Dam55
JF-Expert Member
- Oct 8, 2015
- 5,641
- 11,956
Habari wapendwa,
Kwa dhati ya Moyo wangu nawatakia pasaka njema yenye furaha na amani.
Kuna hii tabia ya wanawake hasa wamama, kwa kweli nisingependa siku hii ya pasaka ikapita huku nikiwa na duku duku rohoni. Wamama acheni tabia ya kuwatukana watoto wenu matusi ya nguoni. Hivi we mama ndio kusema kwamba una hasira sana ama ni vipi hadi unafikia hatua kumtukana mtoto wako uliye mzaa tena tusi linalokuhusu wewe mwenyewe. Huoni kama unamtolea razi mwanao.
Tabia hii imeshamiri sana kwa sasa halafu mnalalamika kuwa watoto hawana akili shuleni, wahuni, watukanaji, hawana nidhamu n.k wakati mmewalaani wenyewe.
Halafu unajidai na we ni mama kweli? Mama gani wewe usiye na haya hata kidogo mtoto wako wa kumzaa unathubutu kumtajia alipotokea? Umechanganyikiwa wewe.
Sijaoa na wala bado sijabahatika kupata mtoto ila nikija kuoa halafu siku nikamkuta anamtukana mtoto mitusi wallah ndoa inavunjika siku hiyo hiyo. Wanawake acheni huu ujinga, mbona wazazi wetu hawakuwahi kututukana namna hiyo hii tabia nyie mmepata wapi? Au ndo kweli nyie wanawake ni mashetani. Na kama ni hivyo basi ni wanawake wa kizazi hiki tu ndo mashetani mana mama zetu hawakuwa na tabia kama hizi. Au ndo mnatukana watu wazima kwa kisingizio cha watoto? Maana haiwezekani kabisa umtukane mwanao namna hiyo.
Samahani kwa niliowakwaza ila ujumbe wangu umefika.
Acheni kuwalaani watoto wenu kwa makusudi, mtoto anapokosea anaelekezwa na sio kutukanwa mitusi.
Ahsante.