Wamasai tunaonekana hatuna msimamo kabisa

Wamasai tunaonekana hatuna msimamo kabisa

loosimingori

JF-Expert Member
Joined
Oct 30, 2017
Posts
920
Reaction score
1,146
hadi leo jumla ya wabunge wa chadema waliojiuzulu ubunge na kurudi ccm kutoka kabila la maasai ni wabunge takribani wa3.Hili tu linatosha kabisa mimi kuhitimisha kuwa hatuna msimamo ktk maamuzi yetu na tumekuwa ni watu wa kuyumbishwayumbishwa mno utadhani hatukuchinjwa pale kishomi
 
poleni wamasai wote kwa kuyumba.. sijui kama mtaweza kuwa handle wanawake zenu mana hivi viumbe ndo hatari zaidi
 
poleni wamasai wote kwa kuyumba.. sijui kama mtaweza kuwa handle wanawake zenu mana hivi viumbe ndo hatari zaidi
asante sana mkuu ila cjui hawa wanaoyumbishwa watakuwa ni rika gani
 
Madhara ya kuchelewa kuingia uwanjani wakati mwingine in kucheza kwa pupa au kilimbukeni.Masai ni kabila LA kuliheshimu sana, ni kabila pekee TZ ambalo halikuchukuliwa utumwani, slave routes zilikwepa eneo lao kutokana na viongozi wao kutokuwa na tamaa ya kuuza watu wao na wao wenyewa kuwa majasiri,waarabu wa biashara ya utumwa waliwaogopa kama ukoma.Wamasai ni watu wema na sio wanafiki, wanaheshimiana sana kwa kuzingatia rika aghalabu kumsikia Mmasai akimtukana mwenzake seuse kiongozi,.Utajiri au madaraka sio vitu vilivyokuwa vinapapatiwa na Masai. Sokoine alikuwa mfano halisi
 
Kwa asili, wanasiasa wote ni vigeugeu! Asiyefanya hivyo yuko kwenye siasa kimakosa! Wanasiasa siku zote wanaangalia political fates zao katika lens ya prevailing political winds.
 
hadi leo jumla ya wabunge wa chadema waliojiuzulu ubunge na kurudi ccm kutoka kabila la maasai ni wabunge takribani wa3.Hili tu linatosha kabisa mimi kuhitimisha kuwa hatuna msimamo ktk maamuzi yetu na tumekuwa ni watu wa kuyumbishwayumbishwa mno utadhani hatukuchinjwa pale kishomi
Wamasai halisi hawawezi kukubaliana na utapeli wa Mbowe.
 
Madhara ya kuchelewa kuingia uwanjani wakati mwingine in kucheza kwa pupa au kilimbukeni.Masai ni kabila LA kuliheshimu sana, ni kabila pekee TZ ambalo halikuchukuliwa utumwani, slave routes zilikwepa eneo lao kutokana na viongozi wao kutokuwa na tamaa ya kuuza watu wao na wao wenyewa kuwa majasiri,waarabu wa biashara ya utumwa waliwaogopa kama ukoma.Wamasai ni watu wema na sio wanafiki, wanaheshimiana sana kwa kuzingatia rika aghalabu kumsikia Mmasai akimtukana mwenzake seuse kiongozi,.Utajiri au madaraka sio vitu vilivyokuwa vinapapatiwa na Masai. Sokoine alikuwa mfano halisi
ni kweli mkuu ila hawa kina mollel,ole millya,na kalanga wametuaibisha kabisa
 
Wamasai kama wafugaji wengine nchi hii wameonewa sana ,kwa kuchelewa kwenda shule wameporwa ardhi zao bila hata kulipwa fidia kama vile maeneo ya malisho sio matumizi halali ya ardhi. Leo hii wanafukuzwa kila mahali wanapokwenda. Tazama maeneo makubwa yaliyochukuliwa kwa matumizi ya jeshi, Tz Canada Wheat Project Malbadang nk,wakati wa ukoloni Masai steppes ilikuwa kwa ajili ya ufugaji tu
 
Wamasai wana misimamo ya kuua simba, kutembea na silaha viunoni, kuvaa mashuka na kuchunga ng'ombe,
hawa wanaohamahama nadhani hawajawahi kuua cmba,kuvaa rubega na kuchunga ngombe kwanza nahisi huenda walichomwa cndano ya ganzi wakati wa jando
 
Ni wamasai na wakurya. makabila niliyotegemea wamepitia jandoni kumbe hamna kitu. hata ukiweza kuwakoromea na tigo unapata
 
Kununuliwa ni kama kupigiwa simu laini ya tigo. mpigaji akishapiga anakuona kama vyangudoa wengine tu hata mezani pake hukai maana anajua huna msimamo na unapigwa ovyo ovyo isitoshe unanuka.
 
Masai ni Vigeugeu haswa, nna ushahidi katika hili, has upande wa kwenye Biashara.....!
 
sasa kwann walijiunga na huyo mbowe before

Labda walidhani alikuwa morani kumbe he actually wasn’t! ...Jamaa tapeli la mjini tu!🤣

Seriously, huo ulikuwa upepo wa safari isiyokuwa ya matumaini ya morani mwenzao, ambaye, kwa sababu ya uchu wake wa kwenda ikulu, alitapeliwa mabilioni chapuchapu na mtoto wa mjini! Hata hivyo, ENL mcheza kamari mzoefu; anajua kuna kula au kuliwa. Jamaa alicheza za wengine zikaliwa!
 
Usijilaumu sana, zama zinabadilika haraka sana zama za kina Ole Konchellah, Ole Saibul,Lepillal Ole Molloimet, Benedict Lesuritia, Edward Mbarnot,Edward Lowassa na mpendwa wetu Edward Sokoine na wengine wa rika hizo waliingia siasa kabla haijawa biashara.Sasa hivi kuingia siasa bila kubebwa na MTU mwenye musuli sio rahisi, sio suala LA kabila wala Tanzania.Hivi umewahi kujiuliza kama Marekani wanalalamika chaguzi zao kuingiliwa kwetu ikoje, ni kura zetu kweli zinazisimika viongozi na kama huna kitu na huna MTU wa kukubeba waweza shinda uchaguzi? Kina Nyerere, Lumumba, Nkuruma, Nasser bado wapo Afrika? Bora huyu wakwetu ingalau ana ujasiri hata wa kusema ukweli. Usikate tamaa historia huwa inajirudia ,kwani hata kina Nyerere, Mandela nk sio mashujaa wa kwanza Afrika, Mungu, wakati , uhitaji utawanyanyua wengine yaweza kuwa akina Julius Malema Afrika kusini, Ole Sendeka au wewe kwa Wamasai .Usikate tamaa wala usihofu, wala kwa sasa ambapo watu karibia wrote mpaka maprofesa wanafikiria kwa kutumia matumbo yao na sio vichwa vyao usitegemee Masai awe tofauti sana.Sasa Masai anahitaji bodaboda ya kuzunguka mbugani, anahitaji gari,nyumba ya kisasa,wapo wanaovaa chain za dhahabu ,wanahitaji miziki, wanakula kuku, mayai na samaki nk kifupi wanahitaji mapesa mengi ikiwa inachangiwa na shule za kisasa au kizungu wanazosoma. Life style
 
Back
Top Bottom