Walokole ni noma.

Bujibuji Simba Nyamaume

Platinum Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
78,121
Reaction score
165,984
Ofisini tumepata kijana, kaja kuanza kazi.
Kwa kuogopa ukali wa foleni nikamwambia twende tukazuge sehemu kisha baadae tutaondoka.
Tukaenda kwenye bar iliyopo jirani na ofisi, mziki ulikuwa unapigwa kwa sauti ya chini, hali ya utulivu ilikuwa imetawala.

Mzee nikaagiza Mbuga baridi a.k.a Serengeti, jamaa akawa kimya bila kuagiza. Nikamwambia muhudumu asikilize jamaa atahitaji nini.
Kwa ujasiri jamaa akasema anahitaji chai ya rangi na maandazi mawili.
Nikazima, nilipozinduka nikakuta jamaa yuko bize na kuniombea na amelowa jasho chapachapa.

Nikamuuliza kulikoni akajibu eti bia yangu ilikuwa na mapepo, kwa hiyo yameniangusha baada ya kumuona yeye ndugu mlokole
 
Bujibuji, we si bar man, sasa ulienda kunywea wapi tena?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…