Wamekataa ya Serikali na Haya nayo Watakataa ?

Logikos

JF-Expert Member
Feb 26, 2014
12,388
19,394
Wamesema Serikali Tatu gharama na wananchi hawataki Serikali 3 wanataka Amani na Maendeleo.., Sasa sababu maendeleo yanaendana na kupunguza gharama na uwajibikaji, Je ikifika wakati wa kujadili haya itakuwaje :-

  • Kufuta viti maalumu / kupunguza idadi ya wabunge
  • Mawaziri kutokuwa Wabunge
  • Kufuta Wakuu wa Wilaya
  • Kupunguza Madaraka ya Rais
  • Kurekebisha Tume ya Uchaguzi

Hivi kweli hawa jamaa watakubali kupunguza idadi ya wao wenyewe au tusubiri watakuja na ngonjera gani kutetea viti maalumu na idadi lukuki ya wabunge, (au watanzania pia hawakusema kuhusu haya mambo) na ni vipi tutawabana pindi wakileta ngonjera hizo ?
 
Hapo chacha tuwaache tu waendelee na bunge lao tutakutana kilimani sesani
 
Hawa CCM wamenipa msamiati mpya, ukipiga nyumba yako rangi uwatangazie watoto kuwa ni mpya hata wakikataa walazimishe kwa viboko.
 
Wamesema serikali tatu ni gharama, watasema pia kufuta viti maalum ni gharama! Ili mradi wapingingane na rasimu ya Katiba
 
Wamesema serikali tatu ni gharama, watasema pia kufuta viti maalum ni gharama! Ili mradi wapingingane na rasimu ya Katiba

Sasa hapo gharama ipo wapi, ila hawa jamaa hawakosi sababu watasema tu yakusema siku ikifika, watasema mawaziri wasipokuwa wabunge hawawezi kutekeleza kazi zao, na vitu maalumu watasema tunawanyunya dada zetu, ila tume ilipendekeza kwamba kila mkoa kuwe na wabunge wawili tu, yaani wa kike na wa kiume, hakuna mambo ya kila Jimbo
 
hawa ccm wamenipa msamiati mpya,ukipiga nyumba yako rangi uwatangazie watoto kuwa ni mpya hata wakikataa walazimishe kwa viboko.

Au wadanganye kwamba hii kupaka rangi ndio mtindo wa kisasa na hii itadumu zaidi kuliko mpya.., na mkikataa kabisa basi basi na hii rangi niliyopaka taichafua nyumba ibaki kama zamani
 
Kumbe wamekataa duh sasa wanataka mbunge apewe muda wa miaka saba as well as kuwa na wabunge wawili kila jimbo (mwanamke na mwanaume)
 
Wakati tunajitayarisha kwa Katiba Mpya tujikumbushe wale wale waliokuwepo then ni nini walifanya and what has changed wasifanye yale waliyofanya then...
 
Back
Top Bottom