Waliotelekeza viwanda wapewa miezi sita

singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,394
1,536
WAMILIKI wote waliokabidhiwa viwanda vya serikali baada ya kubinafsishwa, lakini wakashindwa kuviendeleza, wametakiwa kuanzia Julai wawe wameanza uzalishaji.
Vinginevyo, wameelezwa kuwa hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
Waziri wa Viwanda, Biashara ya Uwekezaji, Charles Mwijage alitoa tamko hilo juzi mjini hapa baada ya kutembelea na kukagua viwanda vya serikali, vilivyobinafsishwa kwa wawekezaji .
Mwijage alimwagiza Mkurugenzi wa Viwanda wa wizara yake kufuatilia Wizara ya Fedha na Mipango na taratibu mbalimbali za kisheria kwa wamiliki wa viwanda, vilivyofungwa ama kushindwa kuendelea kuzalisha, kabla ya hatua nyingine za kisheria kuchukuliwa kwa watakaoshindwa kutekeleza agizo .
“Viwanda vya mashirika yote ambayo yalibinafsishwa na kupewa wawekezaji, nahitaji kuona vinafanya kazi mwaka ujao wa bajeti Julai 2016,” alisema Mwijage akiwa na Menejimeti ya Kiwanda cha Abood Seed Oil (Moproco).
Alisema lengo la serikali ni kuona viwanda vyote vilivyobinafsishwa na kushindwa kutimiza malengo yaliyokusudiwa, vinafanya kazi za uzalishaji kulingana na maelekezo yaliyomo ndani ya mikataba ili kuwezesha kutoa ajira nyingi za Watanzania.
Alisema mkoa wa Morogoro ni wa uwekezaji wa viwanda na baadhi vilijengwa kutokana na upatikanaji rahisi wa malighafi, zinatokana na sekta ya kilimo .
Vile vile alisema mpango wa ubinafsishaji, ulikuwa ni kutoa fursa pana kwa wawekezaji kutoa ajira nyingi na kuongeza kasi ya uzalishaji wa bidhaa kukuza uchumi, tofauti na ilivyo sasa.
“ Serikali ya awamu ya tano ni ya viwanda na Morogoro ni sehemu iliyopewa kipaumbele cha kwanza cha uwekezaji wa viwanda vipya na kufufuliwa vya zamani, hivyo ni jukumu la wizara yangu kuona viwanda vyote vinafanya kazi kuanzia mwaka ujao wa fedha,” alisema akiwa na viongozi wa serikali mkoani hapa.
Akiwa katika kiwanda cha G&T Shoe ( Moro Shoe Ltd), Waziri alimwagiza Mkurugenzi wa Viwanda wa Wizara, Obadia Nyagilo kuwasiliana na Mamlaka ya Maeneo Huru ya Uuzaji Bidhaa Nje ya Nchi (EPZA), eneo hilo apewe mwekezaji mwingine mwenye uwezo wa kujenga kiwanda .
Moro Shoe Ltd ambacho kinamilikiwa na Guled Shoe Co. Ltd, kiliungua moto kikiwa chini ya mwekezaji huyo na eneo hilo limebaki gofu. Waziri pia aliagiza uangaliwe utaratibu wa namna ya kutwaa kiwanda cha Morogoro Ceramic Wares Ltd na kupatiwa mwekezaji mwingine.
Kiwanda hicho kilichobinafsishwa kwa mwekezaji Pure Bond Ltd, kimefungwa kwa muda mrefu.
Waziri alitaka apewe mwingine mwenye uwezo wa kuendesha uzalishaji wa bidhaa aina nyingine zinazotumia malighafi za ndani. Alisema viwanda vilivyopo Morogoro vinaweza kutoa ajira nyingi kwa wananchi wa Morogoro na nje ya mkoa.
Awali, Mkurugenzi wa Kampuni za Abood, Talal Abood, akitoa maelezo mafupi kwa waziri huyo baada ya kutembelea kiwanda chao cha Morogoro Canvas Mill (1998), ambacho kimefungwa, alisema hakifanyi kazi kutokana na changamoto mbalimbali.
 
Wapewe na mitaji ya kufufulia hivyo viwanda na wahakikishiwe masoko yao yatalindwa dhidi ya bidhaa za mchina zisizolipiwa kodi.
 
Wapewe na mitaji ya kufufulia hivyo viwanda na wahakikishiwe masoko yao yatalindwa dhidi ya bidhaa za mchina zisizolipiwa kodi.
mitaji wapewe na serikali tena serikali haina pesa ya kukopesha wawekezaji kama wameshindwa kukopa bank wavirudishe viwanda wapewe wengine wanaoweza kuviendeshe na wenye mitaji ya kutosha
 
Kupewa mitaji.... No Sir

Masoko kulindwa dhidi ya bidhaa za mchina..... Yes Sir
Sasa wakichukuliwa hatua za kisheria na wakasema wamefilisika watafanywaje?
Kwa kifupi wenye uamuzi wa mwisho ni waliovinunua. Kama vinalipa watavifufua bila shuruti.
 
mitaji wapewe na serikali tena serikali haina pesa ya kukopesha wawekezaji kama wameshindwa kukopa bank wavirudishe viwanda wapewe wengine wanaoweza kuviendeshe na wenye mitaji ya kutosha
Wakivirudisha watapewa hela yao? Na serikali itamuuzia nani viwanda visivyofanya kazi? Hizi ni propaganda za ccm kuendeleza maigizo.
 
Sasa wakichukuliwa hatua za kisheria na wakasema wamefilisika watafanywaje?
Kwa kifupi wenye uamuzi wa mwisho ni waliovinunua. Kama vinalipa watavifufua bila shuruti.

Kwa hiyo serikali inahitaji kuwabembeleza siyo. ......naona unawaza ki Membe Membe. !
 
Kwa hiyo serikali inahitaji kuwabembeleza siyo. ......naona unawaza ki Membe Membe. !
Ni kelele za kisiasa tu hizo mtu alazimishwi kuwekeza asipotaka. Serikali inatakiwa kulinda bidhaa za ndani hapo utaona viwanda vinafufuliwa kimyakimya kwa kasi.
 
Wapewe na mitaji ya kufufulia hivyo viwanda na wahakikishiwe masoko yao yatalindwa dhidi ya bidhaa za mchina zisizolipiwa kodi.
Ndugu unajielewa kweli....Kama hawakuwa na mtaji...uhakika wa Soko LA Bidhaa zao...kwanini...waliiomba Serikali wawape hivyo Viwanda
 
Wapewe na mitaji ya kufufulia hivyo viwanda na wahakikishiwe masoko yao yatalindwa dhidi ya bidhaa za mchina zisizolipiwa kodi.
WENGI WALIOPEWA VIWANDA HIVYO SIO WAMILIKI HALISI WALIOJIPA VIWANDA VIVYO WAPO PEMBENI NDIO MAANA VIWANDA VINGI VIMEBADILISHWA MATUMIZI.VINGINE VIMENG'OLEWA MASHINE NA KUUZWA YAMEBAKI MAGODOWN.SERIKALI LAZIMA ITATHINI JINSI WALIVYOKABIDHI VIWANDA HIVYO NA HALI HALISI YA VIWANDA HIVYO IKIWEZEKANA WAMILIKI HAO WAFIKISHWE KWENYE VYOMBO VYA DOLA KWA UHUJUMU UCHUMI.
 
Ni kelele za kisiasa tu hizo mtu alazimishwi kuwekeza asipotaka. Serikali inatakiwa kulinda bidhaa za ndani hapo utaona viwanda vinafufuliwa kimyakimya kwa kasi.
Mpaka wameingia mkataba wa kuvinunua hivyo viwanda kupitia ubinafsishaji ni kuwa walikidhi vigezo na masharti e.g. wana mitaji ya kutosha kuendesha viwanda hivyo .. lazima wafuate makubaliano waliyosaini na serikali. Cha msingi ni serikali kuweka mazingira rafiki i.e.gharama za uzalishaji kama umeme, kodi, maji ziwe afodabo na bidhaa toka nje zipigwe kodi ya kutosha kulinda viwanda vya ndani..
 
WENGI WALIOPEWA VIWANDA HIVYO SIO WAMILIKI HALISI WALIOJIPA VIWANDA VIVYO WAPO PEMBENI NDIO MAANA VIWANDA VINGI VIMEBADILISHWA MATUMIZI.VINGINE VIMENG'OLEWA MASHINE NA KUUZWA YAMEBAKI MAGODOWN.SERIKALI LAZIMA ITATHINI JINSI WALIVYOKABIDHI VIWANDA HIVYO NA HALI HALISI YA VIWANDA HIVYO IKIWEZEKANA WAMILIKI HAO WAFIKISHWE KWENYE VYOMBO VYA DOLA KWA UHUJUMU UCHUMI.
Waliouziwa nyumba za serikali mbona hawafikishwi vyombo vya dola? Sera iliyotumika kuuza viwanda ilikuwa ubinafsishaji , sasa mali ikishakuwa ya mtu binafsi utampangiaje jinsi ya kuitumia? Viwanda haviendeshwi kisiasa. Unategemea mitsmbo ya miaka 30 iliyopita inaweza kutoa bidhaa za kukubalika soko la leo?
Hizi ni kelele za mwaka mmoja ionekane ilani zinatekelezwa baadae kama kawaida.
Mchina ameshaharibu mazingira ya ya tanzania kuwa nchi ya viwanda.
 
Back
Top Bottom