Walioondolewa CCM wanyoe/kusuka

m2020

JF-Expert Member
Jul 10, 2016
979
1,353
Nawashauri waamue kunyoa ama kusuka.

Kunyoa ni pale watakapo amua kuendelea na shughuli/bishara zao na kuachana kabisa na siasa.

Na kusuka ni pale watakapoamua kuendelea na siasa kupitia vyama vingine vya siasa.

Ushauri wangu kwao ni kwamba:-

1. Wakinyoa wajue wataendelea na maisha yao raha mustarehe kwani maisha si lazima uwe mwana siasa.

2. Wakisuka wajue wameumia na wameanguka zaidi kwani lazima wataingia kwenye kushindana na mume/mke wa awali mwenye misuli atakaye waangamiza kabisa kisiasa/kibiashara.

Mifano ni mingi ila kwa sasa naishia hapa kwani wale waliojiondoa wenyewe wakati wa uchaguzi 2015 sasa wanajuta wakiwemo wale waliokuwa wasaidizi wa mkuu wa nchi kwa nyakati tofauti kipindi hicho. Hawana jinsi ya kufanya walichagua option no. 2 hapo ndipo walipo wamebaki kuishi kwa matumaini.

Mungu awarehemu na ifahamike kuwa Afrika hakuna wanasiasa bali matapeli wa siasa.

Hawa waliokuwa vinara ndani ya CCM na wafannya maamuzi hawajafanya lolote kwa wananchi je huko upinzani ndo watafanya?

TUIUNGE MKONO SERIKALI YETU AWAMU YA 5. IMESIMAMA VYEMA, INAKIMBIZA NA INATISHA KWA MAENDELEO AFRICA.
 
Back
Top Bottom