Wamenitapeli miaka 2 iliyopita sasa tena

Wamenitapeli miaka 2 iliyopita sasa tena

ndanda masasi

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2014
Posts
772
Reaction score
1,179
SIMU KUTOKA TIGO

ngrrriiiiiii!!!!!!!!! NGriiiiIIIIII!

TIGO; mimi ni -----naongea kutoka Tigo tunaongea na?

MIMI; nakusikiliza
TIGO;umewahi kutumiwa ujumbe wowote juu ya TIGO BIMA?
MIMI; ndio lakini sikushughulika nao

TIGO; nataka nikufahamishe kuhusu TIGOBIMA
MIMI; nam eleza nakusikiliza

TIGO; kuna bima ya afya na bima ya gari
MIMI; eleza kwanza hiyo ya afya

TIGO; unalipia tsh 16,000 kwa mwakaa na utakapo umwa utahudumiwa kwa kupewa kila siku tsh 40,000 kwa kila siku kwa siku 30 yani utapata tsh 1200000 ikiwa utalazwa katika hospital ya serikakali au binafsi na ipite mwezi mmoja baada ya kujiunga kwako

MIMI; na nafsi yangu kimya kimya hawa ndio wezi tu kama vile vile BIMA zingine kwanini wasiende muhimibili wampe mgonjwa 1200000 na mgonjwa awape Tigo 16000? huruma ya mamba hii sio bure

MIMI; okey je nisipo umwa kwa miakaa 5 na nikafa kwa ajali?

TIGO; ahha unajua sasaa halafu aaah kwaniiii

MIMI; kwahiyo nisipo umwa ndio mtakuwa mmeniibia sio?

TIGO; kwani kama utaumwa na ukatumia tsh 120000 huoni nawewe utakuwa umetuibia?

MIMI; kwahiyo mnatangaza mchezo wa kuibia sio? mjanja kupata?

TIGO; hapana kakaa unaaonekana mgumu wa kuelewa sana au huna shida ya BIMA?

MIMI; enewey sasa nakuuliza je nikiumwa na kulazwa siku zaidi ya 30?

TIGO hapo hutolipwa kwani umezidisha siku za vigezo na masharti

MIMI; kwahiyo una tangaza wazi kuwa mteja wenu wabima mta mtelekeza na kuachana naye akafie mbali?

TIGO;aahhh unajua sasaa kwani masharika mengine unadhani yatakubali hali hiyo?

MIMI; hao mimi najua ni matapeli tu kwahiyo na nyie ni matapeli?

TIGO; vigezo na masharti kuzingatiwa

MIMI; enewey umesema nikiwa nimelazwa hosptali je kama naugulia nyumbani?
TIGO ; hulipwi? kwani lazima iwe hospital

MIMI;kwahiyo mimi nikivunjika mguuu nikafungwa chuma sipewi pesa hizo mpaka niwe hosptali na hali ndio nahitajia gharama?

TIGO; mpaka uwe hospitali tu

MIMI; huu ni mpango wa nyie na mahosptali kuwakamua masikini na si zaidi

TIGO; kwanini? lakini we kaka mbona mgumu kuelewa?

MIMI; unajua unapo lazwa hosptal unalipia kitanda doctar taa feni mpaka tv mfano kama kwa siku ni 40,000 ina mana pesa yenu yote itaishia hapo hospitali sio? sasa mimi nitafidika na nini?

TIGO; si utapata pesa za kutibiwa?

MIMI;sasa kuvunjika mguu na nimefungwa vyuma lazima nilazwe hopitali? ili pesa yangu iliwe na hospitali? unajua si kila ugonjwa lazima ulazwe hospitali au hilo hujui?

TIGO; aah jamani we kaka! yan yaani yani huelewi kabisa !

MIMI; okeee nimeelewa kuwa ni ubabaishaji tu sasa nakuuliza je mjamzito na mwenye ukimwi?

TIGO ;mjamzito mpaka awe na mwaka mmoja tangu kujiunga kwake

MIMI; kwahiyo mjamzito hana thamani kabisa kwenu wedada umesha zaa ukajua dhiki ya ujauzito? kwanini mwanamke huyu hana thamani kwenu?

TIGO; kimyaaa

MIMI; halooh! upoooo?

TIGO; kimyaaaa!!!1

ttiii t,t,ttiiii tiiiiii!!!!!!!!!!!!!!

0675-672 708 iliyo tumika kupiga

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wamenipigia mie pia leo jamaa akatoa maelezo mengi ya Tigo bima, kisha akaniambia nimechaguliwa kuwa mmoja wa wateja watakaopewa kiasi cha shs. Milion 2 nachotakiwa kufanya ni kutuma kiasi cha shs. Elfu 36 ili wanitumie zawadi nikawapongeza sana kwa jinsi wanavyojali wateja mwisho nikawaambia wapunguze hicho kiasi kwenye zawadi niliyoshinda[emoji16]wakakata simu
Walitumia namba 0711814052

Sent from Ili iweje
 
Utapeli wao ni wakipuuzi sana na. Na hihohiyo imetumka tena ujumbe huu

OSTADHI OMALI MZEE NIBINGWA WA MABINGWA Anatoa Utajili Kwanjia Ya Majini Je Ukotayali Kumuua Mzazi Wako Au Kumfanya Mke Au Mtoto Kichaa Kama Hiyo Ngumu Unaweza Kumuabudu Shetani Kama Mungu Wako Basi Mchinjie Jini Wako Mbuzi Kila Siku Au Uwe Mlemavu Wa Macho Na Ukosehisia Ya Mapenzi Tafadhali Kama Unahitaji Mali Yetu Ya Majini Piga 0711814052 Ukiipata Sms Hii Walushie Wenye Ndoto Za Utajili Watimize Ndoto Zao Halaka Sana?

Sent from Ili iweje
 
Safi sana uwekwe Uzi maalum kwa ajili ya number za hawa matapeli kama jamaa walivyofanya itasaidia sana. Ila niwaombe TCRA sio kila kitu mpaka Rais aseme hizi number zinazotumika kufanya utapeli zimesajiliwa na makampuni yetu ya simu. Watu wanalamika kila siku number zilezile zinazotapeli....kwanini haya makampuni haziblock hizi number? Yaani mtu akitapeliwa sasa hivi piga fines na kampuni ilepe fidia kwa muhanga wa utapeli
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] nimependa namna ulivyomtahini huyo Malaya.

Hawa wahuni wa mitandao wajue kwamba hela sasa haitoki kwenda kwa mtu kizembe,hali ni ngumu.
 
Back
Top Bottom