Wamiliki wa vyombo vya usafiri Bukoba Wagoma | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wamiliki wa vyombo vya usafiri Bukoba Wagoma

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kaa la Moto, Jun 25, 2009.

 1. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #1
  Jun 25, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Wakuu,

  Leo asubuhi katika mji wa Bukoba kumekuwa na mshituko baada ya wasafiri kutoka maeneo mbali mbali kukosa usafiri katika stand kuu ya mji wa Bukoba.

  Imebainika kwamba wamiliki wa Mabasi makubwa na Hiace ambazo ndizo husafirisha abiria wengi kuingia na kutoka mjini Bukoba wamechukua uamuzi wa kugoma baada ya Sumatra kuwaamuru wenye mabasi na hiace kushusha nauli zinazotozwa sasa.

  Watu wengi wamejikuta kwenye hali ngumu ya usafiri toka vijijini na kwenda vijijini pia.

  Hali yenyewe stand kuu iko hivi kama inavyoonyeshwa hapa chini:


  [​IMG]
  IMGP2044i.jpg
   
 2. Amosam

  Amosam Senior Member

  #2
  Jun 25, 2009
  Joined: Jan 15, 2009
  Messages: 154
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Lwakatare yupo atawasaidia akishindwa ndugu wa Kaskazini wamejaa tele Bukoba watatoa msaada tuu msihofu
   
 3. JosM

  JosM JF-Expert Member

  #3
  Jun 25, 2009
  Joined: Oct 11, 2008
  Messages: 684
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Poleni sana wakazi wa Bukoba,ndugu hapo ndio Bukoba mjini? hapo sioni kitu naona vumbi tu!
   
 4. Kamakabuzi

  Kamakabuzi JF-Expert Member

  #4
  Jun 25, 2009
  Joined: Dec 3, 2007
  Messages: 1,499
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Hata wa Karagwe nao wamekwama. Stendi ya Omurushaka abiria wamejaa na wenye magari wamegoma kabisa.

  Hapa kuna tatizo: Nauli zilipanda kufuatia kupanda kwa bei ya mafuta hadi shs 2000 kwa lita; bei ya mafuta iliposhuka hadi shs 1400 kwa lita, nauli hazikushuka hata senti tano. Kwa sasa wamesikia eti bei ya mafuta imeanza tena kupanda hivyo wanataka kupandisha nauli. Ilibidi bei ishuke kwanza na mafuta yakipanda nayo ipande.

  Tatizo lingine lilisababishwa na mbunge wa Jimbo la Kyerwa Mhe. Katagira. Kuna wakati fulani aliulizwa swali la kwanini nauli hazishuki wakati bei ya mafuta imeshuka? Alijibu kwa kuwatetea wasafirishaji kwamba gharama za usafirishaji si mafuta peke yake, hivyo nauli haikuwezi kushuka kwani vipuri viko juu. Akawa amewapa kichwa wasafirishaji.

  Nadhani alipaswa kuwakomalia wauza vipuri nao washushe bei.

  Serikali- Sumatra wanachotakiwa kufanya ni kufuta leseni za wote waliogoma na kuitisha waombaji wapya wa routes zinazohusika. Watajitokeza tu. Kwa wasiojua - kutoka Bukoba hadi Karagwe ni km120, serikali inasema nauli iwe shs 3000 wakati wasafirishaji wanang'ang'ania shs 5000. Is it fair?
   
 5. B

  Binti Sayuni JF-Expert Member

  #5
  Jun 25, 2009
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 357
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Hiyo ndiyo stand kuu ya mabasi manispaa Bukoba mjini mkuu si unajua miji yetu.Vumbi mtindo mmoja
   
 6. JosM

  JosM JF-Expert Member

  #6
  Jun 25, 2009
  Joined: Oct 11, 2008
  Messages: 684
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kweli safari yetu bado ni ndefu mno.
   
 7. Omutwale

  Omutwale JF-Expert Member

  #7
  Jun 25, 2009
  Joined: Feb 4, 2008
  Messages: 1,429
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Amosam,
  Ndiyo kwenyewe kwetu Nshomile. Tunahitaji sana msaada toka kwa Wajumbe wa Kaskazini. Watu wetu wametusaliti. Wanajenga Dar, wananunua majengo Canada. Ila usione hivyo migombani ni kuzuri zaidi ya mjini. Kuna maghorofa na majumba ya thamani zaidi ya mjini.
   
  Last edited: Jun 25, 2009
 8. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #8
  Jun 25, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Wacha viroja, Lwakatare awasaidie kwani yeye ndiye anaye kusanya kodi zao?

  Wanao jitengea mabilioni ya chai wakawajibike kwa walipa kodi wao.
   
 9. M

  Magezi JF-Expert Member

  #9
  Jun 25, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Kagasheki anafanya nini na ndevu zake?? Nakumbuka nilipita Bukoba mwaka 1997 palikuwa hivyo bado tu....
   
 10. Omutwale

  Omutwale JF-Expert Member

  #10
  Jun 25, 2009
  Joined: Feb 4, 2008
  Messages: 1,429
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Niwe mkweli, Kagasheki hakuwa mbaya kwa BK bali alikosea ki-fikra na ki-mkakati katika kutafuta ubunge. Akilini mwake aliweka fikra ya kuja kuwa Mfalme/mtawala na katika mkakati akajidanganya kwamba pesa inanunua heshima na ufalme. Badala yake amebadilishwa kuwa DECI. Wananchi wanafiki wanakamua weeeee halafu hapati kitu.

  Ubaya wa mtindo wa pesa za kugawa kinafiki eti kisa fulani ni mwenzetu au ni ngangari mnunueni hazileti maendeleo. Na kwa sababu Mbunge analea majungu, kila anayehitaji pesa njia ni moja tu, kumpelekea Mbunge majungu. Badala yake pesa hizi zimeongeza chuki na kubadilisha maana nzima ya Mbunge na Ubunge. Sasa ubunge BK una maanisha kugawa pesa, kuandaa tafrija za walimu na wafanyakazi, kuchangia kila msiba unaokuvutia 50,000 etc. Ni activities nzuri lakini haziwezi kumkomboa mwananchi wala kuleta mabadiliko chanya.

  Kagasheki ni mwoga sana kufanya kazi na wasomi hasa vijana. Hii ndiyo sababu kubwa ya yeye kushindwa katika utekelezaji wa miradi mizuri ya maendeleo na yenye mguso kwa wananchi. Kwa mfano unashika SACCOs unampa layman awe mhasibu, Kazi za PR unaziweka mikononi mwa watoto wa Uswahilini na baadhi ya vijana waliotoka jela, hapa unategemea nini?
   
 11. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #11
  Jun 26, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Leo siku ya pili ya mgomo. Hakuna usafiri kwenda nje na kuingia ndani ya mji wa Bukoba.
   
 12. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #12
  Jun 27, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Sumatra imekubaliana na wamiliki wa magari kuendelea kutoza nauli mpya kwa muda wakati wana review rates walizotangaza.
  Wameonya kuwa wakiendelea na mgomo watafuta leseni zao.
  naona magari kidogo leo yamekuwepo standi kuu.
   
Loading...