waliopitia JKT majasusi wa ufisadi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

waliopitia JKT majasusi wa ufisadi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by wakitei, Aug 18, 2011.

 1. w

  wakitei Member

  #1
  Aug 18, 2011
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 77
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Hotuba ya makadrio ya matumizi ya fedha ya wizara ya habari vijana na utamaduni na michezo iliyowasilishwa na Dr Emmanueli Nchimbi ilijadiliwa kwa hisia kali. Jambo ambalo wabunge walipendekeza lirudishwe ni JKT ili vijana wote wakajifunze ukakamavu, ujasiri, na uzalendo.

  Hivi vijana wote waliopitia JKT ni wazalendo kwa nchi yao? Je ni kweli jambo hilo llinawajenga vijana kuthamini nchi yao na kuilinda? Je ni kweli wanaotoka jando hilo ni wakakamavu jasiri na wenye maadili mema? Angalia waliochota fedha za EPA , RADA , MEREMETA , TANGOLD na walioingia mikataba mibovu ya madini je ni nani kati ya hao hakupitia JKT?

  Uzalendo uko wapi wakuanzisha kampuni ya kitapeli kama RICHMOND? Je uzalendo ni kutia ndani fedha kutokana na ubinafsishaji wa shirika la usafiri Dar es salaam ( UDA)? Kuuza ekari 800,000 wilaya ya mpanda ?

  Kwa kuwa watu waliopitia JKT ndio wanaifisadi nchi bila kificho ni sahii kusema JKT imejenga ujasiri wa kifisadi na uhaini.
   
Loading...