Waliouawa Darfur: JK atoa tamko kali

Waliouawa Darfur: JK atoa tamko kali

Iyokopokomayoko

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2011
Posts
1,785
Reaction score
443
Waliouawa Darfur: JK atoa tamko kali

968858_597688873595087_1696276908_n.jpg


Dar es Salaam. Rais Jakaya Kikwete ameutaka Umoja wa Mataifa (UN), kuruhusu kutumika kwa mtutu katika operesheni za kulinda amani zinazoendelea.

Alitoa kauli hiyo jana baada ya kutoa heshima zake kwa wapiganaji saba wa Tanzania waliokuwa Darfur, Sudan katika operesheni ya kulinda amani ya UN na Afrika (Unamid) ambao waliuawa na kundi linalodaiwa la wanamgambo wa Janjaweed wanaoungwa mkono na Serikali ya Sudan inayoongozwa na Rais Omar al-Bashir.

Wapiganaji waliouawa ni Oswald Chaula kutoka 42KJ Chabruma, Songea, Peter Werema (44KJ Mbeya), Fortunatus Msofe (36KJ Msangani, Pwani), Rodney Ndunguru (92KJ Ngerengere), Mohamed Juma (94KJ Mwenge), Mohamed Chukilizo (41KJ Nachingwea) na Shaibu Othman (MMJ- Upanga).

"Lazima nikiri kuwa taarifa hiyo ya vifo vya vijana wetu ilinihuzunisha, kunisikitisha na kunikasirisha. Kwa nini watu wa Darfur wawaue wanajeshi wetu ambao wamekwenda kule kuwasaidia wapate utulivu ili kunusuru maisha yao, kuwaondolea wasiwasi na kuwawezesha wafanye shughuli zenye tija kuendesha maisha yao?

"Moja kwa moja sikusita kuamini kuwa waliofanya hivyo ni watu wahalifu. Tangu uhuru ni sera ya nchi yetu kutetea wanyonge dhidi ya ukoloni, ubaguzi, uonevu, dhuluma na watu wote walioko katika mazingira hatarishi Afrika na duniani. UN ifanyie marekebisho sheria ili majeshi yanayolinda amani yawe na nguvu za kujihami ili kuzuia maafa yanayoweza kujitokeza."

Hivi karibuni, Msemaji wa Unamid, Chris Cycmanik alimwambia mwandishi wetu: "Majeshi ya UN mjini Darfur yanaweza kufanya kazi chini ya Kifungu cha VII ambao inaruhusu kutumia nguvu lakini kwa hali iliyopo hawafanyi hivyo," alisema.

Rais Kikwete alisema eneo hilo ni hatarishi kwa sababu hadi sasa watu 41 kutoka katika nchi mbalimbali wameuawa wakati wakilinda amani huku wengine 55 wakijeruhiwa tangu mpango wa kulinda amani ulipoanza mwaka 2007.

"Tumeshawasilisha UN maombi kutaka Kifungu namba Sita cha kulinda amani kibadilishwe na kitumike Kifungu namba Saba ambacho kinawataka askari kujihami pindi wanapovamiwa na maadui," alisema.

Alisema tayari amewasiliana na Rais al-Bashir akimtaka kufanya uchunguzi na kuwachukulia hatua kali wote waliohusika na tukio hilo huku akiwataka wanajeshi kutokata tamaa kwa tukio hilo na kulichukua kama changamoto katika kujilinda na kuwabaini maadui.

Aliwapa pole wafiwa na kusema Serikali na wananchi wote wapo pamoja katika kipindi hiki kigumu na kuwataka kuwa na subira. Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha alisema kitendo cha waasi kuwaua wanajeshi saba wa Tanzania ni mkakati wa vikundi vya waasi kuhakikisha kuwa jitihada za kuleta amani zinagonga mwamba.

Mkuu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Jenerali Davis Mwamunyange alisema askari hao pamoja na wengine walikuwa wakisindikiza msafara wa walinzi wa amani uliokuwa ukitoka katika kambi yao karibu na Mji wa Nyala.

Alisema walipofika kilometa 25, katika eneo la Khor Abeche walivamiwa kwa kushtukizwa na kikundi cha watu wachache na kwa sababu hawakuwa na silaha za kujihami, walishindwa kujitetea na kusababisha vifo hivyo.

Simanzi, vilio vyatawala

Rais Kikwete aliwasili katika Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa saa 11.10 asubuhi na kupokewa na Makamu wa Rais, Dk Mohamed Gharib Bilal, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha na Jenerali Mwamunyange.

Muda mfupi baadaye, malori saba kila moja likiwa na mwili wa wanajeshi hao yaliwasili katika viwanja vya wizara hiyo.

Wakati miili hiyo ikiteremshwa kwa ajili ya kuaga, wafiwa ambao awali, walikuwa wametulia kwenye viti walianza kulia.

Rais na mkewe, Salma walianza kutoa heshima zao na kisha kuwapa mkono wa pole wafiwa.

Askari wawili wa JWTZ walizirai wakati utoaji huo wa heshima za mwisho ukiendelea na walibebwa na wenzao kwenda kupatiwa huduma ya kwanza.

Mamia ya wakazi wa Dar es Salaam walijitokeza katika viwanja hivyo kiasi cha wengine kukosa nafasi ya kuingia ndani hivyo kulazimika kukaa nje hadi miili hiyo ilipoondoshwa tayari kwa kusafirishwa sehemu mbalimbali kwa maziko.


Source: Habari Leo
 
Yaani upo shambani harafu huna jembe, panga au kikapu....!!!? Kazi ipo kiukweli...
 
Waliofanya kitendo hicho ni magaidi na ni hao hao wanaoendelea kusumbua Amani ya eneo zima la maziwa makuu!

Ni lazima hatua kali zichukuliwe na kuwaadhibu bila ya kuwaonea aibu!
 
Sheria nyingine bana! yaan watu mnashambuliwa na nyinyi mmekaa tu eti kisa sheria namba 6 inakuzuieni msijibu mashambulizi!!!, jamani huko Darful ni eneo hatar sana, sasa inakuaje mnazikubali sheria za kijinga namna hii?
 
Hivi mpaka idadi inafikia 41 walikuwa wapi kuomba kutumia hicho kifungu cha VII?

Inamaana Kikwete hakuwa anajua kwamba kutatokea majanga kama hayo mpaka sahvi ndo ajifanye kukurupuka?

Alafu Mwanajeshi kuzimia zimia ni udhaifu ukiwa vitani ukaona mwenzako kauliwa si ndo watakuwa wanazimia kila saa??

Rest in Peace our men in uniform.
 
Hivi kwanini kila siku walinda amani wanatoka Tanzania?

Sheria nyingine bana! yaan watu mnashambuliwa na nyinyi mmekaa tu eti kisa sheria namba 6 inakuzuieni msijibu mashambulizi!!!, jamani huko Darful ni eneo hatar sana, sasa inakuaje mnazikubali sheria za kijinga namna hii?
 
Sasa nimegundua kwamba tuliwapeleka ili wafe au walindwe na miujiza ya MUNGU ,kama hawaruhusiwi kujihami(kujilinda) manayake ni kwamba hata silaha inawezekana hawakuwapewi.Huu ni ujinga ni bora tusiwapeleke vijana wetu katika operation kama hizi

Sent from my BlackBerry 9700 using Jamii Forums
 
Hivi mpaka idadi inafikia 41 walikuwa wapi kuomba kutumia hicho kifungu cha VII?

Inamaana Kikwete hakuwa anajua kwamba kutatokea majanga kama hayo mpaka sahvi ndo ajifanye kukurupuka?

Alafu Mwanajeshi kuzimia zimia ni udhaifu ukiwa vitani ukaona mwenzako kauliwa si ndo watakuwa wanazimia kila saa??

Rest in Peace our men in uniform.

Unafikiri kupewa kibali cha chapter 7 ni sawa na kununua ticket za fast jet?
Tanzania tumekuwa tukiomba this for years
uchama usikufanye uponde kila kitu mkuu
 
Sheria na kanuni katika bara la Afrika nying tunatumia zile tulizo rithi toka kwa wakolon, na hao ndio viongiz wakubwa wanao ongoza UN, Sasa watatengua vp? Je mtaungana na mheshimiwa ........... Aliyetengua kile kifungu bungen kwa kusema ...... Kwa yeyote atakae ...... Apigwe? Mheshimiwa JK kampa sapoti PM of TZ. Mungu ibariki Dunia, Mungu ibariki TZ. Amen
 
Back
Top Bottom