Wall master

Wall master

Joined
Nov 12, 2013
Posts
29
Reaction score
16
Habari zenu wadau,
Hii ni kwa wazoefu kwenye maswala ya ujenzi na mafundi wa kupaka nyumba rangi. Naombeni mnijuze hii wall master ni kitu gani na ina umuhimu gani? Manake nna quotation hapa ya vifaa vya rangi bei zake zimerange laki tatu mpaka laki sita. Bt hii wallmaster peke yake cost yake imekwenda mpaka milioni moja na nusu, kwa mahesabu ya 150,000@ kwa ndoo moja.
Karibuni kwa mawazo/ ushauri.
Natanguliza shukrani.
 
Ngoja nijaribu kueleza kidogo kama utanielewa.
Ni aina fulani ya unga ambao ukichanganganywa na kimiminika unakuwa kama gundi hivi, halafu kuna aina fulani ya vimawe vidogo sana unachanganywa pamoja ,then unapakwa kwenye ukuta wa nyumba badala ya rangi na kuifanya nyumba muonekano wa nje inakuwa na michirizi ya mistari ukutani.Kama uko Dar,angalia Hotel ya Grand Villa.Ni material nzuri, inaifanya nyumba kupendeza.
 
Nimeshaifahamu kuna baadhi ya nyumba nimeona zipo hivyo. Ninakushukuru sana. Ubarikiwe, siku njema.
 
Yaaa. Hiyo gharama ni sawa. Kama Nyumba yako ni kuishi Mwenyewe utaifurahia sana.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom