Athari za ufuasi wa viongozi katika vyama vya siasa badala ya ufuasi wa itikadi, misingi, madhumuni

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
ATHARI ZA UFUASI WA VIONGOZI KATIKA VYAMA VYA SIASA BADALA YA UFUASI WA ITIKADI, MISINGI, MADHUMUNI NA FALSAFA.

Prof Lipumba wa CUF na Zitto Kabwe wa CHADEMA Wana alama hizi.....

Aliyekua Mwenyekiti wa The Civic United Front (CUF) Taifa prof Ibrahim Haruna Lipumba aliyejiuzulu uenyekiti wake agost 2015 ameonesha kulilia kiti cha Uenyekiti huo katika harakati za uchaguzi tarehe 21/08/2016.

Miezi miwili kabla ya tarehe ya uchaguzi wa marudio wa kumtafuta Mwenyekiti mpya wa CUF, Makamu Mwenyekiti CUF, wajumbe wa baraza kuu yaani tarehe 21/08/2016 Prof Lipumba aliitangazia dunia kwamba anataka kurejea katika nafasi yake ya uenyekiti wa CUF taifa.

Tangazo lake hilo kwa dunia kupitia vyombo vya habari vya ndani na nje ya nchi Prof Lipumba alidai kwamba ameona kwamba CUF inapoteza mvuto bara na visiwani, CUF imeshindwa kutetea ushindi wake wa urais Zanzibar, CUF imeshindwa kujiimarisha zaidi na akamalizia kwamba anataka kurudisha CUF yenye nguvu...

Prof Lipumba anasahau kwamba CUF katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 ilipata madiwani wachache Sana na hakuna Halmashauri ambayo CUF iliongoza upande wa Bara na ilikua na wabunge wasiozidi 3 bara . Leo CUF ina madiwani katika Mkoa wa Tanga, Lindi, mtwara, Tabora, Dar Es Salaam nk. Wabunge hawa wameongeza ruzuku ya CUF na hawana damu wala jasho la Prof Lipumba..

Prof Lipumba akiwa mgombea urais mwaka 2010 alisaliti dhamira ya chama chake CUF kwa kuhubiri udini kwa kusema kwamba yeye Lipumba anamuunga mkono Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuwa ni muislamu mwenzake. Yaani aliacha lengo la kushinda uchaguzi na kuunda serikali akaanza kufanya Kazi ya kumpinga Dk Slaa mkristo na kumuunga mkono muislamu mwenzake Jakaya Kikwete. Usaliti wa wazi tena.

Lipumba aliamua kusaliti umma wa wapenda mabadiliko mwaka 2015 akaelekea nchini Rwanda kwa Kile alichoita kufanya tafiti na kubaki mwanachama wa kawaida wa CUF. Alionekana kusifu kwamba Lowassa ni fisadi na akahubiri wazi wazi kwamba ni heri Magufuli ashinde. Lipumba alifika ikulu ya magogoni mara kadhaa mwezi novemba 2015 kuonana na Rais Magufuli kwa mambo ambayo aliyajua yeye na Rais Magufuli. Wachambuzi wa mambo ya siasa walihusianisha ziara ya Lipumba ikulu na uteuzi wa ushauri wa kiuchumi au uwaziri wa uchumi na mipango. Lakini Baraza la mawaziri lilipotangazwa, jina la prof Lipumba halikuonekana na ndipo prof Lipumba akaanza kufika makao makuu ya CUF na kutoa matamko ya kutoridhishwa na Rais Magufuli mwezi Machi wakati mwezi disemba alisifu na kutukuza utawala wa Magufuli. Alitoa matamko ya kutaka CUF ipewe ushindi wake Zanzibar...

Baadaye ndipo akatangaza kutaka kurejea katika nafasi yake ya uenyekiti wa CUF makao makuu ya CUF na nje kukiwa na wanaosadikiwa kuwa wanachama wa CUF wafuasi wa Lipumba waliovalia fulana (t-shirts) zenye maandishi yaliyosomeka "LIPUMBA KWANZA CHAMA BAADAYE", "LIPUMBA KWANZA MAMBO MENGINE BAADAYE "," LIPUMBA TUNAIMANI NA WEWE "

Maneno hayo yaliambatana na nyimbo za kumsifia, kumtukuza na kumuabudu Prof Lipumba. Matamko mbalimbali ya wanaoitwa wazee wa CUF Temeke, wanachama wa CUF mkoa wa Dar Es Salaam, wanachama na Viongozi wa CUF Tabora na maeneo mengine. Hatua zote hizi na sarakasi nyingine nyingi zilikua ni kutaka prof Lipumba arudishiwe uenyekiti kwa namna yoyote ile hata kwa kuvunja katiba ya CUF.

Sarakasi hizo za Prof Lipumba na wafuasi wake nazifananisha na sarakasi za kisiasa za aliyekua Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA bara Zitto Kabwe mwaka 2013, 2014 na 2015.

Tarehe 23/11/2013 kamati kuu ya CHADEMA baada ya kufanya Vikao tarehe 21/22/11/2013 iliazimia naibu Katibu Mkuu CHADEMA Zitto Kabwe, Mjumbe wa kamati kuu CHADEMA taifa Prof Kitila Mkumbo na Mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Arusha Samson Mwigamba kuvuliwa nyadhifa zao ndani ya CHADEMA na kujieleza ndani ya siku 14 kwa nini wasifukuzwe uanachama wa CHADEMA.

Zitto Kabwe alianza kuyumbisha chama kwa kuandaa vijana waliojiita wanamabadiliko, kuandaa Viongozi waliojipachika Vyeo na kutoa matamko makali na matusi, wanachama mbalimbali waliochoma kadi za CHADEMA maeneo mbalimbali nchini.

Tarehe 24/11/2013 vijana waliojipachika Vyeo vya Viongozi wa vyuo vikuu wakiongozwa na Nyakarungu walitoa tamko kali dhidi ya CHADEMA kwa kupinga maamuzi ya Kamati kuu. Nyakarungu alisema yeye ni Katibu wa shirikisho la wanafunzi wa Chadema chuo kikuu cha Dar Es Salaam yaani Chadema Student's organization (CHASO UDSM). Tamko hili liliniletea shida Sana maana mimi ndiye nilikua Katibu wa CHASO UDSM mwaka 2013. Hii ilitulazimu wanafunzi wa vyuo vikuu mkoa wa Dar Es Salaam Chini ya Himida, Gwamaka Mbughi, Lumola Steven Kahumbi, Julius Marco kutoa tamko kukanusha tarehe 27/11/2013.

Vikao vya usiku na mchana vya vijana wa Zitto kabwe wakiongozwa na Habib Mchange, Nyakarungu na wenzao walizunguka nchi nzima wakishirikiana na Mbaruku wa Tabora kushinikiza baadhi ya Viongozi kujiuzulu uongozi, kutukana chama nk.

Baadaye kamati kuu ilimwita Prof Kitila Mkumbo kujitetea mbele ya kamati kuu, akajieleza na maelezo yake hayakujitosheleza na hivyo kuvuliwa uanachama huku Samson Mwigamba aligoma kuhudhuria kikao hicho kwa Kile alichoita ilikua siku ya ibada (Jumamosi) siku ya sabato kwake kama muumini wa Kanisa la Sabato...

Zitto Kabwe aliamua kufungua kesi Mahakama Kuu kanda ya Dar Es Salaam kutaka apewe na Katibu Mkuu maazimio ya kamati kuu ya CHADEMA na tuhuma zake Ili kukata rufaa Baraza kuu CHADEMA dhidi ya maamuzi ya kamati kuu. Kesi hiyo ilifunguliwa tarehe 02/01/2014 chini ya mwanasheria /Wakili wake Albert Msando.

Kesi ilitajwa tarehe 03/01/2014 ambapo Zitto Kabwe na wafuasi wake walikua tayari wameshanunua fulana mpya za CHADEMA zaidi ya 1000 na vijana hao kujaa Mahakama Kuu huku wakivaa t-shirt mpya wakati kandambili /ndala zikiwa fananisha, zimeisha kweli kweli na suruali na bukta chafu. Kwa KIFUPI vijana wa Zitto walikua mateja waliokusanywa maeneo mbalimbali ya Dar Es Salaam na kuvalishwa fulana za CHADEMA huku wakiwa na mapanga, visu na mawe.

Vijana wa Zitto kabwe ambao walijitenga na wanachama halali wa Chadema walikua wakiimba nyimbo kwamba ZITTO KABWE KWANZA CHADEMA BAADAYE. Walikua na mabango yaliyosomeka "ZITTO KWANZA CHADEMA BAADAYE"

Baada ya mapambano makali ya kisheria kati ya wakili wa Zitto Albert Msando dhidi ya Mawakili wa Katibu Mkuu wa CHADEMA Dk Slaa, Tundu Lissu, Peter Kibatala na John Mallya na kesi kuahirishwa, wafuasi wa Zitto kabwe walianza kuzomea wanachama wa Chadema.

Hali hiyo ilipelekea mapambano makali Sana.Nakumbuka mawe yalitumika, visu, mapanga na ngumi. Nakumbuka vizuri niliokolewa mikononi mwa teja mwenye panga na meya wa kinondoni Boniface Jacob. Nilikua katikati ya mateja na niliokolewa na Boniface Jacob. Ben Saa Nane aliokolewa na Philipo Mwakibinga wakati akishambuliwa na vijana hao wa Zitto waliotaka kumpora Laptop na IPAD yake. Jeshi la polisi lilitutawanya kwa mabomu na risasi za moto. Binafsi nilipoteza sh laki Tatu na vitambulisho kadhaa...

Hali hiyo ya kisiasa, iliifanya CHADEMA kuandaa OPERATION iliyojulikana "OPERATION M4C PAMOJA DAIMA" ambapo Choppa(Helkopta) Tatu zilirushwa ANGANI na Chadema.

Mbowe akiwa Kigoma alitupiwa mawe na walioitwa wafuasi wa Zitto kabwe. Dk Slaa alipondwa mawe Tabora na Kigoma. Zitto Kabwe alikwenda Kigoma kufanya mikutano ya hadhara kueleza Kile alichoita ng'ombe akiumia malishoni hukimbilia zizini. Aliishtaki Chadema kwa wananchi wa Kigoma...

Mtikisiko huo ulipelekea Makamu Mwenyekiti CHADEMA Taifa bara Said Arfi kujiuzulu Nafasi yake, Viongozi wengine wa mikoa ya Tabora, Kigoma nk walijiuzulu huku bendera mbalimbali za CHADEMA zikichomwa moto, bendera zikishushwa na ofisi za CHADEMA zikifungwa...

Nimeeleza haya kwa kuwa katika vyama vya siasa hasa Tanzania, wanasiasa wanatengeneza wafuasi wao badala ya wafuasi wa itikadi, falsafa, misingi, sera na kanuni za chama cha siasa kwa lengo la kuunda serikali. Viongozi hao wanapoachana na siasa, wanapofariki,kuhama chama, kujiuzulu au kufukuzwa uanachama wa chama husababisha Mtikisiko wa chama husika.

Zitto alitikisa CHADEMA mwaka 2013, 2014 na 2015, Edward Lowassa alitikisa Ccm mwaka 2015, Lyatonga Mrema alitikisa NCCR MAGEUZI mwaka1999, 2000 nk

Anachokifanya Prof Lipumba CUF kwa kukataliwa kwa kura zaidi ya 400 na kupata kura zisizozidi 120 na kulazimisha kupewa uenyekiti kwa nguvu ni muendelezo wa athari za kuwa na wafuasi ndani ya chama.

Vyama vya siasa visimamie kuwajenga wanachama wake katika sera, itikadi, falsafa, misingi, madhumuni na kanuni zake.

Lipumba akae pembeni, hana mvuto kwa umma, amepoteza radha ya MAGEUZI nchini. Amejaa usaliti na unafiki mkubwa. Haaminiki na hakubaliki. Aheshimu demokrasia. CUF bila Lipumba inawezekana.
 
ni mpuuz kama wew ndo utaamin profesa hakuleta mafanikio, serikali za mitaa cuf ilifanya VIZURI, ambapo ndo msingi wa hao madiwani na wabunge sehem mbalimbali, mafanikio ya kisiasa huwezi kuyapima kwa mwezi mmoja bila kuzingatia investment iliyofanya kipindi cha nyumba , na hata slaa na mbowe wanajua kufanya kwao VIZURI kuna misingi iliyowekwa , ndo tunajivuniea 2015
 
Back
Top Bottom