Labda wawekezaji kanjanja/Feki. Unajua kuna wawekezaji wapiga deal tu, na kuna wawekezaji hasa. Wale wapiga deal ndio huwa wanatuchungulia kwanza kuangalia weakness zetu kabla hawajaja, wanatumia mapungufu yetu kutengeneza faida. Siku ukushtuka utasikia ohoo ulisaini mwenyewe na blabla, yeye aliingia akijua hujui kitu fulani na aliwekeza hapo, lakini muwekezaji makini ambaye anaijua biashara yake hafanyi uhuni kama huo. Wenzetu huko wanasainishana mikataba huko WTO, mikataba imepimwa haina ujanjaujanja, haki na maslahi ya wahusika yanazingatiwa na kulindwa kisheria.Tunaweza kusema ni habari njema kwetu lkn kwa upande mwingine tuna sera ya viwanda, tutakimbiwa na wawekezaji, swali la kujiuliza je tupo tayari ku sustain hilo kwa muda gani.
Hawa wakwetu wanatuvizia, wanatupiga. Tukishtuka wanaanza kututisha mara nitakushitaki unilipe fidia, mara twende kwa arbitrator, ilimradi fujo tu.
Mkuu sasa ulevi na ujinga umeanza kututoka, yale ma hang over yanaishia hivyo tumeanza kujua jua tuko wapi, na tunafanya nini. Tunataka waje tukiwa sober, wasituibie.
Kabla hawajaja tuli stustain vipi mkuu?! Tutastastain for as long as anapatikana muwekezaji atakaye kubali masharti tuliyojiwekea. Tusikubali kubend kwa kila ajae, tuwe na msimamo wenye kulinda maslahi yetu. Nimesema huko juu tunaweza kuwa wamwisho sokoni au wa mwisho kuuza lakini tuuze kwa faida.