Walitaka ya kuzungusha mikono, Magufuli anatuletea mabadiliko ya kweli wanapiga kelele

singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,394
1,536
Takribani miezi saba au nane iliyopita tulishuhudia wimbi la wanasiasa wakizungusha mikono hewani wakidai kuwa wanataka mabadilko, huku wakijidai mbele ya watanzania wenzao kuwa kuzungusha mikono ni mwanzo wasafari ya kuelekea katika mabadilko.

Wakaimba sana mabadilko, mabadilko, mabadiko mpaka masikio ya wenzao yakaziba, upande wa pili uliongozwa na jemedari Dk. John Pombe Magufuli ukawaambia watanzania waliokuwa wakihadaiwa kwamba mabadilko ya kwelia hayawezi kuletwa wala kupatikana kwa kuzunmgusha mikono, bali yataletwa na watu wenye nguvu na afya njema wanaoweza kupiga push up zaidi ya 10 kwa dakika bila kuchoka.

Watanzania walio wengi wakazinduka kutoka katika usingizi wa hao wazunguusha mikono na kumwelewa Dk. Magufuli na kumpa kura za kutosha kabisa, leo wazungusha mikono hawataki kuyaona mabadiliko yakitokea, wanapiga kelele wakitaka kutubakisha watanzania kule kule ambapo wao wenyewe walikukataa miezi saba au nane iliyopita.

Serikali ya Dk. Magufuli inamtaka kila mmoja atimize wajibu wake wa kufanya kazi yake kikamilifu na kwa ufanisi mkubwa kabisa ili kuleta tija kwa taifa letu, bila kujali nafasi zao wazungusha mikono hawa wanapiga kele wakitaka waendeleze mipasho yao ndani ya bunge kwa kuuza sura hali ya kuwa majimboni hatuwaoni kana kwamba mipasho hiyo na kuuza kwao sura kutawaongezea shibe na kero zilizowakabili watanzania katika majimbo yao.

Tumeona pia Dk. Magufuli na serikali yake wakiwawajibisha watumishi wa umma waliowazembe na wasiojiwajibika ipasavyo bado waziungusha mikono wakapiga kelele wakiwatetea kwa kusema wanaonewa.

Jinge amabalo nashindwa kuwaelewa kabisa hawa wazungusha mikono ni hatua ya Rais kubadlisha matumizi katika maeneo kadhaa na kupeleka kwenye umuhimu zaidi kwa mfano pesa za sherehe za uhuru zilitumika kujenga barabara ya Moroco jiji Dsm amabayo ilikuwa kero kubwa kwa wapitao kwa barabara hiyo vile vile jambo kama hilo likafanyika kule Mwanza, lakini bado wazungusha mikono wakaendelea na makelele yao ooh Rais anaingilia mambo ambayo siyo ya kwakwe.

Ninachojiuliza wzungusha mikono hawa walikuwa wanahubiri mabadiliko gani? au walikuwa wanatulaghai watanzania huku wakiwatetea mafisadi na wahujumu uchumi au walikuwa wachumia tumbo tu na hawapo kwa maslahi ya watanzania wengi?

Nimalizie kwa kuawaambia wazungusha mikono kuwa watanzania tupo makini na tunalizishwa na kasi ya Magufuli na utumbuaji majipu na kama hawatakuwa kuwa makini wataendelea kuwatetea mafisadi na wazembe wasije kupoteza muda wa kugombea 2020 kwani watarajie aibu na fedhea kubwa kuwakuta amabayo haijawahi kuwakuta katika historia ya vyama vingi katika nchi hii.
 
Tatizo la wazungusha mikono ni kunyimwa hoja ya kisiasa ambayo inauzika kisiasa katika jamii
 
Back
Top Bottom