Clemence Mwandambo
JF-Expert Member
- Dec 2, 2018
- 1,384
- 1,438
'Theme' ni ile ile, "vijana ni wavivu"; halafu baadae inapanda - "WaTanzania ni wavivu",!3. Vijana wengi ni wa vivu. Ni lini vijana wamekutana kama kikundi na kuomba mashamba ya ujasiliamali kwa serikali wakanyimwa. Lakini kitu kingine vijana sio waaminifu wanafikiria kuiba sana na hili linawarudisha nyuma kwenye kazi za kufanya pamoja.
'Theme' ni ile ile, "vijana ni wavivu"; halafu baadae inapanda - "WaTanzania ni wavivu",!
Ulishalisikia hili likisemwa na akina nani? Akina 'kamundu' kama hutaki kujibu swali.
Tatizo lako ni moja siku zote, na ni tatizo kwelikweli. Sijui uraia wa nchi yako hii uliupata vipi, lakini kuna kitu katika damu yako kinakataa kabisa kukuondoa kwenye jamii uliyoamua kuiacha nyuma na kuchukua uraia wa nchi nyingine.
Hii ina maana, huu uraia wa kupewa ni gheresha tu, ya kukupa nafasi ya kila mara kutanguliza maneno "Nchi yetu Tanzania", huku kwenye damu ukibaki kuwa raia halisi wa nchi yako ya asili.
Niseme, unajitahidi sana kuonyesha uTanzania wako, lakini katika mawazo unayowasilisha mara kwa mara yanakusuta jinsi usivyoridhishwa na mambo mengi ya nchi yako hii mpya, huku ukitamani yale yaliyoko kwenye nchi uliyoiacha ndiyo yawepo hapa. Sijui kama siku moja itakuwa hivyo, sijui. Itakuwa bahati sana kwako ikitokea iwe hivyo.
Huenda hawasaidii Tanzania kama unavyosema lakini wanahudumia familia zao na kusaidia ndugu ambao ni watanzania.
Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
Hoja ni ipi hapo, au hujui maana ya hoja ni nini!Unapenda kutupotezea muda na kwenye nje ya hoja. Ongelea hoja nimekuja na list pale kama unakubaliana au una mawazo tofauti badala ya kujifanya unanijua sijui mimi ni Nurse … hunijui na wala sina shida ya kukujua twende na hoja za kusaidia wananchi badala ya kila topic yangu kujaribu kuibadilisha na kuniongelea mimi badala ya hoja!. Hunijui na mimi sikujui tuishie hapo.
Sawa kabisaaa. Sasa nenda pale kariakoo ukawahutubie hao machinga hizo propaganda zako bilashaka watakuelewa zaidiiWatanzania wengi hawajui kwamba Wamachinga hawasaidii nchi yetu badala yake wanatumika kwa siasa pekee. Watanzania wanashangilia wamachinga ambao hawalipi kodi halafu wanalalamika wenyewe kuongezewa kodi!
1. Hawalipi kodi yeyote ya maana na vibali vya machinga ni kama kukejeli Watanzania.
2. Wachafuzi wa mazingira. Hivi hizi gharama za usafi analipa nani hasa kwa watu wasio lipa kodi.
3. Wanauza vitu vya kijinga ambavyo havina msaada wowote wa maana kwa viwanda vyetu wala sera muhimu kama kilimo, elimu au afya.
4. Wanasaidia viwanda vya china sio Tanzania hebu tukaangalie kama vitu vya machinga ni vya Tanzania! Utakuta ni majalala ya kichina hivyo tunasaidia wachina na sio Tanzania.
5. Wanaua wafanyabiashara wadogo ambao wanalipa kodi maana wameweka magenge ambayo hayana mpangilio mbele ya biashara nyingine
Almost zero😁..mchango wa sekta ya wamachinga ktk pato / uchumi wa Tanzania ni kiasi gani?
Almost zero😁
Watanzania wengi hawajui kwamba Wamachinga hawasaidii nchi yetu badala yake wanatumika kwa siasa pekee. Watanzania wanashangilia wamachinga ambao hawalipi kodi halafu wanalalamika wenyewe kuongezewa kodi!
1. Hawalipi kodi yeyote ya maana na vibali vya machinga ni kama kukejeli Watanzania.
2. Wachafuzi wa mazingira. Hivi hizi gharama za usafi analipa nani hasa kwa watu wasio lipa kodi.
3. Wanauza vitu vya kijinga ambavyo havina msaada wowote wa maana kwa viwanda vyetu wala sera muhimu kama kilimo, elimu au afya.
4. Wanasaidia viwanda vya china sio Tanzania hebu tukaangalie kama vitu vya machinga ni vya Tanzania! Utakuta ni majalala ya kichina hivyo tunasaidia wachina na sio Tanzania.
5. Wanaua wafanyabiashara wadogo ambao wanalipa kodi maana wameweka magenge ambayo hayana mpangilio mbele ya biashara nyingine
Kuna waliosema nina mada za ajabu ajabu tujiulize leo hii Raisi wa Tanzania kasema yote niliyosema!!Huyo jamaa huwa ana mada zake za ajabu ajabu sana.
Sijui kama huwa anamkakati wowote na hizi mada au la, lakini kuna aina fulani ya mfanano ukizifuatilia vizuri.
Kuna wakati aliandika kulaumu vijana wa kiTanzania wasivyojituma na kuchangamkia fursa, akilinganisha na vijana wa nchi aliyozaliwa yeye. Leo analalamika kwa hawa vijana kujishughulisha na kilichopo wanachoweza kukifanya.
Sasa sijui kama ni kwa bahati mbaya, au ndivyo zilivyopangiliwa.
Kwanza eleza rais kasema nini, halafu tuone kama ndicho ulichosema wewe.Kuna waliosema nina mada za ajabu ajabu tujiulize leo hii Raisi wa Tanzania kasema yote niliyosema!!
Kwanza eleza rais kasema nini, halafu tuone kama ndicho ulichosema wewe.
Nina hakika kabla hata sijakiona hicho unachodai rais amekisema kitakuwa ni tofauti na wewe ulichowahi kukisema wewe, tena kwa maksudi ya kuwadharau hao vijana wa kiTanzania ukilinganisha na hao wa huko kwenu.
Hoja ni ipi hapo, au hujui maana ya hoja ni nini!
Hivi ngoja nikuulize, wale vibaka wa CBD Nairobi wanaonyang'anya watu mali zao mchana kweupe unadhani ni bora zaidi ya hawa waTanzania wanaojihangaikia kupata ridhiki yao kwa jasho lao kihalali? Ndiyo, shughuli inayofanywa na hawa vijana ni halali kabisa, wewe usiyekuwa na ufahamu wowote juu ya jambo hilo ndiye unayeimba upuuzi hapa.
Ni orodha ipi uloiyoweka pale ijadiliwe, mbona siioni?
-" Hawalipi kodi"? Unajuwa maana ya kodi ni nini wewe? Wao hawanunuwi vitu kwa mahitaji yao? Hili nalo hulijui?
-" wachafuzi wa mazingira"? Hao walioajiriwa kuweka usafi unataka wakaajiriwe wapi, au unataka mpaka tuwaite jina unalolijuwa wewe kutokana na huko ulikotokea -"Kazi Vijana Mitaani"; ndipo utambue kwamba kuna watu walioajiriwa kufanya kazi ya usafi?
-"wanauza vitu vya kijinga"? Angalia ulivyo mpuuzi. Unataka wauze vinavyotokea huko kwenu ndio utambue kwamba wanauza vitu vizuri? Na kwa maana hiyo, una maana waTanzania wanaonunua vitu vya "kijinga" na wao unawadhyarau? Una akili timamu wewe? Eti unasema tujadili orodha!
-"wanasaidia viwanda vya China" Unajitokeza hapa kutaka wasaidie viwanda vya Kenya?
Uchafu huu ndio unaotaka tuujadili?
Sitaki unijue, kwa sababu huna msaada wowote kwangu, na kusema kweli, huna msaada wowote kwa Tanzania. Upo tu ukijitangaza uraia wako wa makaratasi ukisubiri kwamba siku moja Tanzania itamezwa na Kenya. Hilo halitatokea hata siku moja.
.
Sijasema popote kwamba wewe ni "Nurse" na wala kazi unayofanya haina msaada wowote kwangu.
Kwa hiyo hilo la "kutolipa kodi" ndilo unalonitafutia nije hapa nikubali kwamba wewe na rais mnakubaliana?Namshukuru Raisi kuwa mkweli na mwenye maono na kukubaliana na mimi "" Hawalipi kodi"
Kwa hiyo hilo la "kutolipa kodi" ndilo unalonitafutia nije hapa nikubali kwamba wewe na rais mnakubaliana?
Ni lini ulisikia nikitetea wasiolipa kodi, tena akheri ya hao wamachinga, kuna wengi wasiolipa kodi wanaotakiwa walipe kodi hasa!
Wazo zuri,kulitekeleza ndo kazi ngumu,hii ni nchi maskini sana yenye raia kama milioni60Huo ndio ukweli mchungu. Wamachinga wanaelemea taifa na kuchukua haki za walipa kodi wengine. Ni muda sasa kama Taifa kuwatafutia shughuli nyingine ya uzalishaji itakayo walipa na kuwaondoa barabarani.