Wamama: Kwanini mkisalimiwa na vijana hamuitikii?

Wamama: Kwanini mkisalimiwa na vijana hamuitikii?

Ryzen

JF-Expert Member
Joined
Dec 6, 2012
Posts
7,312
Reaction score
8,754
Nafikiri hili hata kuna wengine limeshawahi kuwatokea!

Kuna wamama wawili na mdada mmoja (ambaye ni binti wa mama mmoja kati ya hao) naishi nao jirani, sasa hapo nilipopanga mtoto wa hio nyumba ni age mate wangu japo nimemzidi kama mwaka mmoja ni rafiki yangun sana na mara kibao nakaa nae hapo kwangu.

Ishu ipo ivi mimi nina safari zangu ambazo huwa nakaa mwezi mpaka miezi miwili ile nikirudi Nikiwasalimia hao wanawake basi wanakuwa na mzuka wanapokea salamu vizuri tu.

Pia mimi hata nikiwa hapo gheto ni mtu wa kutoka asubuhi na kurudi usiku wa manane, kurudi mchana mara moja moja.

Tatizo linakuja hapa hawa wamama bwana mimi nawaheshimu kama mama zangu na nawasalimia with full respect.

Sasa tatizo nikiwasalimia wanaitikia kwa kujivuta sana jambo ambalo mimi linanivunja moyo kuwasalimu au sometimes wasiitikie kabisa sasa hapa nina wazo la kutowasalimia kabisa always tupishane tu kama strangers.

Je nitakuwa nakosea? Mnanipa mawaidha gani katika hili? Kwa kuwaongezea siwategemei direct katika lolote maana mimi ni mtu ninayejitegemea.

Pia hebu watu wakubwa mjifunze kuheshimu vijana hakuna kijana anapungukiwa kitu asipokusalimu. Mnateta kwamba vijana wamekosa adabu kumbe tatizo linaanzia kwenu.

Stay Blessed

TheMason!
 
Nafikiri hili hata kuna wengine limeshawahi kuwatokea!

Kuna Wamama wawili na Mdada Mmoja (Ambaye ni binti wa mama mmoja kati ya hao) naishi nao Jirani...sasa hapo nilipopanga mtoto wa hio nyumba ni age mate wangu japo nimemzidi kama mwaka mmoja ni rafiki yangun sana na mara kibao nakaa nae hapo kwangu!

Ishu ipo ivi mimi nina safari zangu ambazo huwa Nakaa mwezi mpaka miezi miwili......ile Nikirudi Nikiwasalimia hao wanawake basi wanakuwa na Mzuka wanapokea salamu vizuri tu!

Pia Mimi hata nikiwa hapo Gheto ni mtu wa kutoka asubuhi na kurudi usiku wa Manane...Kurudi mchana mara moja moja.....!

tatizo linakuja hapa hawa wamama bwana mimi nawaheshimu kama mama zangu na nawasalimia with full respect...sasa tatizo nikiwasalimia wanaitikia kwa kujivuta sana jambo ambalo mimi linanivunja Moyo kuwasalimu au sometimes wasiitikie kabisa!

sasa hapa nina wazo la kutowasalimia kabisa Always....tupishane tu kama strangers

Je nitakuwa Nakosea? Mnanipa Mawaidha gani katika hili? kwa kuwaongezea siwategemei direct katika lolote maana mimi ni mtu ninayejitegemea!

Pia hebu watu wakubwa mjifunze kuheshimu vijana....Hakuna kijana anapungukiwa kitu asipokusalimu!.....Mnateta kwamba vijana wamekosa adabu kumbe tatizo linaanzia kwenu!

Stay Blessed

TheMason!
Badili strategy ya kuwasalim, wasalimie habari zenu; za kushinda; mnaendeleaje; mmeamka salama; wazima; MAMBO VIPI! Hii ya mwisho wataipenda sana ila usiitumie, ukiitumia hii kuna 'ukuta' wa heshima ulioujenga kati ya wewe na wao wataanza kuuruka.
 
Badili strategy ya kuwasalim, wasalimie habari zenu; za kushinda; mnaendeleaje; mmeamka salama; wazima; MAMBO VIPI! Hii ya mwisho wataipenda sana ila usiitumie, ukiitumia hii kuna 'ukuta' wa heshima ulioujenga kati ya wewe na wao wataanza kuuruka.
Genius!
 
wamama wa mjini hawataki shikamoo
Na huo ndio ukweli. Kuna mmoja nikimsalimia ananijibu mambo. Alaf ananichangamkia ile mbaya, sasa sijui ni huwa wanatengeneza mazingira
 
Salamu ya mjini siku hizi ni MAMBOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO.

Na mtu mzima anaitikia POUWAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAH.

Huku amekenua meno yote nje.
 
Usingewafikiria yasingekuumiza, achana nao fanya yako. Na ukijua kwamba heshima haitafutwi, inakuja yenyewe
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom