Wamarekani weusi (USA) wanatumiwa kama Kiatu!

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,811
Katika watu ambao ni ngumu sana kwangu kuwaelewa ni hawa Wamarekani wenye asili ya Afrika au Wamarekani weusi, kwangu mimi ni kundi la watu ambao wamechanganyikiwa na hawajui wanataka nini na maisha yao matokeo yake wanaishia kutumiwa tu wanasiasa kama vile kiatu!

Kwa mfano Obama wakati anakampeni walitumiwa na maelite kuambiwa kwamba ni Mmarekani wa kwanza mweusi kuwa Raisi wa Marekani wakati ukweli ni kwamba Obama siyo mweusi hivyo hawezi kuwa raisi wa kwanza mweusi lkn hiyo ni mada nyingine!
Wakajitokeza kwa wingi wao kumpigia kura Obama hata wale ambao hawajawahi kupiga kura maishani mwao walipiga kura siku hiyo Obama akashinda wengine mpaka wakawa wanalia machozi siku Obama alivyoshinda.

Miaka 8 baadaye hakuna chochote Obama alichofanya kuisaidia hiyo jamii anaiacha kama alivyoikuta bado zaidi ya asilimia 85% ya walio jela USA ni kundi lao yaani Wamarekani weusi ingawaje wao ni 20% ya Wamarekani wote, mpaka leo hii leo hii Mmarekani mweusi anapigwa risasi na Polisi kwa sababu tu ni mweusi hakuna jipya!

Haya hilo likapita sasa leo hii kuna Donald Trump hawa hawa Wamarekani weusi wanatumiwa tena na wale wale waliowatumiwa wakati wa Obama ili wampinge D.Trump kama ilivyotokea huko Chicago Trump ameshindwa kufanya Mkutano wake kwa sababu waandamanaji ambapo wengi wao ni Wamarekani weusi wamemletea fujo Trump pamoja na Wafuasi wake ambapo ni kinyume na hata Katiba ya Marekani, Trump hajavunja sheria yoyote ile ya USA kwanini wamfanyie fujo na ashindwe kufanya kampeni?

Hivyo Establishment hawamtaki Trump sasa wanawatumia Wamarekani weusi kama walivyowatumia wakati wa Obama kumnyima kura Trump lakini mwisho wa siku watatumiwa na maestablishment kama kiatu na kutupwa bila kukumbukwa kama vile tufanyavyo na kiatu pindi kinapochakaa tunakitupa mara moja bila hata kukumbuka kwamba kilitufaa!

Sio weusi tu
ImageUploadedByJamiiForums1457844023.294031.jpg
 
Kwa hiyo mama yake Obama alichepuka na huyo mzee Hussein akaingizwa mkenge? Wewe unamjua baba halisi Wa Obama? Eti Obama si mweusi..

Ni muda wa weusi utawala ulikuwa umefika Kama ambavyo Magufuli akimaliza muda wake itakavyokuwa zamu ya CHADEMA kutawala.

Ubaguzi wa rangi Marekani upo ila sheria ni kali Sana tofauti na hapa Tanzania. Marekani mzungu akibainika kufanya crime yoyote dhidi ya mweusi anakamatwa na kufungwa.

Halafu kuhusu weusi wengi kuwa jela si kwamba wanaonewa wengi wao ni criminals, hawapendi Shule, ni wajinga, wanateswa na asili ya uafrika ya kuupenda umaskini kama wewe ulivyo.

Kwanza Marekani hujawahi kufika, unaiona kwenye TV tu, halafu unasimulia ujinga wa kusadikika hapa.
 
Kwa mara ya kwanza nasikia kwako kuwa obama sio mweusi...
Amekusudia hivi, Obama si kutoka kizazi cha watumwa weusi waliopo US! Mamake ni mzungu na babake alikua mwanafunzi toka Kenya wale dizaini ya hit & run kwa excuse ya fake marriage
 
Amekusudia hivi, Obama si kutoka kizazi cha watumwa weusi waliopo US! Mamake ni mzungu na babake alikua mwanafunzi toka Kenya wale dizaini ya hit & run kwa excuse ya fake marriage
Sio weusi wote walioko Marekani ni kizazi cha watumwa.

Mimi si kizazi cha watumwa. Marekani kuna form unajaza rangi. Nitajaza mweupe au mweusi?
 
Sio weusi wote walioko Marekani ni kizazi cha watumwa.

Mimi si kizazi cha watumwa. Marekani kuna form unajaza rangi. Nitajaza mweupe au mweusi?
Issue si wewe au yule! Point ilielekezwa particularly kwa Obama as daud1990 doubted!!
 
Tangu lini Obama ni mzungu? Bora hata ungesema shombe la kijaluo, na hiyo hoja yako naona kama chuki na wazungu tu.
 
Mkuu with all due respect hujui ulisemalo. Obama ni mweusi and so is Stephen Curry, Drake(Canada), na wengine wote ambao wazazi wao mmoja au babu zao ni weusi. Kuwa light skin hakukufanyi kuwa mzungu na hakuna race inayoitwa half caste(0.5)

Trump anahubiri chuki na ndiyo sababu kuna kundi kubwa la watu na wengine ni Republicans hawamkubali. Mtu yeyote anayejielewa hawezi msapoti Trump
 
Nimekusoma bro.
 
Issue si wewe au yule! Point ilielekezwa particularly kwa Obama as daud1990 doubted!!
Point iliyoletwa ni kwamba Obama hajazaliwa kizazi cha watumwa waliopelekwa Marekani na hivyo hawezi kuwa mweusi, kitu ambacho ni sawa na mimi.

Nikasema mbona mimi naitwa mweusi na si kizazi cha watumwa?

After all, Wandengereko wa Rufiji nao pia ni weusi ingawa hawajazaliwa kizazi cha utumwa.

Soma mtiririko, usirukie tu.
 
Back
Top Bottom