona kituko.
 

Nyerere mjamaa huyu Njonjo alikuwa bepari
 

Mkuu The Boss, heshima mbele! Yaani umenikumbusha mbali sana kuhusu huyu jamaa Charles Njonjo. mimi nakumbuka ile story aliyosema kwamba hawezi kupanda ndege ambayo pilot wake ni mtu mweusi, yeye anataka Pilot mzungu tu!
Umenena haswa, kwamba Paka ukishampa nyama tu, urafiki umekwisha, mpaka amalize kula hiyo nyama, ndio atakutazama kwa matumaini na unyenyekevu. Ila hii haiwahusu CCM tu, inatuhusu watanzania wote. Najaribu kujiuliza, hivi Magufuli atakapoanza kupiga kampeni ya kuomba awamu ya pili, atapiga tena pushup? maana sasa hivi ameshika nyama, anaunguruma tu kwa ukali. ikiisha nyama atakuwa mpole?
 

Magufuli anatoa maswali ya kila aina

maswali kwa watanzania..

maswali kwa wana CCM

maswali kwa katiba tuliyonayo

maswali kwa wasomi na kadhalika

Sikutegemea mtu kama Ayubu Rioba kupokea 'amri na maagizo' kutoka kwa mtu kama Paul Makonda
but it is happening.....
 
Kwa hiyo tuseme Makonda ndiyo Tanzanian version ya Charles Njonjo? atapungukiwa kwenye elimu. ila hayo makeke, hashindwi hata kumzaba kibao nanihii...
 
Kwa hiyo tuseme Makonda ndiyo Tanzanian version ya Charles Njonjo? atapungukiwa kwenye elimu. ila hayo makeke, hashindwi hata kumzaba kibao nanihii...

Hii nchi mkuu ni tuiombee tu
mengi yanayotokea sasa ni unbelievable
 
Wewe ni LICHADEMA tu, CCM hatuna Mawazo ya Ovyo Ovyo kama hayo, M/kiti wetu Taifa hana ubaguzi, hana uonevu, hana chuki na mwanachama yeyote, Kumbuka Li-Mbowe lenu si lilibadiri hadi Katiba ili litawale milele baada ya kuondoa kile kifungu cha kuongoza miaka mitano mitano na ikifikia 10, basi kiongozi huyo haruhusiwi tena kugombea hata kama atakuwa anapendwa kiasi gani. Lakini yeye kutokana na Uroho wa madaraka na Udikiteta alikiondoa. Sasa Leo wewe badala ya kuongelea tatizo hili kubwa, unahangaika na CCM. Anyway, hangaika ili utimize ushahidi wa malipo yako.
 
Duh hii hadisi kweli imeshililiwa vizuri na Mbowe, yaani yeye hata hilo wazo la kugawa nyama hataki hata kulisikia.
 

Yes, ya Charles Njonjo ni ya kweli kabisa na mimi ni mmoja wa mashahidi kipindi hicho tukiwa Nairobi Kenya kwa shuhuli zetu za kizalendo! Long live President Dr Magufuli, usikubali wanachama waliolewa madaraka ndani ya chama tawala, chama chako, wakuburuze. You are in procession of the Machette and the Hammer/hoe do the needful, play your part skillfully with integrity! The hyenas within and outside CCM are crying and lamenting and the common people are with you!
 
Hii story ya Paka akipewa nyama huwezi kumnyang'anya tena,inanikumbusha ndugu yetu Lowassa maana baada ya kukaribishwa chadema na kupewa nafasi ya kugombania urais sidhani kama mbowe ataweza kumzuia kugombania urais kwa kipindi kingine maana now lowassa baada ya kupewa nyama anataka kuwa ndio mwenye sauti Ndani ya Chama. Imefikia hatua hata kwenye vikao vya kamati kuu lowassa ndio wa mwisho kuingia na wa kwanza kutoka.
Kweli Paka akipewa nyama...........
 
Paka anakuwaga mnyonge sana pale anaposubiri umrushie kipande cha nyama
sasa ukismrushia nenda jaribu kumnyang'anya ndo utamjua vizuri
Napenda style yake ya kudubiria. Anakali chini kwa utulivu huku miguu yake ya mbele kaiweka tayari kudaka anachorushiwa
 
Si hayo tu yapo mengi.

Nakumbuka siku za mwanzo tukibishana kuhusu mwelekeo wa awamu ya tano na kinara wake. Si wengi wenye ujasiri wa kusema ulikuwa sahihi kwa sehemu kubwa wakati sisi kwa lugha ya mitaani "tulibugi". Faraja yangu pekee ni kusema nothing is cast in stone.

Mzee Mwanakijiji kaziita "distractions" za JPM. Hamna kitu kama hicho. Limeishavunda. Tukubali ukweli. Tulichofikiria imekuwa tofauti kabisa.

The man has become the LAW onto himself. Yeye kawa mahakama na Bunge pia. Report ya CAG mwaka huu, italeta sunami. Wizara kutumia 200% ya budget yake!
 
Hakuna aliejua kama Mh Magu akipewa uwenyekiti atafanya mapinduzi ndani ya chama chao.
,Hakuna aliejua Magu atabadirisha katiba ya chama kwa kupunguza wajumbe zaidi ya theruthi,na huku wanaopunzwa wakimshangilia.
Na walipongaka akina Njonjo (Bashe,Msukuma) hakusita kuwakabidhi kituo cha polisi wasimjaribu, next time atawasahau gerezani.
Magu anajua udhaifu wa wabunge wa CCM hata alivyowachimbia mkwala mzito huko Chimwaga alijua tiyari wameongezewa kiwewe,hofu,wameishafyata mkia.
Mapinduzi yameishatua Chama Cha Mapinduzi.
 
Mi nikitazama mambo yanayoendelea nchi hii kwa sasa kuna muda natamani kutafuta uraia wa Uzbhekstan
hauna ndugu huko,nifikie siku mbili tatu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…