Walokole kugomea mawigi

Walokole kugomea mawigi

Jaji Mfawidhi

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2016
Posts
17,505
Reaction score
27,351
KUVAA MAWIGI NA KUJIPAMBA NI SAHIHI KIBIBLIA?

Ebu tuachane na hoja za ku-attack dhehebu au ku-attack mtu binafsi anazozitoa huyu jamaa,turudi kwenye hoja yake ya msingi

Je Sahihi kibiblia, kwa Mwanamke aliyeokoka Kuvaa Mawigi(Artificial Hair)? (ISAYA 29:16)

Je, Ni sahihi Kibiblia Mwanamke aliyeokoka Kujipamba kwa nje?(1 TIMOTHEO 2:9-10, 1PETRO 3:3-5)

Zaidi Sana,Je ni sahihi kwa Mama.Mchungaji, mama Askofu au mama Mtume,Kuvaa Mawigi na mapambo yote kama Yezebeli, Kahaba (2WAFALME 9:30)

{ISAYA 29:16}

[16]NINYI MNAPINDUA MAMBO; Je! Mfinyanzi ahesabiwe kuwa kama udongo; Kitu kilichofinyangwa kimnene yeye aliyekifinyanga , Hakunifinyanga huyu; au kitu kilichoumbwa kimnene yeye aliyekiumba, YEYE HANA UFAHAMU?

{1 PETRO 3:3-5} "KUJIPAMBA KWENU, KUSIWE KUJIPAMBA KWA NJE yaani, kusuka nywele; na kujitia dhahabu, na kuvalia mavazi;bali kuwe utu wa moyoni usioonekana, katika mapambo yasiyoharibika ; yaani, roho ya upole na utulivu, iliyo ya thamani kuu mbele za Mungu.Maana hivyo Ndivyo Walivyojipamba wanawake watakatufu wa zamani, waliomtumaini Mungu, na kuwatii waume zao.

{YEREMIA 4:30} "Na wewe, utakapotekwa, utafanyaje? Ujapojivika mavazi mekundu, UJAPOJIPAMBA MAPAMBO YA DHAHABU, UJAPOJITIA WANJA MACHONI,UNAJIFANYA KUWA MZURI BURE TU ; wapenzi wako wanakudharau; WANAKUTAFUTA ROHO YAKO."

Ebu toa maoni kwa misingi ya maandiko si kutetea dini au mama mchungaji wako ,Je ni sahihi sisi viumbe kumkosoa Mungu kwa uumbaji aliotuumba nao, kwamba ni waafrika ila tunajibadilisha ngozi kwa kujichubua, au Mungu ametupa nywele za asili yetu ya kiafrika ila sisi tunazikali na kuzibreech, au sisi tunajiongezakwa kuvaa mawigi?Je tunapofanya hivyo hatumkosoi Mungu?
 
Back
Top Bottom