Sasa ni dhahiri kwamba serikali kupitia NACTE imewanyima nafasi ya kusoma vyuo vikuu wahitimu wa Diploma kutoka vyuo vya mifugo nchini! Hii ni hatari kwa sekta hiyo na wanafunzi hao ambao wanalazimika kusubiri hadi mwakani.
Wahitimu hao ambao wamesoma vyuo vya Tengeru, Mpwapwa, Morogoro, Madaba na kile cha Tanga; mpaka leo hii matokeo yao hayajathibitishwa na NACTE na hivyo hayajaingizwa kwenye mfumo wa udahili kwasababu maofisa wa NACTE hawana nafasi.
Awali nilikuwa nikifuatilia suala hili lakini majibu ya NACTE yalikuwa kwamba hawajapokea matokeo kutoka vyuo husika au kupitia wakala (LITA). Lakini nilipoanza kufuatilia kwa kufika ofisi husika nikianzia na TCU, NACTE, LITA na baadaye NACTE, nimegundua kuwa NACTE ilipokea matokeo hayo mapema mwezi Agosti lakini hadi leo wameshindwa kuitisha baraza lao ili kuyathibitisha na kuyaingiza kwenye mfumo ili wanafunzi waweze kuomba kudahiliwa. Ofisa mmoja wa NACTE niliyezungumza naye jana amenithibitishia kuwa licha ya kupokea matokeo kutoka LITA lakini hawajaitisha baraza lao kuyathibitisha na kuyaingiza kwenye mfumo.\
"Muda hautoshi kuitisha baraza, kuthibitisha matokeo na kuyaingiza kwenye mfumo kwasababu mfumo wa udahili unafungwa kesho (leo)" Na nilipomuuliza hatma ya wahitimu hao alinijibu kuwa kama haiwezekani hadi kesho wasubiri mwakani.... Dah hii ndiyo Tanzania ya Magufuli, huo ndio uwajibikaji. Inakuwaje fani nyeti kama hilo lisipewe kipaumbele mmmmhh.