Wamama tupunguze unyanyasi kwa watoto wa wenzetu

Raynavero

JF-Expert Member
Apr 29, 2014
38,413
56,030
Heri ya mwaka mpya wana MMU

Leo nimeona niongelee hii tabia ya baadhi ya wanawake kunyanya au kuwatesa watoto wa waume zao wa waliozaa nje,wametengana wazazi au wazazi wamefariki wao wakaolewa.

Kwa kweli km mwanamke naumia na kujisikia vbaya sana na nachukia mwanamke mnyanyasi kwa mtoto wa mwanamke mwenzio

Sio jambo zuri na wala halipendezi na km wanawake tunapaswa kubadilika sana maana ht wewe ambae unatesa mtoto wa mwenzio huna garantii utaishi miaka mingapi hapa duniani.
Naongea hivi kwa mifano hai hapa kazini kwetu

Leo amekuja mzazi wa kike na mwanafunzi wake shuleni kufika ameenda ofisi ya nidhamu akaona kushtaki akaanza kumpiga kipigo cha mbwa mwizi,ikabdi baadhi ya walimu wamgombelezee mm nikamuuliza"Mama huyu mwano wa kumzaa?"
Akajibu "hapana namlea tu"
Nikasema ndo maana..nikamuita mtoto akaja ofisini kwangu na kumuanza kumuhoji namna wanavyoishi kwa kweli ni huzuni

Mtoto wa kwake yule anasoma shule za binafsi,wa mwenziwe serikali na haruhusiwi kuondoka bila kufanya usafi ndani,akirudi shule apike na aoshe vyombo.
Hapewi hata mia anavyokuja shule kila siku anakaa km kilometa 5 hivi mpk kufika shule Ila nauli hapewi.

Mama yake amefariki toka yuko mtoto mdogo sana wako wawili yy na Dada ake!
Mama ake Mara kwa Mara anamchongea kwa baba ake anapigwa mpk anavimba

Kosa la Leo ni kukamatwa na simu nikamuuliza simu kapata wapi?akanijibu"Madam simu kuna mkaka kanipa natembea nae na yy ndo ananipa hela ya kula na nauli kila siku na mm nachoka wenzangu wanapelekwa na skuli bus shule mm natembea ka miguu,sipewi ht mia.Kingine madam na mm ht pedi(asshakum si matusi)sinunuliwi,ukimuambia baba anakuambia muambie mama ako na mama akipewa pesa hanipi na nikikuomba saa ingine ananiambia si uende kwa mabwana zako.

Kanieleza mengii ya kuhuzunisha kwa kweli nikajiuliza hivo huyu mwanamke anajiskiaje yaani kutesa mtoto wa mwenziwe kiasi hicho?

Hiyo sio kua kadanganya hapana nilishajaribu kufatilia kabla kwa wenziwe wakaniambia hvyo hvyo na huyo sio mwanafunzi pekee anayenyanyasika wapo wengi haswaa wanaokaa na wamama wa kambo.

Wababa hivi mnalishwa nn mpaka mnajisahau hvyo jamani kwa watoto wenu ambao hamuishi na mama zao?

Jitahidini kuwachunguza watoto wenu wana mengi Ila hamuwapi nafasi ya kuwasikiliza

Nakubali mapenzi yana nguvu Ila jitahidi mwanao uwe karibu nao
au ndo mnalishwa nyama za chini...

Na nyie wamama wenzangu baadhi jitahidi kupenda mtoto wa mwenzio kuna Leo na kesho daahhh...

Kumbuka na yeye amebeba mimba miezi tisa km wewe na alizaa kwa uchungu pia!
Uwepo wako isiwe chanzo cha mateso kwa mtoto wa mwenzio.

Jioni njema
 
Mama wa kambo hao, yani utakuta hata makosa mengine mtoto hajafanya but yote apewa lawama mtoto, anyway kuna kabila lina sema

√√Mtoto wa mwenzio mkubwa mwenzio
 
Kama watakuelewa natapeleka mswada wa kuomba usemi ule wa ''MAMA WA KAMBO SI MAMA''...Ufanyiwe mabadiliko....Sometimes kuna misemo iliyoibuliwa zamani sana na wazee wetu na ukijaribu kuangalia ni kweli kabisa hadi unajiuliza walijuaje hayo...Ni wachache sana wanawake wanaoweza kuwapenda kwa dhati watoto wa mwanamke mwenzio labda awe hakai na hao watoto....
 
Ndugu hata baba WA kambo Ni wachache sana wanaopenda watt ambao si damu yao hiyo Ni nature ya wanyama wote. Si tetei hayo manyanyaso nimeona mama Wa kambo wazuri tu ila wengine WA wanyama huwa hawapendi watoto WA mwingine. Shemeji yangu naona mtoto Wa mke Wake hampendi Na anambagua kabisa
 
Kuna rafiki yangu wa karibu sana alibahatika kupata mtoto ila kwa sababu mbalimbali hakuweza kuishi na mzazi mwenzie.. Uamzi aliochukua katika maisha yake ni kuishi peke yake mpaka kifo kimkute..Ukimuuliza kwanini hataki kuoa anakujibu rahisi tu kwamba anampenda mwanae hataki alelewe na mama wa kambo kwa sababu hata kuwa na uchungu naye.
 
Ndugu hata baba WA kambo Ni wachache sana wanaopenda watt ambao si damu yao hiyo Ni nature ya wanyama wote. Si tetei hayo manyanyaso nimeona mama Wa kambo wazuri tu ila wengine WA wanyama huwa hawapendi watoto WA mwingine. Shemeji yangu naona mtoto Wa mke Wake hampendi Na anambagua kabisa
Unadhani kwa nini kukawa na usemi huu wanao sema MAMA WA KAMBO SI MAMA na hakuna unaosema BABA WA KAMBO SI BABA?
 
Ila jua kua kuna watoto pia ni shida hasa wakiwa katika kipindi cha balehe
Kwanza kulea mtoto asie wako ni kipaji haswaaa!!
Alafu wakati mwingine sio wa kuwaamini sanaaa, kuna mmoja aliwahi ongea mazitooo kuhusu mama yake wa kambo, kufuatilia kumbe yule mtoto kashindikana,na anamwambia kabisa yule mama "huwezi nifanya kitu wewe sio mama yangu". Alipelekwa private akakaa miezi mi3 tu akafukuzwa shule, ikabidi yule mama aje amuombee aendelee tu pale.

Baada ya kuujua ukweli ikabidi tumbane tena aseme ukweli, akakubali kuwa yeye ndio mkorofi,sio siri mama wa watu alihangaika hadi kuhakikisha yule mtoto anamaliza shule japo kwa taabu sana. Alikuwa anajitahidi kufuatilia kila hatua ya maendeleo ya binti kama mwanae, adolescents ni taabu sana kudeal nao.
 
I bet kwenye huu uzi hakutakuwa na mnyanyasaji hata mmoja, kila mmoja atavutia kamba kwake.
Haha wote tuna roho nzuri leo mbona.

Ndoa tunapenda, watoto hatuwataki. Afu mtoto wa mwenzio umemkuta, kama uliona huwezi kumlea si ungeenda tu kwa fresh man jamani. Ila hili ni somo pia kwetu, kama hakuna sababu ya msingi, it's better mtoto alelewe na wazazi wake wote wawili. Ila tulivyofanya kuzaa tu kama fashion siku hizi mmh, tunatesa sana watoto
 
Kwanza kulea mtoto asie wako ni kipaji haswaaa!!
Alafu wakati mwingine sio wa kuwaamini sanaaa, kuna mmoja aliwahi ongea mazitooo kuhusu mama yake wa kambo, kufuatilia kumbe yule mtoto kashindikana,na anamwambia kabisa yule mama "huwezi nifanya kitu wewe sio mama yangu". Alipelekwa private akakaa miezi mi3 tu akafukuzwa shule, ikabidi yule mama aje amuombee aendelee tu pale.

Baada ya kuujua ukweli ikabidi tumbane tena aseme ukweli, akakubali kuwa yeye ndio mkorofi,sio siri mama wa watu alihangaika hadi kuhakikisha yule mtoto anamaliza shule japo kwa taabu sana. Alikuwa anajitahidi kufuatilia kila hatua ya maendeleo ya binti kama mwanae, adolescents ni taabu sana kudeal nao.
Yana kulea mtoto wa mtu mwingine kama wa kwako ni Neema. Nina aunt yangu mmoja ana neema ya kulea watoto wa wenzake, kakusanyiwa wote hapo hana hata shida. Tatizo baba anawatia jeuri watoto, mama zao pia ndo usiseme. Yule aunt ni kama takataka tu pale nyumbani. Kuna siku sijui alimfanyaje mtoto wa kiume, mbona alikoma matusi kwa mama mzazi wa mtoto. Kuna huyo wa kike mkubwa walidundana akamchoma kisu mama ake wa kambo kwenye titi. Me sijui kama ningeweza, hapana jamani
 
Back
Top Bottom