Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,487
- 13,612
Kumezuka upendo wa ajabu sana kwa Mama Tanzania katika siku chache za hivi karibuni. Baada ya mtoto wa Odinga kusema kuwa Olduvai Gorge ipo Kenya. Mwanamama kaomba radhi lakini watanzania kama kawaida yetu, tumemsakama kwa kwenda mbele. Tunayo haki, tunapigania kilicho chetu.
Kuna swali moja najiuliza, ikiwa leo hii waliotutawala wakiamua kuifanyia marekebisho mipaka ya kila nchi ambayo waliiweka miaka mingi iliyopita kule Berlin. Tutatumia nguvu hii hii tunayotumia kuitetea Tanzania ya sasa, katika kuitangaza nchi ambayo itakuwa na muonekano mpya kwetu?.
Rasilimali tulizonazo, tumeshaweza kuziwekea mkakati sahihi ili zitufao kwa asilimia angalau 90?.
Tunaufanyia kazi kila upungufu uliopo kwenye sekta ya utalii ili iweze kuboreka na kuongeza pato la Taifa?.
Sehemu kubwa ya kaskazini ya Kenya ni kame lakini sehemu chache yenye rutuba na ubora wa kuitangaza nchi, wenzetu wamehakikisha wanaitumia vilivyo. Sehemu kubwa ya Tanzania inao mvuto mkubwa, je sekta ya utalii ya Tanzania imeweza kuendana na ukubwa wa utalii wetu.
Bila ya kuwa wabunifu kwenye utalii na utunzaji wa mali zetu, tutakuwa walalamikaji wa kudumu. Najua haiwezi kutokea, lakini kama ingewezekana leo hii wazungu wakaibadilisha ramani ya Afrika, pengine hata hizi lawama tunazozielekeza kwa wakenya, zitapoteza umuhimu.