Waliokosa mikopo elimu ya juu wapewa siku 14!

Informer

JF-Expert Member
Jul 29, 2006
1,582
6,627
WANAFUNZI 1,107 wa masomo ya kipaumbele waliokosa mkopo kutokana na fomu zao za maombi kuwa na dosari, wamepewa muda hadi Novemba 6 mwaka huu, wawe wameshasahihisha fomu hizo. Wanafunzi hao wanaonufaika ni wa ualimu wa hisabati (20), ualimu wa sayansi (164), wanafunzi wa sayansi na tiba (111), uhandisi –umwagiliaji (7), ualimu (617), sayansi ya kilimo(20), uhandisi (70) na sayansi (98).

Taarifa iliyotolewa na Bodi ya Mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) kwenye tovuti ya bodi hiyo, imeonesha kuwa wanafunzi hao wamepewa siku 14 kufanya masahihisho hayo kuanzia Oktoba 24 hadi Novemba 6 mwaka huu.

HESLB imebainisha kuwa waombaji na wadhamini ambao hawakuweka saini zao kwenye fomu hizo, wanatakiwa kwenda wenyewe kwenye ofisi za bodi hiyo kwa ajili ya kufanya masahihisho hayo.

Pia kwa waombaji ambao hawakuambatanisha vyeti vya kuzaliwa, picha, nakala ya hati ya kusafiria au nakala za kadi za mpiga kura za wadhamini wao, wanaweza kutuma nyaraka hizo katika bodi wakiambatanisha na barua inayoonesha jina kamili la muombaji na namba ya cheti za kidato cha nne.

"Nyaraka zote zinatakiwa kuthibitishwa na Kamishna wa Viapo. Bodi inatoa tahadhari kwa waombaji kuwa makini na baadhi ya watu wasiowaaminifu ambao wanaweza kutumia nafasi hii kudai fedha.

"Ifahamike kuwa masahihisho yote yatafanyika nje ya mfumo wa mtandao (OLAS) kwani hakuna dosari inayohusu mfumo," imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.

HESLB itatafuta Sh bilioni 2 kutoka kwenye makusanyo ya wadeni au fedha za matumizi mengine, na Wizara itatoa Sh bilioni 1.1 ili kufikisha Sh bilioni 3.1 zitakazotumiwa na wanafunzi hao huku Serikali ikipanga kukopa vyuo ada ya wanafunzi hao.

Wakati wa udahili wa wanafunzi wa msimu wa masomo wa mwaka 2013 /2014 , bodi ilibaini maombi 6,364 yakiwa yamekosa taarifa muhimu za kuwafanya wapate mikopo.

Baadhi ya vitu vilivyokosekana katika fomu za waombaji ni kukosekana kwa saini ya mwombaji, cheti cha kuzaliwa, picha ya mdhamini, saini ya mdhamini, kukosekana saini ya mamlaka za Serikali za Mitaa na kukosekana kwa saini ya hakimu.

Hata hiyo, pamoja na bodi kutoa nafasi ya kurekebisha fomu kuanzia Agosti 16 hadi 30 mwaka huu, baadhi ya waombaji hawakuweza kusahihisha makosa yao kwa muda muafaka.

HabariLeo - Oktoba 28, 2013
 
Jamani naombeni msaada wenu maana hadi sasa nipo home. Vipi kwa sisi tulioandokiwa NOT ELLIGIBLE Tunafanyaje maana fomu hazijakosewa. Sababu ya kukosa huo mkopo ni kwamba COMPLITED SIX/DIPLOMA MORE THAN THREE YEARS BACK n nilimamiza 2010. Vilevile wengine niliomaliza nao wamepata. Nifanyeje wanajamii?
 
Wapuuzi sana hao jamaa..ukienda mtu ka wewe yaani huna hata vigezo vya kusikilizwa wanadai wanadeal na watu walohitim mwaka 2011, 2012 na 2013 basi..
 
Jamani naombeni msaada wenu maana hadi sasa nipo home. Vipi kwa sisi tulioandokiwa NOT ELLIGIBLE Tunafanyaje maana fomu hazijakosewa. Sababu ya kukosa huo mkopo ni kwamba COMPLITED SIX/DIPLOMA MORE THAN THREE YEARS BACK n nilimamiza 2010. Vilevile wengine niliomaliza nao wamepata. Nifanyeje wanajamii?
Pole sana ndugu! Usikate tamaa, pambana nchi hii ni yako pia
 
Poleni wote tuliokosa mkopo,mimi ni kiongozi wa lile kundi la watu thelathini na 32,tuliokutana na kamati ya maendeleo ya jamii ya Mwenyekiti Mh.Magreth Sitta kuomba na kuishinikiza serikali kutupatia ada ya chuo,tuliangaika sana wiki nne barabarani ila mwishowe ikatolewa bilion 3.1,huwezi amini na juhudi zote jina langu halpo kwa wategemewa wa mkopo,hivyo basi kwa moyo mpya nimeamua kuanzisha harakati nyingine ambayo itawashilikisha wakuu wa nchi hii hadi Mh.Rais,ninaimani sana bodi wanafanya mambo kinyume hawako kwa masilahi ya wanafunzi na umma wapo kwa masilahi yao,hivyo basi kwa yeyote anayejua kuwa suala la yeye kukosa mkopo kwake ni hujuma na hajalidhka na maamuzi ya bodi mfano kupewa sababu feki kama kumaliza shule miaka mitatu nyuma na sio kweli,kutuma fomu ya maombi bodi na yeye kuambiwa hajatuma na wakati una list ya EMS,kutukanwa na wafanyakazi wa bodi kwa aina yoyote ile tafadhali tuwasiliane kupitia 0712177649,tushrikiane kwa ili.HAKI INACHELEWESHWA ILA HAIDHULUMIWI.
 
Haki ya mtoto wa Mkulima lazima ipatikane,haiwezi kupindishwa hata kidogo,
 
Noma san vip fail langu kila cku linabadilika
Nau limeandika Eligible for loan bt burget exhausted
 
Dah nimegundua wabongo hatupendani tunajadili suala la mkpo jamaa analeta issue ya appl.kaka chomoa thread yako sio mahala pake
 
Back
Top Bottom