Walletna hirizi, Sumbawanga mbali

Mnyamahodzo

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2008
Posts
1,943
Reaction score
1,015
Leo nikiwa pamoja na jamaa zangu tumetoka kumwangalia mgonjwa pale Muhimbili tuliisikia kauli ambayo ni ngumu ama yamkini naweza kusema inashangaza.

Ni kijana mwenye umri yapata miaka 30-33 akiwa kwenye ka-hoteli ka Bakhresa mara tu unapotoka geti la kuingilia Muhimbili. Huyu kijana alisikika akinungunika kwa machungu " Wallet yangu ilikuwa na hela nyingi na hirizi. Hela siyo tatizo, chukua tu hela lakini naomba nirudishi hirizi yangu; niliipata Sumbawanga, Sumbawanga mbali kwenda kuipata nyingine......Nirudishieni hirizi yangu tu."

Maoni yangu: Hivi hizi hirizi zina nini hadi watu wanatumainishiwa kuwa kuishi bika hizo, maisha hayapo? Ni jambo gumu sana kwangu kuwa katika zama hizi wako vijana wanasadikishwa nguvu iliyo ndani ya hirizi...si kama tutafika kule tunakotaka kwa wakati.
 
Ni kielelezo cha uozo wa wengi katika jamii yetu. Akili na mwii zimeshikwa kuzimu na wanategemea ibilisi kuwasaidia kuwapa ulinzi na mafanikio kupitia hirizi hizo. Ni akili zilizooza/ corrupt that need to be enlightened with the word of God.

Wabeba hirizi wengi ni watu wenye mashaka sana maishani na self-confidence iko chini sana. Wabeba hirizi wengi wana shida ya ukatili na roho yenye makovu (abused past).

Wabeba hirizi wengi ni waongo maishani, wabeba hirizi wengi hawana haya - ni wanafiki sana. Wabeba hirizi wengi hawajasoma na kama wamesoma wana akili ziko nyuma sana.

Huyo kijana mwoombeeni na ungetafuta njia ya kumsaidia psychologially so that you can restore his self esteem/integrity/dignity through the knowledge of him who trully saves!
 
Tetere, nakubaliana na wewe.
Cha ajabu utakuta si wafanyabiashara si wasomi bado wanaendekeza mambo hayo. Kama haitoshi kwenye jukwaa la siasa, hadi sasa kuna watu wawili wanaohusianishwa vifimbo vyao na namna fulani ya 'uhirizi'.
 
Mngemkemea huyo pepo

Nisome vizuri, tuliyemwona ni kijana (mtu) si pepo. Tafadhali usiudharirishe utu wa mtu kwa kuuita jina la kitu kingine ambacho mimi niliyekuwapo sicho nilichokuandikia.

Sawa, anaweza akawa kapagawa na pepo lakini sijasema hivyo lakini twaweza kujadili from that angle.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…