Waliowahi kushika uongozi wa serikali ya wanafunzi vyuo vikuu wafuate nyayo za Zitto Kabwe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waliowahi kushika uongozi wa serikali ya wanafunzi vyuo vikuu wafuate nyayo za Zitto Kabwe

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by skalulu, Jun 4, 2012.

 1. s

  skalulu Member

  #1
  Jun 4, 2012
  Joined: Apr 30, 2012
  Messages: 78
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Wana JF, kuna Vijana wanaharakati enzi zile miaka ya 2000-2003, Chuo Kikuu cha Dsm tuliwahi kuwa na Viongozi shupavu sana ambao waliwahi kuweka ndani pamoja na kutimuliwa Chuo Kikuu cha DSM kwa kuongoza migomo ambayo tulifukuzwa chuo kizima na tukarudi nyumbani takribani miezi mitatu,

  Uongozi wa DARUSO ulikuwa unaongozwa na msaliti mmoja aliyekuwa anaitwa Julius Kusaja, ambaye alijitoa kwenye mgomo na baada ya hapo katibu wake Mr. Gervas Mkili na Makamu aliongoza migomo mpaka wakawekwa ndani na baadaye wakatimuliwa, ila kwa baadaye tuligoma tena wakarudishwa Chuo.

  Kati yao walikuwemo Zitto Kabwe, Gervas Mkili mwenyewe, Julius Rugemarila, Waziri fulani wa Fedha jina ilimenitoka, na wengine wengi. Lakini ni Zitto peke yake ambaye tayari matunda yake tunayona hadi sasa, ila wengine mlipotelea wapi baada ya Chuo maana mlikuwa very strong kuliko hata Zitto kama vile Gervas Mkili ( Shy/Khm) na Julius Rugemarila (Mwz/Bukoba).

  Je kuna mwana JF yoyote ambaye anatarifa nao? tunapenda wajitokeze ili tuendelee na hii M4C ili tuweze kuwabadilisha wa Tz na kujihakikishia ushindi wa kishindo 2015, twendeni tukiunganisha nguvu kwa pamoja siyo msubiri tu 2015 baada ya ushindi ndo mjitokeze.

  Ila yeye Kusaja nadhani yuko kigambagamba alitusaliti na akabakishwa UDSM utawala.

  Nawasilisha ili ujumbe uwafikie michango yao ni muhimu sana.
   
 2. S

  Sheshejr JF-Expert Member

  #2
  Jun 4, 2012
  Joined: Jan 14, 2012
  Messages: 435
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Ngoja waje wenyewe, wengne miaka hiyo ndo tunaingia o-level.
   
 3. t

  thatha JF-Expert Member

  #3
  Jun 4, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Shujaa Gervas Mkili alifariki dunia miaka michache iliyopita, alikuwa headmaster wa Green Acres Sec School Dar es salaam. Julius Rugemalira yuko Dar ni mwajiriwa wa mamlaka ya elimu Tanzania(TEA). Mwaka 2010 aligombea ubunge jimbo la Nkenge na kushindwa na Asumpta(mbunge wa sasa) kwenye kura za maoni ndani ya CCM. Alisababisha kupungua sana kura za Deodorus Kamala ambaye alikuwa mbunge wa jimbo hilo.
   
 4. M

  Msendekwa JF-Expert Member

  #4
  Jun 4, 2012
  Joined: Mar 11, 2012
  Messages: 440
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mkili alimwakyembiwa au ilikuwaje?
   
 5. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #5
  Jun 4, 2012
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,435
  Likes Received: 3,782
  Trophy Points: 280
  Wapi Sweke?
   
 6. TUMBIRI

  TUMBIRI JF-Expert Member

  #6
  Jun 4, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 1,934
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Rejao hivi na wewe ulikuwa unagoma kweli enzi hizo maana uliniambia miaka ya 2000 - 2003 ndio ulikuwa pale UDSM?
   
 7. montroll

  montroll JF-Expert Member

  #7
  Jun 4, 2012
  Joined: Jul 31, 2011
  Messages: 288
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  Oh yeah, plz kuna wapiganaji makini wa miaka ya tisini katika vyuo vikuu waliopigania mfumo wa vyama vingi na kupinga cost sharing katika vyuo vikuu. Udsm,ardhi,sua,mzumbe na dar-tec. Kwa kweli walikuwa vichwa darasani na nje ya darasani lakini serikali kama kawaida iliwafrustrate kwa kuwafukuza vyuoni na kuwanyima kila nafasi ya kuendelea isipokuwa kwa wale ambao wazazi wao walikuwa na uwezo au majina na nafasi kubwa.
  Wana jf wanao jua hawa mashujaa waliosahauliwa watuambie wako wapi na wanafanya nini sasa, kulikuwa na vichwa vya ajabu sana pale udsm na sua.
  mzee ruksa alipata shida sana na vijana wale jinsi walivyokubalika na wasomi wenzao kwa maslahi ya taifa hili, waliweza kupindua serikali zao zilizokua vibaraka na kuunda serikali za vyuo imara. Waliadhibiwa kwa kutetea maslahi mapana ya taifa.

  Anaye wafahamu atujuze tafadhali kwa manufaa ya kumbukumbu na historia ya mwanzo wa mapambano mapya ya ukombozi wa pili wa taifa hili baada ya uhuru.
   
 8. M

  Msendekwa JF-Expert Member

  #8
  Jun 4, 2012
  Joined: Mar 11, 2012
  Messages: 440
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Sio kwa kumbukumbu za historia tu, pia kufanyike taratibu za kuwakwamua km wamefungiwa milango yote ya riziki na "system"
   
 9. montroll

  montroll JF-Expert Member

  #9
  Jun 5, 2012
  Joined: Jul 31, 2011
  Messages: 288
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  Ni kweli mkuu, tauanze kwa kuwataja nakujau walipo sasa, wa udsm, sua,dar-tec,ardhi,mzumbe nk. Kisha tuwatambue wale ambao wanahitaji suport ya aina moja au nyingine.
   
 10. k

  ksalama0 Member

  #10
  Jun 5, 2012
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 55
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Kusaja yupo UDOM muda mrefu kuanzia 2007 mpaka sasa.
   
 11. N

  Njoka Ereguu JF-Expert Member

  #11
  Jun 5, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 822
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 35
  Aisee Mungu ailanze roho Marehemu Akili mahala pema peponi. Kijana kwa kweli alionyesha ushupavu wa hali ya juu sana katika Mgomo wa mwaka 2000 pale revolution square na baadaye Nkuruma Hall, Makamu wa Rais wa Daruso alikuwa DADA moja mrembo sana tu.

  Aliunganisha nguvu za wanachuo wote baada ya kusaja Kutusaliti.

  Wapo wengine pia kama kina Kengele alikuja kuwa Rais Daruso 2002/2003 kama sikosei, alikuwa mpiganaji wa namna fulani sema alikuwa ulabu sana.
   
 12. Kashaijabutege

  Kashaijabutege JF-Expert Member

  #12
  Jun 5, 2012
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 2,699
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  UDSM (Wanafunzi 10 waliofukuzwa tarehe 10 February 1992)

  1. James Mbatia-Mbunge Simu: 0787 979068
  2. Mosena Nyambabe-Mfanyabiashara (anakaa Ukonga Mombasa)-Amepambana mara 3 na Dr. Wanyancha katika ubunge huko Serengeti. Kwa mara ya mwisho aligombea kwa tiketi ya CUF.
  3. Kelvin Mmari-Lecturer Oregon University huko Marekani. Ana uraia wa Marekani na kati ya wataalam wa kompyuta wanaoheshimika huko Marekani.
  4. Fabian Lutalemwa-Sina habari naye tangia miaka ya 90.
  5. Ludovick Bazigiza-Marehemu
  6. Idrisa Ruta Alnoor-Marehemu
  7. Jasson Kaishozi-Marehemu (Alikuwa wakili wa Serikali kesi ya Zombe)
  8. Aroun Kimaro-Marehemu (Alikuwa Daktari Bingwa Zimbabwe na Mfanyabiashara mashuhuri. Alipitia mkono wa Mchungaji Mtikila)
  9.Rwekamwa Rweikiza-Mhasibu. Alipata CPA mwaka 1996, nimesoma naye MBA pale UDSM na sasa anasoma digrii ya kwanza ya Sheria OUT. Vile vile ana PGDHRM ya IFM. Yuko Dar (Simu-0754 275 305)
  10. Kimweri-Marehemu (Alimalizia Digrii yake ya uchumi Makerere University. Alifariki kwa ajali ya gari miaka ya 90 akiwa njiani kuelekea Zimbabwe kwa Kimaro)

  Wengine

  1. Matiko Matare-Aliongoza mgomo wa mwaka 1990 uliosababisha chuo kifungwe kwa mwaka mmoja. Aliacha UDSM kwa hiari kipindi kile ambapo kuliwa na njaa kali kule Musoma. Alimwambia mkuu wa Chuo (Luhanga) ampe nauli aende nyumbani kwa sababu hakuona haja ya kusoma wakati ndugu zake wanakufa kwa njaa, vingineyo angejinyonga. Wakati huo alikuwa mwaka wa 3. Mkuu wa Chuo alitii amri. Baadaye alijiunga OUT na kuwa mwanafunzi wa kwanza kumalizia digrii ya sheria kwa miaka 3. Baadaye alisoma MA (Distance Learning) hapo hapo OUT. Yuko Songea. Namba yake ni 0757 282151. Anajiandaa kurudi katika siasa kwao mkoani Mara.


  DIT

  1. Mtoka Mtwangi-Sina mawasiliano naye tangia miaka ya 90. Alimalizia Advanced Diploma yake Kenya Polytechnic College.
   
 13. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #13
  Jun 5, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  RIP Mkili
  namkumbuka sana huyu kaka nakumbuka na tukio la prof Mshana kuwaacha pale ubungo mataa na kukimbia
  alipotakiwa kuongozana na viongozi wa daruso ili kwenda polisi kuwatoa kina Mkili na wenzie waliowekwa ndani
  enzi hizo nlikuwa mwaka wa kwanza UDSM enzi hizo chuo kikiwa na heshima yake.
  bofya hapa kuona uzi wa mwenzetu alietupasha kifo cha gervas

  https://www.jamiiforums.com/matangazo-madogo/38112-gervas-mkili-is-no-more.html
   
 14. Kashaijabutege

  Kashaijabutege JF-Expert Member

  #14
  Jun 5, 2012
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 2,699
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Simu ya Mosena Nyambabe ni 0754 373 203
   
 15. R

  Rwechu Member

  #15
  Jun 5, 2012
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 85
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Kengele alikuwa Makamu wa Rais, Rais alikuwa anaitwa John Samwel
   
 16. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #16
  Jun 5, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Aisee umenikumbusha mbali, nakumbuka hilo Sakata lilianzia Pyongyoung S. Korea pale viongozi wa DUSO walipowekwa detention!

  Nimefurahi kusikia Matiko bado yuko hai.
  Pia akina Mkenda yuko UDSM ingawa alikuja kuacha mambo ya Siasa
  Pia Alfaxid Lugora MB.(Mwibara) enzi tuliomfanya yule PS wa Elimu Ngonyani afukuzwe na mzee Ruksa baada ya kushindwa kuongea Kingereza Nkurumah na kuomba kuongea kiswahili takapinga akibidi arudi hata bila kuongea alichotumwa na Mwinyi.
   
 17. manuu

  manuu JF-Expert Member

  #17
  Jun 5, 2012
  Joined: Apr 23, 2009
  Messages: 4,063
  Likes Received: 9,673
  Trophy Points: 280
  Very interesting.
   
 18. T

  The State Member

  #18
  Jun 5, 2012
  Joined: Mar 19, 2012
  Messages: 14
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Matiko Matare hakuacha kwa hiari ila alifukuzwa baada ya kuongoza mgomo mkubwa wa 1990 uliotikisa nchi kwani ulikuwa una lengo la kumwondoa Mwinyi madarakani. Sikumbuki kama Luhanga ndiye alikuwa VC. But I remember VC alikuwa Mmari. Luhanga ameanza 1991. Matiko alipelekwa kijijini kwao kwa helkopta ya serikali na kuwekewa kizuizi cha kutotoka kijijini kwao for 5 yrs. Baada ya 5yrs serikali iliendelea kumfuatilia sana kupitia idara ya usalama wa taifa hata alipokwenda kufundisha Musoma techical sec school (zamani maarufu kama musoma alliance) na baadaye mwembeni sec school hapo hapo musoma.baadhi ya watu waliokuwa wanamfuatilia ninawafahamu.Yeye nimewahi kuongea naye mara nyingi lakini nashukuru kwa kufahamu alipo sasa. Frankly speaking, yule jamaa ana uwezo mkubwa kichwani.
   
 19. Kashaijabutege

  Kashaijabutege JF-Expert Member

  #19
  Jun 5, 2012
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 2,699
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Mkuu ulikuwepo siku ile tulipoandamana mpaka Ikulu kuishinikiza serikali kuwarudisha madaktari wa Muhimbili? Yalikuwa ni maandamano makubwa kufanyika kabla ya kuwepo kwa mfumo wa vyama vingi. Wewe ulikuwa Hall gani?
   
 20. Kashaijabutege

  Kashaijabutege JF-Expert Member

  #20
  Jun 5, 2012
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 2,699
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Mkuu, wale wote waliosimamishwa mwaka 1990 walirudishwa. Walikuwemo kina Andrew Kazimoto, Marehemu Lubega (aliongoza FAT), Eng. Kakoko (Tanroad Arusha), n.k. Alirudi mwaka 1993 kumalizia digrii yake. Mpigie simu upate uhakika. Kaka, mimi Matare ni best wangu, hivyo najua yote yanayomhusu.
   
Loading...