Waliomuua Sista Dar Wakamatwa

Waliomuua Sista Dar Wakamatwa

amakyasya

JF-Expert Member
Joined
Jun 26, 2013
Posts
3,480
Reaction score
918
Waliofanya mauaji ya sista wa kanisa katoliki Dar wamekamatwa akiwemo dereva bodaboda.

Source: RFA magazetini leo

======================================

RUTH MNKENI NA JAFARI JUMA (TSJ)
JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limefanikiwa kuwakamata majambazi wawili wanaodaiwa kuhusika kumuua kwa risasi Mtawa wa Kanisa Katoliki Parokia ya Makoka jijini Dar es Salaam, Cresencia Kapuri (50).
Sista Kapuri ambaye alikuwa mhasibu wa Parokia hiyo, aliuawa Juni 23 mwaka huu mara baada ya kutoka benki kuchukua kiasi cha Sh milioni 20 ambazo ziliporwa na majambazi hayo.
Akizungumza na waandishi wa habari jana Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam,

Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova

, alisema majambazi hayo mbali ya kuhusika na mauaji ya mtawa huyo, pia wanahusishwa na tukio la uporaji mali katika Benki ya Barclays Tawi la Kinondoni.
Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Manase Ogenyeka maarufu kwa jina la Mjeshi (35) mkazi wa Tabata Chang'ombe na Hamisi Shaabani maarufu kama Carlos mkazi wa Magomeni.

Alisema majambazi hao wamekamatwa kutokana na operesheni kali inayoendelea jijini Dar es Salaam baada ya kifo cha mtawa huyo.
"Majambazi hawa wawili hatari licha ya kuhusishwa na kifo cha Mtawa wa Kanisa Katoliki na kupora milioni 20 pia tulikuwa tukiwatafuta kwa muda mrefu kwa tuhuma za tukio la uporaji wa fedha katika Benki ya Barclays Tawi la Kinondoni.
"Jambazi Mjeshi alikuwa akiendesha pikipiki akimbeba jambazi mwenzake akiwa na fuko la mamilioni ya fedha na kutoroka nazo na Carlos ndiye aliyekuwa kiongozi wa tukio hilo," alisema Kamishna Kova.

Hata hivyo aliendelea kusema kuwa Jeshi la Polisi bado linaendelea kuwatafuta watuhumiwa wengine wawili waliohusika katika tukio la Sisha.

Aidha alisema mbali na watuhumiwa hao jeshi hilo limefanikiwa kuwakamata majambazi wengine sita ambao ni Beda Mallya (37) mfanyabiashara na mkazi wa Mbezi Msakuzi, Michael Mushi maarufu Masawe (50) mkazi wa Mbezi Makabe, Sadick Kisia (32) mkazi wa Mbagala Kizuiani, Elibariki Makumba (30) mkazi wa Buguruni Madenge, Nurdini Suleiman (40) mkazi wa Buguruni Madenge na Mrumi Salehe maarufu chai bora (38) mkazi wa Kigogo Fresh.
Alisema watuhumiwa watatu kati ya hao sita ambao ni Makumba, Suleiman na Chai Bora walikamatwa baada ya kutumia hati bandia wakiwa wanaomba kazi ya ulinzi katika Kampuni binafsi ya Instant Security Service iliyopo Mtaa wa Makangira Msasani jijini Dar es Salaam.
 
safi sana jeshi la polisi.
 
Hili litakuwa changa la macho.....Kwani we hujui hata aliyemteka na kumpiga Dr. Ulimboka walikamatwa...?
 
Changa liko wapi wewe mpuuzi.Polisi wamefanya kazi kubwa wapewe hongera unaleta ujinga wako!

Kwani lazima utukane...???? Mimi sasa ndo nimesema hiyo ni changa la macho....Wamekamatwa vibaka wazoefu na sio hao majambazi..
 
Kama vile jeshi la polisi limepoteza imani ya wananchi.kifuatacho ni sheria mkononi tu.
 
Kukamatwa-sawa na hukumu yao ni habari ingine. Hatuchelewi wiki ijayo kuwakuta mtaani~!
Ile ya Z'bar ya Padre alepgwa risasi ili-ishia wapi?
 
Aliesema nani

Kuna ya dk ulimboka mpaka Leo sina aamu ati mahakamma Yakana alieletwa sio yeye

Huku alietutangazia mmkubwa kabisa polisi

Mpaka Leo ajaomba mssamaha kuidanganya umma
 
[h=2]Waliomuua Sista wanaswa[/h]

RUTH MNKENI NA JAFARI JUMA (TSJ)
JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limefanikiwa kuwakamata majambazi wawili wanaodaiwa kuhusika kumuua kwa risasi Mtawa wa Kanisa Katoliki Parokia ya Makoka jijini Dar es Salaam, Cresencia Kapuri (50).
Sista Kapuri ambaye alikuwa mhasibu wa Parokia hiyo, aliuawa Juni 23 mwaka huu mara baada ya kutoka benki kuchukua kiasi cha Sh milioni 20 ambazo ziliporwa na majambazi hayo.
Akizungumza na waandishi wa habari jana Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam,
Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova

, alisema majambazi hayo mbali ya kuhusika na mauaji ya mtawa huyo, pia wanahusishwa na tukio la uporaji mali katika Benki ya Barclays Tawi la Kinondoni.
Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Manase Ogenyeka maarufu kwa jina la Mjeshi (35) mkazi wa Tabata Chang'ombe na Hamisi Shaabani maarufu kama Carlos mkazi wa Magomeni.

Alisema majambazi hao wamekamatwa kutokana na operesheni kali inayoendelea jijini Dar es Salaam baada ya kifo cha mtawa huyo.
"Majambazi hawa wawili hatari licha ya kuhusishwa na kifo cha Mtawa wa Kanisa Katoliki na kupora milioni 20 pia tulikuwa tukiwatafuta kwa muda mrefu kwa tuhuma za tukio la uporaji wa fedha katika Benki ya Barclays Tawi la Kinondoni.
"Jambazi Mjeshi alikuwa akiendesha pikipiki akimbeba jambazi mwenzake akiwa na fuko la mamilioni ya fedha na kutoroka nazo na Carlos ndiye aliyekuwa kiongozi wa tukio hilo," alisema Kamishna Kova.

Hata hivyo aliendelea kusema kuwa Jeshi la Polisi bado linaendelea kuwatafuta watuhumiwa wengine wawili waliohusika katika tukio la Sisha.

Aidha alisema mbali na watuhumiwa hao jeshi hilo limefanikiwa kuwakamata majambazi wengine sita ambao ni Beda Mallya (37) mfanyabiashara na mkazi wa Mbezi Msakuzi, Michael Mushi maarufu Masawe (50) mkazi wa Mbezi Makabe, Sadick Kisia (32) mkazi wa Mbagala Kizuiani, Elibariki Makumba (30) mkazi wa Buguruni Madenge, Nurdini Suleiman (40) mkazi wa Buguruni Madenge na Mrumi Salehe maarufu chai bora (38) mkazi wa Kigogo Fresh.
Alisema watuhumiwa watatu kati ya hao sita ambao ni Makumba, Suleiman na Chai Bora walikamatwa baada ya kutumia hati bandia wakiwa wanaomba kazi ya ulinzi katika Kampuni binafsi ya Instant Security Service iliyopo Mtaa wa Makangira Msasani jijini Dar es Salaam.

[h=3]cc maguzumasese2005 OKW BOBAN SUNZU GOOGLE amakyasya[/h]
 
Hizo ni bla bla tuu.Aweke ushahidi au mazingira ya kusema hao ndiyo wanahusika
 
Kama hao majambazi wanafahamika siku zote kwanini waliendelea kuwa uraiani mpaka waue sista ndio eti mnajifanya kuwakamata. Kwa hiyo asingeuwawa sista hawa majambazi wangeendelea kusumbua tu. Polisi bana!
 
ile movie ya yule mkenya aliyemteka ulimboka imeishia wapi kova mm sina imani na habari zake hawa waliokamatwa huenda ni vibaka tuu
 
[h=2]Waliomuua Sista wanaswa[/h]

RUTH MNKENI NA JAFARI JUMA (TSJ)
JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limefanikiwa kuwakamata majambazi wawili wanaodaiwa kuhusika kumuua kwa risasi Mtawa wa Kanisa Katoliki Parokia ya Makoka jijini Dar es Salaam, Cresencia Kapuri (50).

HUU NI USANII WA HABARI AU NI MAELELZO YA KUPAMBA HABARI?

Kichwa cha habari,
MAJAMBAZI YA LIO MUUA SISTA YAKAMATWA.
Maelezo,
Jeshi la polisi limefanikiwa kuwakamata majambazi wawili wanao sadikiwa kumuua sister.

Kichwa cha habari na habari yenyewe vina pishana. Huku wauaji wamekamatwa ,huku wanasadkiwa.
 
Hawana ujanja wa kuwakamata majambazi, wakizidiwa wanakamata wapiga debe wanawapa kesi, mchezo kwisha na wanaendelea kula mshahara na kunywa bia za bei poa.
 
Waliomuua Sista wanaswa
RUTH MNKENI NA JAFARI JUMA (TSJ)
JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limefanikiwa kuwakamata majambazi wawili wanaodaiwa kuhusika kumuua kwa risasi Mtawa wa Kanisa Katoliki Parokia ya Makoka jijini Dar es Salaam, Cresencia Kapuri (50).
Kichwa cha habari na habari yenyewe vina pishana. Huku wauaji wamekamatwa ,huku wanasadkiwa.
Kazi ya POLISI ni kutuhumu
Kazi ya Mahakama inatoa kutoka KUTUHUMU kwenda HUKUMU (ambayo ni kuwatia Hatiani au kuwaachia huru km haijathibitika)
Magazeti hayajakosea tuiachie MAHAKAMA
 
Back
Top Bottom