Wamasai wa Monduli, Arumeru wapigana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wamasai wa Monduli, Arumeru wapigana

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by MziziMkavu, Mar 1, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Mar 1, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  Yamezuka mapigano ya kati ya Wamasai wanaoishi Wilaya ya Monduli na wa Wilaya ya Arumeru mkoani wa Arusha, na kusababisha maboma manane yenye nyumba 65 kuchomwa moto katika kijiji cha Mfereji, Monduli.

  Kufuatia tukio hilo, mamia ya wananchi wamebaki bila makazi na kulazimika kwenda katika vijiji vya jirani kuomba hifadhi.Tukio hilo lilitokea juzi.
  Diwani wa Kata ya Monduli Juu, Elibariki Sumuni, alisema morani zaidi ya 500 kutoka katika vijiji vya Imbibia na Engalaoni, Lengijave na Mwandet walivamia mamboma ya Wamasai wa Monduli na kuyateketeza.

  Sumuni alisema morani hao ambao walibeba silaha za kijadi walipiga mbiu na kuitana usiku wa kuamkia juzi kisha kuvamia katika kijiji hicho kilichoko katika eneo lenye mgogoro wa muda mrefu na kutekeleza unyama huo.

  “Ilikuwa ni hatari, nilipewa tarifa kuwa wa Arusha wameitana karibu kutoka kata nne, ilibidi morani wetu wakimbie kwani hao watu walikuwa wengi sana, wamechoma nyumba kuharibu mali nyingi,” alisema Sumuni.

  “Mgogoro huu uliwahi kusababaisha mauaji ya mtu na mali nyingi kuharibiwa na umekuwa ukiibuka nyakati za kiangazi tatizo ni eneo la malisho watu wa upande wa Monduli wanawazuia wafugaji wa uapande mwingine wasichunge,” alisema.
  Alisema chanzo cha mgogoro huo uliodumu kwa muda wa miaka zaidi ya 40 ni eneo la malisho ya mifugo ambalo kila upande unadai ni la kwake.

  Baadhi ya waathirika wa tukio hilo walisema kuwa walivamiwa na morani zaidi ya 500 juzi na kulazimika kukimbia kwa hofu ya kuuawa kutokana na kuwa wengi wakiwa wamesheheni silaha za kijadi.
  Lemali Orkonyori, alisema kuwa hawakufanikiwa kuchukua chochote kutokana na kuvamiwa usiku wa manane na makundi ya morani kutoka Arumeru.

  Kaimu Kamanda Polisi mkoani Arusha, Akili Mpwapwa, alisema kuwa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa imefanikiwa kuzima vurugu hizo.  CHANZO: NIPASHE
   
Loading...