GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 59,949
- 119,212
Hivi inaingia akilini kweli kwa Kikundi fulani cha Waumini wanaojiita Walokole ( wenye kujifanya wanamjua Mungu kushinda Watu wote duniani ) kupenda kuimba Makanisani hasa nyakati za usiku huku wengine wakikesha na nyimbo zao ambazo kimsingi zinatufanya na sisi wengine tukose usingizi?
SWALI
Nyie mnaotuimbia kwa kutupigia makelele yenu usiku kwa kisingizio kuwa mnamuabudu na kumuimbia Bwana ( Mwenyezi Mungu ) je huyu Mungu muumba wetu alishawaambia kuwa na Yeye usiku huwa halali au haupendi usingizi hivyo atakuwa tu macho na masikio kodo akiwasikiliza nyie na makelele yenu kwa Wapendwa wake wanaojitambua ambao wamelala?
Hivi mnadhani Mwenyezi Mungu atakuwa wa hovyo hovyo kama mlivyo hivyo mida ya usiku na Yeye ahitaji kupumzika kusudi aweze kuamka akiwa vizuri na aendelee na Kazi yake ya Uumbaji?
Mnakera sana na tabia hii wanayo sana Walokole na hawa Watu sijui wa TAG na kidogo Walutheran lakini huwezi kuikuta hii tabia kwa Wakatoliki, Waanglikana na Wasabato.
WITO
Hizo nyimbo zenu muwe mnaziimba kuanzia Saa 10 jioni hadi Saa 12 jioni au basi mwisho uwe Saa 2 usiku lakini siyo mnajua kabisa kuwa hayo Makanisa yenu yapo Uswazinyo ambako stress zimejaa Kibao na Watu wamepumzika na nyie bado tena mnavurumisha Migitaa yenu, Vinanda vyenu, Drums huku mkiimba kwa Sauti za Fujo ambazo husindikizwa na kupewa ushirikiano na hali ya hewa tulivu ya mida hiyo ya kuanzia Saa 5 usiku hadi Saa 10 alfajiri.
Nimeamua kutema nyongo yangu leo ( kutoa dukuduku langu ) na kama mtanichukia na kuniambia lile neno lenu kuwa nina Pepo poa tu lakini naamini kwa dozi hii mujarab kabisa mtafikishiana hii taarifa na mtabadilika vinginevyo sisi mnaotupigia hiyo mikelele yenu usiku mnene tutatafuta njia mbadala na yenye ushirikiano kwetu ili tuwakomesheni kisha twende sawa.
Nimemaliza.